KERO Kuna changamoto kuhusu Uhalali wa Kumiliki Duka la Dawa Muhimu

KERO Kuna changamoto kuhusu Uhalali wa Kumiliki Duka la Dawa Muhimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mtumishi wa Afya, Afisa Tabibu mwajiriwa wa serikali.

Naomba ujumbe huu uwafikie Baraza la Famasia Tanzania.

Je! Kwanini Mimi mtumishi wa Afya ninapotaka kufungua Duka la Dawa Muhimu, naambiwa Nitafute Cheti cha ADDO au Cheti cha Pharmacy ili niweze kufanya usajili.

Ikiwa mimi nilipoajiriwa nafanya Prescription n.k. huyo mwenye cheti cha ADDO amesoma kuliko Mimi?

Kwanini kusingekuwa na utaratibu wa Kada ya afya kuanzia ngazi ya Stashahada kufanya usajili kupitia vyeti vyake pamoja na Leseni yake ya kazi?

Tunaomba Baraza Husika liangalie upya muongozo ili kusaidia wale wanaokuwa wameona fursa mahali waifanyie kazi, na sio mwajiriwa wa Tamisemi kufa kwa Umaskini sababu ya kuminywa Kila upande.
 
hivi ukiwa na cheti ukapata leseni innabidi wewe mwenye cheti ndo uwe dukani muda wote?
 
Back
Top Bottom