Uchaguzi 2020 Kuna dalili zote kuwa endapo kutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, umoja wa Upinzani unaweza kuchukua nchi Oktoba 2020

Same old stories
 
Mkuu nakuunga mkono kwa [emoji817]% tupige kura kwa wingi lkn eti tususe kisa hakuna Tume huru...hilo mi nalipinga...kura zangu ni chadema tu kuanzia diwani hadi rais
 
Endelea Kukariri hivi hivi ukiwadia chaguzi mnashiriki mkishapigwa za uso endeleeni Kukariri tena,wapiga kura hawawezi kupoteza kura zao kwenu wapinga maendeleo
Wapiga kura siyo wajinga wanajua maendeleo ni lazima kwani ni pesa zao za walipa kodi maendeleo siyo Hisani za CCM, wananchi wanajua palipo na wingi wa upinzani Serikali huchelewesha maendeleo kwa makusudi ili kumkomoa mbunge diwani, hizo figisu figisu zote wamezivumilia wakijua ipo siku upinzani utaingia ikulu na kuwafidia machungu yao yote waliyofanyiwa na CCM.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa [emoji817]% tupige kura kwa wingi lkn eti tususe kisa hakuna Tume huru...hilo mi nalipinga...kura zangu ni chadema tu kuanzia diwani hadi rais
Pia ni kuomba mungu wakurugenziccm wasitangaze washindi feki na CCM wasiibe kura kufanya uchakachuaji wowote, washikwe na Ganzi wakitaka kufanya uonevu na uovu.
 
Nachoona ni kwamba "makubaliano" 2020 ipite km ilivyo bila kokoro(maslah yamezingatiwa)... ila harakat zianze baada ya hapo maana "walibip" kwa kuwaondoa wakurugenz ishu ikaonekana inawezekana.... so, harakat zitakoma 2024.... probably nzi akaondolewa 2025....

Ndo nshawaza tayar.
 
Nauliza hivi kuna Mtanzania mwenye akili timamu atapanga stari kupiga kura?
 
Imagine kusingekuwa na ukandamizaji huo sijui ingekuwaje.
Mkuu M-mbabe, "pasingekuwa na ukandamizaji huo" na mambo kadhaa kama ukiukwaji wa sheria na Katiba..., upinzani ungekuwa na hali ngumu sana!

Sijui kama umeliwaza vyema hili!
 
Nauliza hivi kuna Mtanzania mwenye akili timamu atapanga stari kupiga kura?
Wewe na hao wenzako msiopiga kura ndio mnatakiwa kupimwa akili. Nyinyi ndio maadui wakuu wa taifa letu. Nyinyi ndio mnaowahimiza CCM waendelee kuliumiza taifa letu.
 
Dalili kuu ya ugonjwa wa akili ni DELUSIONS
 
Mkuu M-mbabe, nilipokujibu huko juu, nilikuwa sijakusoma huku chini.

Sasa nimekusoma kote, na nina machache:
1. Umesema "kwa bahati mbaya", au sijui kwa kupitiwa tu, au kwa kujua kwamba hawatasikilizwa..., wapinzani hawakuliweka mbele hili swala la Tume Huru.
Kwa kweli inashangaza kwa nini hawakufanya hivyo, au pengine wana mikakati juu yake? Hatujui.

Lakini mimi kama wewe bado nashangaa kwa nini hili hawakulishughulikia kwa nguvu zote.

Ninachoweza kukisia tu kwamba kiliwafanya wasishughulikie swala hilo kwa wakati mwafaka, pengine ni kujua historia na tabia za waTanzania katika maswala kama haya. Hapakuwa na uvuguvugu wowote, na hakuna kiongozi mwenye kuwasha moto ndani ya waTanzania kwa wakati huu.

Kumbuka, Mbowe katiwa kwenye misukosuko mikubwa tokea awamu hii ianze, na hadi kaweka gerezani. Ile kesi iliyomfikisha Segerea na binti Akwilina kupoteza maisha, unakumbuka mazingira yake yalivyokuwa?

Ulisikia sauti toka kokote?

Kama wewe ni kiongozi, na unapata hali ile, utakuwa na moyo wa kwenda mbele zaidi?

Naomba sana unielewe kwa hili hata kama sikulieleza kiufasaha zaidi.

Na uje, CCM, hasa kule juu, wanaisoma sana hali hiyo ya wananchi na ndiyo inayowatia moyo kuendeleza ukandamizaji.

2. "Wasijidanganye sana na mkakati wa kulinda kura."

Hata nami nina mashaka sana kama huo ndio mkakati watakaoutegemea uwape ushind; ila ningeukubali mkakati huo kama watatumia mbinu, na mojawapo ya mbinu hizo ni kuhimiza waTanzania wajitokeze kwa wingi sana kwenda kupiga kura. Ingewezekana kuwatia hamasa wananchi wengi wajitokeze kupiga kura ingesaidia sana kuzuia uharifu wa hiyo tume ya uchaguzi.
Wanapojitokeza wapiga kura asilimia arobaini kati ya waliojiandikisha kupiga kura, inawawia rahisi sana hao watu wa tume kuvuruga uchaguzi.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, njia pekee iliyobakia yenye mategemeo kwa wapinzani ni kufanya kazi kubwa sana ya kuwahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura.

Hii ni kazi inayowezekana mradi wawe wamejipanga vizuri kueleza kwa nini kupiga kura ndiyo njia pekee iliyopo sasa kujikwamua toka kwenye makucha ya wakandamizaji CCM.

Mkuu M-mbabe, sina shaka wewe uliwahi kuwa mwanafunzi. Mfano huu ungependeza zaidi kama ungewahi kuwa mwalimu.
Kama uliwahi kuwa mwanafunzi, halafu mwalimu kwa sababu zake tu akakumiminia mamaksi kwenye mtihani uliojua umefeli, utakuwa unajidai tu wewe kuwa kipanga, lakini moyoni mwako unasutwa na tendo hilo. Hali kadhalika, mwalimu wako atakuwa kila ukikutana naye tendo hilo linamkumbusha aibu hiyo

Wananchi wakijitokeza kwa wingi wao, wakapiga kura zao nyingi kuwapa wapinzani, hiyo tume itapata wapi uthubutu wa kubadili matokeo yaliyo dhahiri?

Licha ya yote; hata wakilazimisha kuwapa CCM ushindi, ushahidi wa kura zote hizo zilizovurugwa utapotezwa vipi?

Wakuu JF hapa huwa hawapendi kuyajibu haya maswali.

Huenda safari hii utanisaidia kupata majibu mkuu wangu M-mbabe.

Halafu kuna watu wanahimizana wasiende kupiga kura, kana kwamba hilo ndilo litawazuia CCM kuendelea na uhalifu wao.
 
Ila we jamaa kwa fix ni mzima sana.. Hivi hiyo tume huru ni tofauti na iliyowapa ushindi kina Qambalo, Mbowe, Matiko na wapinzani wengine? Kubalini mlishajichanganya kwa Lowasa na yaliyofuatia baada ya hapo so hamna mtanzania mwenye akili timamu wa kuwaamini tena.. Vuneni mlichokipanda 2015
 
what is tume Huru? Acha kushikiwa akili, tume huru haisimamiwi Na malaika wa mbinguni, ni jina tu tume huru!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…