Kuna demu analalamikia wazazi kwa kumsomesha

mlisha

Member
Joined
Aug 23, 2026
Posts
23
Reaction score
42
Huyu demu anasema kabla ya kwenda chuo ndoto yake ilikuwa ni kuolewa na mwanaume ambaye walipendana sana na wakati huo Huyo demu alikua anajishughulisha na biashara ya miamala

Sasa anasema wazazi wake walimshauri asome, kitu ambacho kwa upande wake haikua ndoto yake. Tena anasema yeye alitaka kudili na biashara ya miamala na kuolewa basi.

Anasema baada ya kwenda chuo biashara yoke ilikufa na pia mchumba wake waliachana ,na huko chuo alirudi na mimba na kwa hali ilivyo ajira ni kipengere ,anajutia sana uamzi wa kwenda chuo kwa shinikizo la wazazi
 
Shida siku hizi wazazi wanafosi kila mtoto asome, kitu ambacho hakina uhalisia.

Ndiyo maana China siyo kila mtoto anakuwa na vigezo vya kwenda chuo, kuna li mtihani lao hilo huwa wanafanya kila mwaka, usipofaulu hakuna kwenda chuo, mkafanye shughuli zingine.
Ni kweli kabisa anasema kabla ya kwenda chuo mambo yake yalikua vizuri
 
Huyo Binti anatatizo la kutokujaji matokeo.
Ulitaka kusema kujaji kwa maana kwamba akae chini ajiulize hatua aliyopo akubaliane na hali kisha aendelee na maisha au ulimaanisha kujali kwamba wazazi wake pamoja na kumpotezea muda mwingi kwa kitu asichokitaka aendelee kuwashukuru?

Personally,naamini ktk uhuru wa mtu kujiamulia kama tayari binti alishajichanganya mtaani akaona anasogea ilikuwa haina haja kukimbizana nae habari za chuo sijui kuongeza elimu elimu yenyewe hii ya Tanzania isiyomsaidia msomi.
 
Huyu demu anasema kabla ya kwenda chuo ndoto yake ilikuwa ni kuolewa na mwanaume ambaye walipendana sana na wakati huo Huyo demu alikua anajishughulisha na biashara ya miamala ,sasa anasema wazazi wake walimshauri asome ,kitu ambacho kwa upande wake haikua ndoto yake Tena anasema yeye alitaka kudili na biashara ya miamala na kuolewa basi. Anasema baada ya kwenda chuo biashara yoke ilikufa na pia mchumba wake waliachana ,na huko chuo alirudi na mimba na kwa Hali ilivyo ajira ni kipengere ,anajutia sana uamzi wa kwenda chuo kwa shinikizo la wazazi
Wazazi walizaa binti MPUMBAVU.
Huko chuoni alienda kusoma au kutafuta mimba?
 
Huyu demu anasema kabla ya kwenda chuo ndoto yake ilikuwa ni kuolewa na mwanaume ambaye walipendana sana na wakati huo Huyo demu alikua anajishughulisha na biashara ya miamala ,sasa anasema wazazi wake walimshauri asome ,kitu ambacho kwa upande wake haikua ndoto yake Tena anasema yeye alitaka kudili na biashara ya miamala na kuolewa basi. Anasema baada ya kwenda chuo biashara yoke ilikufa na pia mchumba wake waliachana ,na huko chuo alirudi na mimba na kwa Hali ilivyo ajira ni kipengere ,anajutia sana uamzi wa kwenda chuo kwa shinikizo la wazazi
Kwa hiyo wazazi wake ndio waliompa mimba?

Kwani hivi haiwezekani kusoma huku ukifanya biashara?

Kwani haiwezekani ukaolewa na ukaendelea na chuo, au ni chuo cha ngazi gani?

NB: mke wangu nimeoa akiwa mwaka wa pili chuo
 
Shida siku hizi wazazi wanafosi kila mtoto asome, kitu ambacho hakina uhalisia.

Ndiyo maana China siyo kila mtoto anakuwa na vigezo vya kwenda chuo, kuna li mtihani lao hilo huwa wanafanya kila mwaka, usipofaulu hakuna kwenda chuo, mkafanye shughuli zingine.
Una kuta mzazi ana watoto 6 wote ana lazimisha waende shule wafike mpka chuo 😄
 
Ulitaka kusema kujaji kwa maana kwamba akae chini ajiulize hatua aliyopo akubaliane na hali kisha aendelee na maisha au ulimaanisha kujali kwamba wazazi wake pamoja na kumpotezea muda mwingi kwa kitu asichokitaka aendelee kuwashukuru?

Personally,naamini ktk uhuru wa mtu kujiamulia kama tayari binti alishajichanganya mtaani akaona anasogea ilikuwa haina haja kukimbizana nae habari za chuo sijui kuongeza elimu elimu yenyewe hii ya Tanzania isiyomsaidia msomi.
Kwa upande wa malezi mzazi huwa anajitahidi kumalizia malezi yake, yaani kulea mtoto on his best ways, not a child desires, sasa hio inapelekea watoto wengi hasa wa kike wanapopevuka kushindwa kuhold misisimko ya mwili na kupelekea kujiamulia bila ya kujali kuwa Bado wako chini ya ulezi wa wazazi , hii inapelekea hata wakija kuolewa hawawezi kuhimili misisimko ya ndoa 😁😁 especially kuwa na utii wa kiafrika
 
Una kuta mzazi ana watoto 6 wote ana lazimisha waende shule wafike mpka chuo 😄
Enzi zetu ilikuwa ni juhudi ya mtoto, ukifaulu wanakupeleka hatua ya mbele, ukifeli basi wanakukaribisha mtaani uendelee na maisha mengine.

Au laah, unapelekwa kwenda kusomea vyuo vya kati upate ujuzi wa kuanzia maisha yako. Na hapo uwe umeonesha nia kweli kweli. La sivyo hakuna mwenye muda na wewe.

Yani ni hakuna kubembelezwa!
 
Anasema kusoma haikua ndoto yake ni shinikizo la wazazi
Ndoto ni kusomea alichotaka ila wazazi wakalazimisha asome wanachotaka wao.

Hii ni funzo kubwa kwa wazazi ili kesho mtoto asikulaumu...

Mwache mtoto asome kitu cha ndoto yake
 
Kwa hiyo wazazi wake ndio waliompa mimba?

Kwani hivi haiwezekani kusoma huku ukifanya biashara?

Kwani haiwezekani ukaolewa na ukaendelea na chuo, au ni chuo cha ngazi gani?

NB: mke wangu nimeoa akiwa mwaka wa pili
 
Back
Top Bottom