round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Mtu katoboa kwenye familia, watu wanarundikana kumuomba pesa tena kwajili ya matumizi badala ya mitaji, kukodi mashamba, n.k. Ndio hawa virusi wanafika miaka 40 bado wanaomba pesa, ukiwanyima unatangazwa ukoo mzima unaanza kushambuliwa huwapi pesa ndugu zako, yani wanachojua ni matumizi tu na wapo entitled vibaya mno, wengine wanaenda mpaka kwenye vyombo vya habari kaka yetu kaacha kututumia pesa, khaaa!!
Watu wenye nguvu na afya kujazana kwa ndugu, Eboo! Mnaenda kujazana kwa ndugu yenu bila shughuli za kimaendeleo kufanya nini wakati hali zenu kiuchumi bado hazijakaa sawa ? ohh tunaenda kwa dada yetu kaolewa, ohh naenda kwa kaka yangu kapata kazi mjini, huko wakifika watakaa hapo bila kufanya shughuli za kimaendeleo ? Yani mnamtegea mume wa kaka atoe pesa au kaka atoe pesa, hao watu wameridhika kabisa hawataki kujituma, unamtafutia mtu kazi anaanza kulalamika huko kwenu "ananinyanyasa kanitafutia kikazi cha laki 2 wakati yeye ana pesa nyingi" jamii zinazojitambua haya mambo ya kusalimiana ni wiki 2 top au ukikaa sana basi uwe kwenye shughuli zako kama masomo.
Uwajibikaji mdogo kwenye vitega uchumi kwasababu ya kuwa familia au koo moja, umeamua kupunguza kelele unawaleta ndugu zako kwenye biashara lakini wanaanza kukuharibia, pesa inachukuliwa bila taarifa, garu ya ofisi inatumiwa matumizi binafsi, kuingia ofisini saa nne, kunyanyasa wafanyakazi wengine, n.k. hii yote ni kwasababu "biashara ni ya kaka", entitlement inayoweza kuua kabisa biashara iliyopata jina kubwa kwa jasho la miaka mingi.
Watu kupoteza muda kwenye majungu na umbea – Kuna baadhi ya sehemu vijana kwa wazee wakiamka kutwa nzima ni kushinda vibarazani, vijiweni wakicheza bao, kula kashata na story nyingi sana za kuzungumzia watu badala ya kujadili mawazo ya maendeleo, watu wanapoteza muda wakijadili maisha ya wengine. Majungu hayasaidii maendeleo ya familia wala ya mtu binafsi.
Kujenga uhasama kwa anayefanikiwa – Badala ya kumtia moyo na kujifunza kutoka kwake, wengi wanamchukia na hata kumuharibia jina kwa chuki zisizo na msingi. Watu wanaenda kwa waganga kuroga ndugu zao