Kuna dawa ya kienyeji ya kutibu ugonjwa wa kisukari?

Kuna dawa ya kienyeji ya kutibu ugonjwa wa kisukari?

SHIGOTTO

Senior Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
156
Reaction score
282
Ndugu zangu wapendwa nawasalimu wote! Niliamua kwenda kwenye moja ya hospitali zetu hapa jijini kwa ajili ya kuangalia afya! Nilitaka kujuwa afya yangu kwa ujumla kuanzia pressure,sukari,ukimwi na n.k.

Baada ya kufanyiwa vipimo ikaoneka sukari yangu iko juu kuliko matarajio hivyo nikaambiwa nirudi kesho yake ili nipimwe tena kabla ya kula.

Hata hivyo sukari ilionekana kuwa 8.4 kabla ya kula. Doctor akanipatia dawa (vidonge vyeupe) kwa description ya kula 1*2, nimetumia siku moja kwa maana nilipata ushauri wa pili ya kuwa nijaribu ku control diet na kufanya mazoezi.

Hata hivyo kuna watu wameniambia naweza pia tibia hiyo hali kwa dawa za miti shamba. Sasa nauliza je kuna mtu anafahamu ya kama kuna dawa zinazosaidia ku control au kutibu tatizo hili?

Napenda kuwakilisha.
 
Jiangalie kwenye chakula chako unachokula na fanya mazoezi kila siku (Hasa nyakati za asubuhi) ndio dawa kubwa ya sukari. Dawa za mitishamba na hospital sio nzuri kwa afya yako, kwasababu;

1) Unapoanza kuzitumia dawa za hospital, baada ya muda mchache mwili wako hautaweza kupambana na sukari bila msaada wa hizo dawa. Mwili utakua unahitaji msaada wa hizo dawa ili uweze kupambana na sukari, mwili wenyewe kama wenyewe itafikia hatua hauwezi kupambana na sukari bila msaada wa hizo dawa, hii itapelekea dose ya dawa kuwa inaongezeka kila baada ya miaka (Kama utaanza na kidonge 1 kwa kila siku, itafikia unakunywa kidonge 1 kila baada mlo, na itafikia hatua vidonge havifanyi kazi hivo itabidi utumie sindano ya dawa).

2) Dawa za mitishamba (Kienyeji) kuna baadhi ya mwili huwa zinakubali vizuri, ila kuna baadhi ya mwili zinakataa. Pia kuna dawa za mitishamba ni kali sana kupelekea kuua maini na figo yako.

Mazoezi na kujiangalia kwenye ulaji wa chakula ndio dawa kubwa, mwili unapofanya mazoezi (Hasa ya kukimbia au kutembea urefu wa mbali) huchoma sukari na mafuta yasiohitajika ndani ya mwili wako, pia mwili hutokwa na jacho linaloambatana na chumvi sambamba na mzunguko wa damu mwilini kuongezeka.

Pia kunywa maji mengi kwa siku, atleast 2.5 littres (Lita mbili na nusu) au zaidi.

Usiogope wala usijitishe mkuu, sukari kuwa 8.4 sio hatari kama unavyofikiria. Ukipiga mazoezi ya kukimbia week mbili na kunywa maji mengi tu hio sukari inakaa level vizuri sana.
 
Ukiona dawa haipo hospital ujue mabeberu imewashinda ata miti shamba hamna. Maana hizi dawa za hospital zinatokana na miti, fungi, genetic engineering (chanjo) n.k
 
Pole, km hutojali, nione PM nikupatie namba ya mtaalamu wa magonjwa hayo akupatie Tiba. Yuko Mbeya kwa Sasa.
 
8.5 sio mbaya kihivyo ila inaweza pia kupanda zaidi. Zingatia zaidi diet na mazoezi kama mdau hapo juu alivyokushauri. Binafsi ninayo na niliamka najisikia ovyo ila nijilazimisha sn kutokutumia vidonge. Hapa muda huu ninaingia ktk garden yangu kujitoa jasho kidogo
 
Kunywa juice ya karela (Bitter Gourd) mara kwa mara; ni chungu sana ila inasaidia sana
 
Fuata ushauri wa wataalam kuhusu diet na mazoezi....Je ushaanza kuonyesha dalili za sukari?
 
Kama unataka kuuliza kujua kama kuna dawa ya kienyeji au ya kisunna ya kutibu ugonjwa wa kisukari . Hizo dawa zipo na zimesaidia wengi. Ni imani yako kama unahitaji nakupa Tiba ya kisunna na inakusaidia. Ukitaka maelezo zaidi . tuwasiliane.
 
nimepimwa mara mbili inaonyesha iko above 8 ndo naona ni dalili za awali
Mcheki huyu[emoji116][emoji116]atakusaidia
Kuna dawa za Asili ya kukutibu maradhi ya kisukari kwa muda wa miezi 3 utapona kabisa maradhi yako nitafute kwa wakati wakonipate kukutibia maradhi yako.
Dawa za asili za kisukari zipo ndugu na unapona kabisa.
 
MwananguWee .. usijaribu kutapatapa na kuchukuwa ushauri wa mitaani... achana nao!!
Nakutahadharisha.

Gonjwa la Kisukari kinahijitahi kuheshimiwa na kufuata maelekezo maalum ya Dokta mtaalam.!!

Cha msingi tumia njia za miiko (ya vyakula na tuache kuendekeza nafsi, matamanio na ulafi)
Fanya mazoezi ya kutembea daily dkk.45.

Pole na Good Luck
 
Kuna dawa za Asili ya kukutibu maradhi ya kisukari kwa muda wa miezi 3 utapona kabisa maradhi yako nitafute kwa wakati wakonipate kukutibia maradhi yako.
Kuwa makini sana na kila unachoambiwa, Mama aliambiwa ndani ya miezi 6 atapona kabisa na kuelekezwa kutofuata masharti hasa ya vyakula na kutopima kabisa sukari.

Mwisho wa siku hali ilikuwa mbaya zaidi, na Daktari alikuwa mkali sana alipofuatwa baada ya kuwa amepiga pesa ndefu. Hivyo za kuambiwa ongeza na za kwako chukua dawa lkn tahadhali na masharti ya vyakula muhimu sana kufuatwa
 
Uwe makini sana, unaweza kupoteza muda , pesa, kuharibu viungo na hata uhai,

Kama uko chini 45 yrs na uzito usiozidi 65 kg, umbo la kwawaida, unaweza kuiarisha sukari hadi miaka 10 (makisio tu) kwa mazoezi bila kuacha pamoja na ratiba thabiti ya ulaji BORA,

Zaidi ya hapo ni hatari hayo mengineyo ni bora kuanza dawa hata kwa dose ndogo sana LAKINI HAKIKISHA UNAPIMA ikiwezekana kila siku, vipimo ndio vitaamua kuendelea na dawa au laa
 
Back
Top Bottom