mbenda said
JF-Expert Member
- Apr 13, 2019
- 1,084
- 2,074
Sio wanaokudikiliza wooote wanakuunga mkono
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio wanaokudikiliza wooote wanakuunga mkono
nakubaliana na arguments zako kwa kiasi kikubwa.Mkuu M-mbabe, nilipokujibu huko juu, nilikuwa sijakusoma huku chini.
Sasa nimekusoma kote, na nina machache:
1. Umesema "kwa bahati mbaya", au sijui kwa kupitiwa tu, au kwa kujua kwamba hawatasikilizwa..., wapinzani hawakuliweka mbele hili swala la Tume Huru.
Kwa kweli inashangaza kwa nini hawakufanya hivyo, au pengine wana mikakati juu yake? Hatujui.
Lakini mimi kama wewe bado nashangaa kwa nini hili hawakulishughulikia kwa nguvu zote.
Ninachoweza kukisia tu kwamba kiliwafanya wasishughulikie swala hilo kwa wakati mwafaka, pengine ni kujua historia na tabia za waTanzania katika maswala kama haya. Hapakuwa na uvuguvugu wowote, na hakuna kiongozi mwenye kuwasha moto ndani ya waTanzania kwa wakati huu.
Kumbuka, Mbowe katiwa kwenye misukosuko mikubwa tokea awamu hii ianze, na hadi kaweka gerezani. Ile kesi iliyomfikisha Segerea na binti Akwilina kupoteza maisha, unakumbuka mazingira yake yalivyokuwa?
Ulisikia sauti toka kokote?
Kama wewe ni kiongozi, na unapata hali ile, utakuwa na moyo wa kwenda mbele zaidi?
Naomba sana unielewe kwa hili hata kama sikulieleza kiufasaha zaidi.
Na uje, CCM, hasa kule juu, wanaisoma sana hali hiyo ya wananchi na ndiyo inayowatia moyo kuendeleza ukandamizaji.
2. "Wasijidanganye sana na mkakati wa kulinda kura."
Hata nami nina mashaka sana kama huo ndio mkakati watakaoutegemea uwape ushind; ila ningeukubali mkakati huo kama watatumia mbinu, na mojawapo ya mbinu hizo ni kuhimiza waTanzania wajitokeze kwa wingi sana kwenda kupiga kura. Ingewezekana kuwatia hamasa wananchi wengi wajitokeze kupiga kura ingesaidia sana kuzuia uharifu wa hiyo tume ya uchaguzi.
Wanapojitokeza wapiga kura asilimia arobaini kati ya waliojiandikisha kupiga kura, inawawia rahisi sana hao watu wa tume kuvuruga uchaguzi.
Kwa hiyo, kwa maoni yangu, njia pekee iliyobakia yenye mategemeo kwa wapinzani ni kufanya kazi kubwa sana ya kuwahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura.
Hii ni kazi inayowezekana mradi wawe wamejipanga vizuri kueleza kwa nini kupiga kura ndiyo njia pekee iliyopo sasa kujikwamua toka kwenye makucha ya wakandamizaji CCM.
Mkuu M-mbabe, sina shaka wewe uliwahi kuwa mwanafunzi. Mfano huu ungependeza zaidi kama ungewahi kuwa mwalimu.
Kama uliwahi kuwa mwanafunzi, halafu mwalimu kwa sababu zake tu akakumiminia mamaksi kwenye mtihani uliojua umefeli, utakuwa unajidai tu wewe kuwa kipanga, lakini moyoni mwako unasutwa na tendo hilo. Hali kadhalika, mwalimu wako atakuwa kila ukikutana naye tendo hilo linamkumbusha aibu hiyo
Wananchi wakijitokeza kwa wingi wao, wakapiga kura zao nyingi kuwapa wapinzani, hiyo tume itapata wapi uthubutu wa kubadili matokeo yaliyo dhahiri?
Licha ya yote; hata wakilazimisha kuwapa CCM ushindi, ushahidi wa kura zote hizo zilizovurugwa utapotezwa vipi?
Wakuu JF hapa huwa hawapendi kuyajibu haya maswali.
Huenda safari hii utanisaidia kupata majibu mkuu wangu M-mbabe.
Halafu kuna watu wanahimizana wasiende kupiga kura, kana kwamba hilo ndilo litawazuia CCM kuendelea na uhalifu wao.
Ukiwa kikojozi, halafu kila siku unaficha kwa kutandika shuka jipya, kuna siku godoro nalo litachoka tu."The same old story"
nawahesabu.Ambao ndio unaokusumbua sana wewe, au sio?
Wote ambao mmekuwa mkifutilia rallies za vyama vya upinzani (hapa "upinzani" strictly ninamaanisha ACT & Chadema) hapana shaka mtaafikiana nami kuwa mwamko wa wananchi ku support kambi hii ni mkubwa sana pamoja na uwepo wa vitisho kutoka vyombo vya dola. Imagine kusingekuwa na ukandamizaji huo sijui ingekuwaje.
Ni bahati mbaya sana tena sana kambi hii imeamua kuingia uchaguzini mwaka huu kabla ya kwanza kupigania Tume Huru ya Uchaguzi. Ni bahati mbaya sana kwa sababu japo watashinda kwa sehemu kubwa (>55% kwenye urais na >60% ubunge & madiwani), hawatatangazwa.
Wasijidanganye kabisa na mkakati wa eti "kulinda kura" baada ya polling. Wakifanya hivyo tutakuwa tumeamua kumkabidhi ziraili roho za akina Aquiline nyingine nyingi tu. Endapo "kulinda kura" ndiyo utakuwa msimamo, basi viongozi wa upinzani lazima watambue kuwa there'll be a huge price to pay, and dearly. Suala ni je upinzani umejipangaje ku mitigate hili tishio?
Those are only my 2 cents. Food for thought.
Usisahau kupitia video clip hii hapa chini ili uelewe context ya uzi wangu.
Umegusa sehemu nyeti sana.kosa kubwa la kiufundi ambalo upinzani wa generation ya sasa umelilifanya ni kusitisha maandamano ya UKUTA. pale ndiyo ilikuwa turning point kwani watawala wakagundua wapinzani hawa kumbe ni nyanya tu.
mapambano haya yanahitaji sacrifices lakini pia sidhani kama wadau wetu wa maendeleo wamekuwa engaged vya kutosha na kambi ya upinzani.
Anza kujihesabu mwenyewe ukiwa namba moja.nawahesabu.
Endeleeni kujitokeza.
Vijijini wapi hawajui kuwa ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni ufisadi? Vijijini kote kuna mitandao wanajua maovu yote yanayotendwa na CCMLabda kuongeza viti vya ubunge lakini siyo uraisi. Achana na kelele za jamiiforums na twitter ila huko vijijini sana na mkoani watu wanamjua JPM tu kuliko wapinzani.