KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
PEP-HIV-Treatment-Medication-11.jpg

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na masuali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Tunachokijua
Njia ya kukukinga usipatwe na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira au hali hatarishi ipo. Kitaalamu huitwa Post-exposure prophylaxis, au kwa kifupisho PEP.

Kwa mujibu wa Miongozo ya Matibabu na Orodha ya Kitaifa ya Dawa Muhimu Tanzania Bara iliyotolewa na Wizara ya Afya mwaka 2021, PEP ni utumiaji wa haraka wa dawa ili kuzuia maambukizi kufuatia mazingira ambayo mtu anadhani yanaweza kumsababishia kupata maambukizi ya VVU (Mfano: kugusana kwa damu au maji maji mengine ya mwili).

PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi.

Mtu aliyepitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe VVU anapaswa kufika kwenye hospitali yoyote ya serikali ili apatiwe msaada, pamoja na kupimwa kwanza kama tayari ni muathirika wa VVU au la.

Dozi ya mwanzo inapaswa kutumiwa ndani ya saa 2 baada kuhisi kuambukizwa na kabla ya kumpima mtu mwenye mashaka.

Kwa Tanzania, TDF 300mg+3TC 300mg+DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD ndiyo dozi ya dawa inayotumika kwa watu wazima. Kwa watoto, AZT+3TC+LPV/r ndiyo hutumika.

Muongozo huo wa Wizara pia unaonesha kuwa dozi hiyo hutumiwa na watu wazima kwa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28, huku kwa watoto ikitumiwa mara mbili kwa siku katika muda wa siku hizohizo 28.
Kikubwa watu wazingatie kuwahi mana kadiri muda unavozidi kwenda ndivyo chance ya kupona inapungua kama dawa za kuzuia kushika ujauzito tu
View attachment 2333560

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Huhitaji kujua kama dawa ilifanya kazi.

Matumizi yake ni kuzuia virus washindwe kuzaliana kwenye mwili wako na hivyo kuzuia usipate HIV

Unatumia hii kwa tahadhari ikitokea umekua katika hatari ya maambukizi, huwa hakuna nafasi ya kupima kujua kama umepata virusi sababu vipimo havionyeshi maambukizi katika muda wa siku 3. Na ukkisubiri muda upite ukikuta uliambukizwa PEP haitafaa tena, utaishi hivyo maisha yote
Unaweza kutumia PEP zaidi ya mara moja?
 
Mbombo ngafu. Tujitahidi kuacha michepuko. Imagine starehe ya dakika tano halafu unakunywa PEP kwa siku 28. Nyumbani kumenoga jamani. Turudi nyumbani.

Kwa mfano maduka mengi ya madawa hayana hii PEP ama hayana air condition hivyo dawa ku expire kirahisi au ukute pep yenyewe ya Burundi yaani feki.
Lkn pia uhonge elfu kumi starehe ya dkk tano gharama za pep elfu hamsini.

Turudi nyumbani.
dk5 kivipi mkuu?
 
Hakuna Jibu la Moja kwa Moja kuwa PEP imefail ila kama Ikitokea Ukapata Maambukizi na kwa bahati mbaya Ukaathirika Kutokna na Sababu mbalimbali..Ik8wa ni Pamoja na Kuchelewa Kuanza PEP..
Vipimo vitasoma Positive...

Ushauri wangu, Jitahidi Kuanza PEP mapema Atleast Stat pack ya Ndani ya Masaa mawili na isizidi masaa 72

Mkuu katika uzoefu wako uliishawahi shuhudia mtu aliyeanza dose baada ya masaa kama 50 na mwisho akaja kubaki negative?
 
Back
Top Bottom