2021 hapo bakhresa siku ya kwanza kabisa na ya mwisho,tushabwia pombe Kali ya 2000 double kick,nipo na mwanangu kanjo,viroba vya pumba kilo 30 vinashuka kama vinamwaga huko juu,Mimi nikaambiwa niwe kijiko yaani wale wanaowabebesha wengine viroba,mwanangu anabeba viroba akapange stake huko,night Kali kama saa 9 hivi mwanangu kanjo akaishiwa pawa🤣🤣,akaamua aende kule store ya nguo avunje mlango aibe nguo zake atoroke,katika harakati za kuvunja mlango akakutwa na muhindi,basi muhindi akapiga kelele Kwamba ni wizi unatokea hapo,kazi ikasimama kidogo,kufika pale naona mwanangu yupo mtu kati na raia wawili weusi(chawa),wanamwangushia kipigo ikabidi nijitose tu kurusha ngumu collabo na mwanangu,vurumai lilipoisha tukaambiwq tusepe,muhindi akatupa buku 5 tugawane🤣🤣,tukarudi zetu keko kupitia Ile njia ya relini Hadi king palace tukanunua dabokiki zingine,saa 11 tunafika ghetto,asubuhi tumeamka wagonjwa mamaee🤣🤣,maisha haya wacha tu tunenepe mambo ni mengi sana🤣🤣🤣🤣