Kuna benki unasubiri saa zima kuweka/ kutoa pesa. Ni benki gani ya kuaminika ambayo nitahudumiwa fasta?

Kuna benki unasubiri saa zima kuweka/ kutoa pesa. Ni benki gani ya kuaminika ambayo nitahudumiwa fasta?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kuna benki kadhaa hap nchini imekuwa ni kama utamaduni / mazoea mtu kukalishwa muda mrefu mpala lisaa unasubiri kuweka / kutoa pesa.

Ni kweli mawakala wapo lakini kuna sababu zinatulazimu kwenda bank, mawakala wengi huwezi kuingiza au kutoa zaidi ya milioni 1.

Unaingia Benki, unatoa kikaratasi chako cha kupanga foleni uhudumiwe, Hapo utasugua benchi muda mrefu sana.

Mbaya zaidi kuna madirisha manne lakini ni dirisha moja tu la kuhudumiwa,

Ukienda kuweka zaidi ya milioni 10 mambo ni yaleyale, utaambiwa uende chumba maalum cha bulk lakini kama kuna watu waliokutangulia utasubiri sana.

Nahitaji kuhamia bank yenye huduma za fasta
 
Kuna mawakala kibao tu ml 5 unaweka.
Kwa hiyo kama una 10 unaungaunga kwa mawakala hata watatu unaweka kwa muda mfupi.
Labda shida kwenye kutoa.

Ushauri wa benki ambayo hupangi foleni ni hizi za nje mfano absa, stanbic nk.
Shida hawana matawi mengi nje ya Dsm.
 
Kama upo kwenye miji mikubwa ,nenda Absa , hawana ujinga ujinga
Ila hizi local banks ni Kwa ajili ya waalimu na Watumishi wa halmashauri
 
ebu tueleze mkuu ukiwa na pesa cash mkononi unawekaje online bila kwenda benki au kwa wakala.?
Elewa nilicho kisema hapo pesa za haraka za kutoa na kuweka sehemu ni online tu, ila za mkononi kuzisafilisha lazima sijui upande gari upeleke sehemu husika, kuweka hela sehemu sio mpaka uwe nayo mkononi kuna watu wanahamisha kutoka online kwenda bank hii ndio haina heka heka sijui umenielewa, labda kama unayo mkononi ila vitu vingi sahivi vipo kidigital hata mshahara sipokei cash, hata nikienda dukani siendi na cash mkononi
 
Pia

Dunia inakoenda sasa ni cashless.

Unakuta mtu anatoa milioni 3 anaenda panga foleni benki, kama kwa benki kubwa hizi kuna mawakala mpaka mtaani. Pia kuna mawakala wakubwa unakuta ana hadi limit ya 10m kwa mtu mmoja kutoa..

Hizi channel zimewekwa kuongeza foleni, kuokoa muda na watu kuwa productive kwenye mambo mengine. Kuna mawakala wanafanya 24hrs, kuna benki zina mashine za kudeposit 24hrs.

Nadhani kadri muda unavyoenda tutazoea.
 
Kuna jamaa yangu ye hata laki mpk aenDe ATM NIKIMUULIZA SABABU ETI MAKATO
 
Back
Top Bottom