Kuna brother huku mtaani tangu mwaka 2002 nasikiaga ni mchimba Madini ila hajatoboa kachoka mbaya

Hii inakuaje wazee Kuna broo huku mtaani kwetu Kila mwaka anasafiri kwenda mikoa mbali mbali kuchimba madini tangia mwaka 2002 ndio kazi yake hiyo cha ajabu hakuna alichofanya hata kiwanja Cha hatua 10x10 hana.

Anaishi kwenye upangaji Kila siku kelele na mwenye nyumba Kodi kulipa ni Kwa mbinde bili za umeme na maji anasumbua pia kulipa Kwa shida cha ajabu Kila akirudi kijiweni stori za migodini yaani anazijua a-z yaani kama ameshatoboa.

Mimi namsikilizaga anavyodanganya madogo namuonaga kama Hana akili timamu hivi hii inakuaje wazee umri wake Sasa ni miaka 45 aisee ila familia hata ya mtoto mmoja hana Wala Mali hana yeye ni sigara na pombe sijui uzee wake utakuaje mtu wa dizaini hii
Acha useng£ dogo kilaza wa gen Z ,utafirw@
 
Mkuu sio wachimba madini wote wanafanikiwa.
Hakuna fani au kazi ambayo yeyote yule atakayeifanya lazima afanikiwe .
Maisha ni fumbo mkuu
 
Hii inakuaje wazee Kuna broo huku mtaani kwetu Kila mwaka anasafiri kwenda mikoa mbali mbali kuchimba madini tangia mwaka 2002 ndio kazi yake hiyo cha ajabu hakuna alichofanya hata kiwanja Cha hatua 10x10 hana.

Anaishi kwenye upangaji Kila siku kelele na mwenye nyumba Kodi kulipa ni Kwa mbinde bili za umeme na maji anasumbua pia kulipa Kwa shida cha ajabu Kila akirudi kijiweni stori za migodini yaani anazijua a-z yaani kama ameshatoboa.

Mimi namsikilizaga anavyodanganya madogo namuonaga kama Hana akili timamu hivi hii inakuaje wazee umri wake Sasa ni miaka 45 aisee ila familia hata ya mtoto mmoja hana Wala Mali hana yeye ni sigara na pombe sijui uzee wake utakuaje mtu wa dizaini hii
Ni afadhari aliyechagua kupambana na kutokukata tamaa maan Wakati wa mungu ni wakati sahihi
 
Na uchimbaji unakua kama una ushetani fulani. Ukiaza kuacha inakuwa ngumu sana, unapoteza muda, pesa, unazeeka, ila kitu cha ajabu matumain yanakuwa makubwa

Nilikutana na babu mmoja machimboni (Segese~Ntambalale) ana miaka kama 80 na ushee, akaniambia alianza kuchimba akiwa kijana mdogo, yeye ni mwenyeji wa Morogoro, kwa kifupi kazeekea machimboni, mpaka Msumbiji kaenda akiwa kijana alizaa na mwanamke huko ila hajui hata mwanae yuko wapi, ila yeye anasema anashukuru yuko hai maana vijana wenzie wengine walishafariki na Ukimwi wengine na ajali za machimboni ana imani atapata dhahabu ya kumtajirisha.

Sikia tu habari za dhahabu, ila ingia field uone. Ila ni bonge la experience.
 
Nilikutana na babu mmoja machimboni (Segese~Ntambalale) ana miaka kama 80 na ushee, akaniambia alianza kuchimba akiwa kijana mdogo, yeye ni mwenyeji wa Morogoro, kwa kifupi kazeekea machimboni, mpaka Msumbiji kaenda akiwa kijana alizaa na mwanamke huko ila hajui hata mwanae yuko wapi, ila yeye anasema anashukuru yuko hai maana vijana wenzie wengine walishafariki na Ukimwi wengine na ajali za machimboni ana imani atapata dhahabu ya kumtajirisha.

Sikia tu habari za dhahabu, ila ingia field uone. Ila ni bonge la experience
Asikuambie mtu kutoboa kupitia uchimbaji wa madini ni ngumu sana. Wachache ambao wanatoboa ni wale ambao wanafanikiwa kukuambia na mawe. Madogo weng pale Geita walitoboa kwa njia hiyo, kuna dogo mmoja alifanikiwa kutoroka na mzigo wa mil 500.

Huko Msumbiji nako kuna watz weng sana wamefia huko na wengine wamezeka na hali zao mbaya.
 
madini ni betting na hivi hii sekta ya madini wengi wanaamini uganga yani mtu yupo radhi kumpa mganga milioni 10 atambue kama madini yapo kuliko kumpa hiyo pesa mtaalamu wa jiologia.
Jiologia na mganga wana tofauti gani

Wote wezi tu
 
Nilikutana na babu mmoja machimboni (Segese~Ntambalale) ana miaka kama 80 na ushee,
Dah Hayo ndio maeneo yangu mkuu anzia Segese, Tambalale, Isonda hadi Mwakitoryo namba 2 na 3 Siku zote utanikuta eneo Moja kati ya hizo sehemu nikiwa na vitendea kazi vyangu ponchi na nyundo. Word up!.
 
Ndio Ujue Na Kufahamu Sasa Ya Kuwa Si Kila Ambaye Hajafanikiwa Katika Haya Maisha Ya Kuwa Apambani,,,Maisha Haya Hayanaga Mjanja Hayana Ujanja,,,Ukifanikiwa Wewe Ndio Ujitahidi Kuwainua Wengine Na Si Kuwadharau Na Kashfa Juu...
 
Dah Hayo ndio maeneo yangu mkuu anzia Segese, Tambalale, Isonda hadi Mwakitoryo namba 2 na 3 Siku zote utanikuta eneo Moja kati ya hizo sehemu nikiwa na vitendea kazi vyangu ponchi na nyundo. Word up!.
Niko Geita town mkuu, lakini kuanzia chimbo za Kakola-Bulyankulu kule, namba 9,6, yalikofungwa machimbo nshapita, hadi huku Mgusu, Nyagurusu,Nyamatagata, hadi Nyaluyeye huko nimepita na nikaona harakati za upambanaji.
 
Back
Top Bottom