Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha


Ilo la bei yeye kaambiwa 10k wewe unasema 15k.

Kama unaona aliambiwa ndogo kata rufaa
 

Watu wa kada gani ambao hawatakiwi kujua kiingereza?

Dunia ya sasa hivi hujui ya kesho hivo ni vizuri ukajua mapema
 
Kuna siku Mjerumani alinikimbia kwenye tafrija fulani kisa hajui English,angejua English yangu ilivyokuwa ya kuunga unga hasingekimbia.Nami kwa kutaka sifa nikawa namfuata kila Angle aliyokuwa anaenda kusimama.
 
 

madereva wote wa teksi dar airport hawawezi kuongea kingereza hivyo. Acha kudhalilisha lugha ya kiswahili na utu wako.
 
Dunia nzima sasa wanajitahidi kujifunza lugha aina nyingi na nchi nyingi sasa ni compulsory kujifunza lugha zaidi ya moja shuleni ni baada ya vita vingi na pia kupamba kwa biashara duniani. Kujifunza lugha ni vizuri kwani utaelewa mengi binafsi naongea lugha nne kubwa mbali na kiswahili. Lakini mmarekani kutojua hata cha kuombea maji mi hainiingii akilini either ni mzee sana ambae haendi na wakati I mean technology kushindwa hata kujua kuuliza shilingi ngapi. Unakwenda nchi ngeni unakodisha gari airport ina navigation system you just drive to your destination. Utanawazi bwana simlaumu dereva alikuwa taxi bubu
 
Kwa wanaojua nasikia huwezi pata visa ya uk au usa kama hujui kingereza ni kweli?. Mbn wao wanakuja ilhali hata neno jambo hajui?.
 
 

Kwa upande Wangu Mimi naona mzungu ndiyo mshamba kwa sababu huwezi kwenda ujerumani au ufaransa ukategemea watakuongelesha kizungu. werevu hujifunza japo maneno machache kwanza ya sehemu waendako. zikiwamo slang. mzungu katuaibisha sana na si taxi driver
 
Watu wa kada gani ambao hawatakiwi kujua kiingereza?

Hata tusiende mbali sana, rejelea sifa za Mtanzania anayeweza kuwania kiti cha Ubunge.

Dunia ya sasa hivi hujui ya kesho hivo ni vizuri ukajua mapema

Ni kweli kuwa kesho inaanza leo, lakini wapo wengine ambao kesho yao ni kama leo.
 
Kwa wanaojua nasikia huwezi pata visa ya uk au usa kama hujui kingereza ni kweli?. Mbn wao wanakuja ilhali hata neno jambo hajui?.

Kupata visa siyo lazima ujue english ukifika ubalozi unaulizwa unataka interview kwa kiswahili au english.

Binafsi na ndugu zangu wengi ambao hawajui english zaidi ya ok na yes lakin wamepata visa
 
Uongo huo maana bei haitoi picha halisi ya gharama ya taxi kutoka airport to city centre, kichekesho chako ungekifanya kiendane na hali halisi

Na we umeligundu hilo. Inabidi wawe wanafikiria kabla ya kupost. Kwanza hakuna dereva tax airport ambae ajui hii lugha ya akina thank you ya kutajia bei
 
Na we umeligundu hilo. Inabidi wawe wanafikiria kabla ya kupost. Kwanza hakuna dereva tax airport ambae ajui hii lugha ya akina thank you ya kutajia bei

Nani alikwambia ni airport ?acheni kujitungia mambo yenu
 
nisawa kutojua kiingereza waje nawakalimani wao nasi tupate ajira afu nadhani uyo mzungu alikua nania yakumtapeli mtz. mwenzetu amekuja kutalii na ametembea nch kadhaa za afrika mashariki hajui hata kiswahili lugha inayo kua kwa kasi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…