Uchaguzi 2020 Kuna dalili zote kuwa endapo kutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, umoja wa Upinzani unaweza kuchukua nchi Oktoba 2020

nakubaliana na arguments zako kwa kiasi kikubwa.

however, huwa naona Watanzania wana utayari wa kushirki jambo endapo kuna mtu anawaongoza na kuwa inspire.

miaka ya 1992 - 1994 ilikuwa ni mapito makubwa sana kwa upinzani lakini watu walikuwa wakiandama kutoka viwanja vya Jangwani kuelekea ikulu na wanapigwa mabomu kabla ya hata kufika Akiba but hicho hakikuwafanya wasitishe maandamano - yalirudiwa tena na tena ma tena.

kosa kubwa la kiufundi ambalo upinzani wa generation ya sasa umelilifanya ni kusitisha maandamano ya UKUTA. pale ndiyo ilikuwa turning point kwani watawala wakagundua wapinzani hawa kumbe ni nyanya tu.

mapambano haya yanahitaji sacrifices lakini pia sidhani kama wadau wetu wa maendeleo wamekuwa engaged vya kutosha na kambi ya upinzani.
 
Endapo kutakuwa na Tume huru ya uchaguzi.
 
Labda kuongeza viti vya ubunge lakini siyo uraisi. Achana na kelele za jamiiforums na twitter ila huko vijijini sana na mkoani watu wanamjua JPM tu kuliko wapinzani.
 
Umegusa sehemu nyeti sana.

UKUTA ilikuwa iwe kiyama cha Tanzania. Gharama yake ingekuwa kubwa sana. Uhai wa watu, ikiwemo wa viongozi wa CHADEMA ungekuwa umetoweka.
Wakati huu tungekuwa nchi tofauti sana.

Katika hili nawasifu CHADEMA kwa uamzi waliofanya wakati huo; ila wakakosa mkakati wa kuendeleza vuguvugu lile kwa njia nyingine.

Mkuu M-mbabe tuseme tu kwamba uamzi waliofanya uliwaruhusu kuishi na kuwa na fursa ya mikakati mingine.

That was going to be a disaster of unimaginable proportions. At least they should be thankful for their decision that allowed them to live and tell a story today.
 
Viongozi wa upinzani wameshazoea kulalamika tu kutafuta huruma za wananchi bila kuchukua hatua stahiki, wanajua kabisa bila tume huru hawawezi kupata haki, Bali kuwafanya wananchi wajinga tu wakati na wao pia wanakubaliana na dola kiaina kusiwe na tume huru. Kwa sasa wananchi wengi wameelewa hawajisumbui tena
 
Labda kuongeza viti vya ubunge lakini siyo uraisi. Achana na kelele za jamiiforums na twitter ila huko vijijini sana na mkoani watu wanamjua JPM tu kuliko wapinzani.
Vijijini wapi hawajui kuwa ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni ufisadi? Vijijini kote kuna mitandao wanajua maovu yote yanayotendwa na CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…