Nilisahau siki kwenye gari kipindi nashuka (nilishukia njiani) baada kama ya dk2 nikakumbuka simu nimeosahau kwenye gari.
So nikapanda boda kuifukuzia ile gari nafika stend kuingia simu sikuikuta wale abiria waliokuwa karibu yangu wameshuka nikamuuliza kinda labda kaachiwa simu akajibu hapana.
Kuipigia inaita tu badae ikawa haipatikani. Nikaenda police chap nikatoa vielelezo hadi Imei nikayoa kila kitu walichohitaji.
Wakaomba jela 70k nikawapa.
Subiri nawewe nitapigiwa simu wapi. Badae nikaenda kituoni kama siku6 zimepita nikaambiwa bado wanaitafuta.
Nikachukua no za police anayeifutilia siku1 napigiwa simu anaomba hela 60k nikampa.
Siku zikapita nikapigiwa simu tena tana anagitaji hela ya mafuta ya pikipiki nikampa 30k
Subiria hamna kitu. Nakuja kusikia jamaa alikamatwa aliyeichukua simu ile (yeye aliuziwa) walipomkata wakampa kesi ya ujambazi kuwa aliyeibwa ile simu walimuibia na milioni 7 !!
Nikaenda kituoni kama sijui kitu kwlei nikaikuta ile simu nikaitambua japo ilikuwa imebadilishwa vitu vingi.
Kuiomba naambiwa bado iko kwenye upelelezi maana walipoiba waliiba na hela nikashangaa sana hela gani sasa kipindi nashuka kwenye gari nilikuwa nashusha bagi na nanasi4 tu nilizokuwa nimenunua.
Baada ya kurudi hata simu haikueleweka iko wapi hapo miezi karibia 2 nikaachana nayo.
Police hawafai kabisa kabisa kbs