Kuna familia zinauza bangi / gongo mitaani toka zamani mpaka watoto wamerithi, hili linawezekana vipi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264



Kuna nyumba zimezoeleka miaka nenda rudi kuuza bangi na gongo mitaani, hadi sasa ukienda zinaendelea, unaweza kukuta watoto ndio wanaoziendeleza baada ya wazazi wao kustaafu.

cha ajabu mapolisi wapo, na tena huwa wanabadilishwa wanakuja wengine wapya.

Wote tunajua kuuza huu mmea ama gongo kunaweza mpeleka mtu jela lakini hizi familia zinafanya haya mambo wazi wazi bila kificho, wewe ukiiga unakuta baada ya masaa kadhaa tu umeshughulikiwa

hawa wauza gongo na bangi wana survive vipi
 
wanakula na wakubwa. Me kuna raia namjua mara kadhaa uwa anakamatwa na polisi ila haichukui siku 3 yupo mzigoni.
 
wanakula na wakubwa. Me kuna raia namjua mara kadhaa uwa anakamatwa na polisi ila haichukui siku 3 yupo mzigoni.
mkuu, lakini hao mapolisi huwa wanabadilishwa sana maeneo ya kazi
 
Connection, sio hao tu kuna wale malaya wa kihaya kila ikipigwa ambush hakamatwi hata mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…