Kipindi fulani nilikua nafanya kazi bandarini Dar. Pale Kuna ma shed mengi kuanzia shed number moja Hadi namba 8 lkn pia Kuna MP shed, BPD, LW9 n.k.
Mimi nilikua MP shed na pale ndio walipokua wanapokelea nyama ya mbuzi ya Bakwata kutoka uarabuni ikija kwa meli maalum. Waislamu wa Bakwata sio watu wabaya, wakija kuchukua nyama Yao na sisi wafanyakazi wa bandari tunaambulia kilo tano au zaidi.
Baasi bwana, kipindi kile Mimi Ni senior bachelor nakaa nyumba ya kupanga. Kipindi kile hakuna eti apartment self, kulikua hakuna huo ujinga. Ilikua nyumba ya vyumba sita, korido katikati uani Kuna jiko mabafu na chumba kimoja au viwili.
Mimi nilikua nakaa chumba Cha ndani. Mwenye nyumba chumba Cha mbele. Kuna siku nilipewa nyama nyingi tu na ndugu zangu wa Bakwata, na Mimi kufika nyumbani nikaamua kuwagawia wake za wapangaji wenzangu kwani Mimi nisingeweza kuila yote na hata friji Sina kipindi kile.
Eebwanae, Kuna mwamba alirudi akakuta mke wake amepika Ile nyama na kujiunga kwa Nazi na wali wa nguvu.
Swali la kwanza la jamaa kwa mkewe Ni NYAMA TAMU NAMNA HII UMEITOA WAP?Alipoambiwa imetoka kwangu, siku tatu nyingi. Jamaa alihama Ile nyumba.