Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha

Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha

Hata wewe mwenyewe kiswahili kinakushinda, katika paragraph ya pili "............kiasi gani dereva teksi hakajibu...." unamaanisha nini unaposema hakajibu

Pili wasema rafiki yako alikuwa anakwenda katikati ya mji, kutoka Ubungo kwenda city centre ni Tshs 15 - 18 Thousand, unasema toka ubungo kwenda sinza, tangu lini sinza imekuwa katikati ya mji?

Ilo la bei yeye kaambiwa 10k wewe unasema 15k.

Kama unaona aliambiwa ndogo kata rufaa
 
Umuhimu wa lugha hutegema na uhitaji wa matumizi ya hiyo lugha...

Kuna watu wa kada fulani kujifunza na kufahamu Umombo ni muhimu lakini kuna watu wa kada nyingine si muhimu...

Hivyo huwezi hitimisha kwa kuandika "Kiingereza ni muhimu" pasipo kutaja kwa makundi au kada zipi...

Kiongozi lazima akomalie lugha ya Taifa lake, hii ni sehemu ya utamaduni wetu na ni urithi wa Utaifa wetu.

Sijui kama umeshawahi kujifunza sifa za Taifa kuwa ni lazima wawe na lugha inayowatambulisha??

Watoto wao wanasoma shule hizo kwa kuwa wanahitaji kujua lugha hiyo, la hasha si lazima uende shule hizo ili ujue kwa uzuri lugha ya Umombo.

Nimekuelewa na na hata hiyo sentensi uliyoiandika kama hitimisho nimeiona...

Sijaipa uzito kwa kuwa karibu 90% ya habari yako umesisitiza umuhimu wa lugha ya Umombo...

Watu wa kada gani ambao hawatakiwi kujua kiingereza?

Dunia ya sasa hivi hujui ya kesho hivo ni vizuri ukajua mapema
 
Kuna siku Mjerumani alinikimbia kwenye tafrija fulani kisa hajui English,angejua English yangu ilivyokuwa ya kuunga unga hasingekimbia.Nami kwa kutaka sifa nikawa namfuata kila Angle aliyokuwa anaenda kusimama.
 
Hivyo huwezi hitimisha kwa kuandika "Kiingereza ni muhimu" pasipo kutaja kwa makundi au kada zipi...

Kiongozi lazima akomalie lugha ya Taifa lake, hii ni sehemu ya utamaduni wetu na ni urithi wa Utaifa wetu.

Sijui kama umeshawahi kujifunza sifa za Taifa kuwa ni lazima wawe na lugha inayowatambulisha??"

End of qoute:-

Nilishazungumza hapa JF, Watanzania tunajifanya kama mbuni.
Tuna tabia ya kutia kichwa kichakani wakati mwili wote uko nje.... na kujiona eti tumejificha!

Wengi tunazungumza na kuandika Kiswahili kibovu kabisa! Kiingereza hatukijui si kwa kupenda wala uzalendo, bali ni kwa mfumo mbovu wa elimu ulioanzwa na Mwl. Nyerere kwa faida zake za kutaka umaarufu wa kisiasa.

Sisi ndio ma mbumbumbu wa Afrika Mashariki, na si kwa lugha tu.
 
Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia Tanzania leo kuja kutalii, ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda, kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.

sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.

Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

madereva wote wa teksi dar airport hawawezi kuongea kingereza hivyo. Acha kudhalilisha lugha ya kiswahili na utu wako.
 
Dunia nzima sasa wanajitahidi kujifunza lugha aina nyingi na nchi nyingi sasa ni compulsory kujifunza lugha zaidi ya moja shuleni ni baada ya vita vingi na pia kupamba kwa biashara duniani. Kujifunza lugha ni vizuri kwani utaelewa mengi binafsi naongea lugha nne kubwa mbali na kiswahili. Lakini mmarekani kutojua hata cha kuombea maji mi hainiingii akilini either ni mzee sana ambae haendi na wakati I mean technology kushindwa hata kujua kuuliza shilingi ngapi. Unakwenda nchi ngeni unakodisha gari airport ina navigation system you just drive to your destination. Utanawazi bwana simlaumu dereva alikuwa taxi bubu
 
Kwa wanaojua nasikia huwezi pata visa ya uk au usa kama hujui kingereza ni kweli?. Mbn wao wanakuja ilhali hata neno jambo hajui?.
 
Hivyo huwezi hitimisha kwa kuandika "Kiingereza ni muhimu" pasipo kutaja kwa makundi au kada zipi...

Kiongozi lazima akomalie lugha ya Taifa lake, hii ni sehemu ya utamaduni wetu na ni urithi wa Utaifa wetu.

Sijui kama umeshawahi kujifunza sifa za Taifa kuwa ni lazima wawe na lugha inayowatambulisha??"

End of qoute:-

Sisi ndio ma mbumbumbu wa Afrika Mashariki, na si kwa lugha tu.
Ninyi akina nani mambumbumbu?
 
Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia Tanzania leo kuja kutalii, ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda, kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.

sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.

Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

Kwa upande Wangu Mimi naona mzungu ndiyo mshamba kwa sababu huwezi kwenda ujerumani au ufaransa ukategemea watakuongelesha kizungu. werevu hujifunza japo maneno machache kwanza ya sehemu waendako. zikiwamo slang. mzungu katuaibisha sana na si taxi driver
 
Watu wa kada gani ambao hawatakiwi kujua kiingereza?

Hata tusiende mbali sana, rejelea sifa za Mtanzania anayeweza kuwania kiti cha Ubunge.

Dunia ya sasa hivi hujui ya kesho hivo ni vizuri ukajua mapema

Ni kweli kuwa kesho inaanza leo, lakini wapo wengine ambao kesho yao ni kama leo.
 
Kwa wanaojua nasikia huwezi pata visa ya uk au usa kama hujui kingereza ni kweli?. Mbn wao wanakuja ilhali hata neno jambo hajui?.

Kupata visa siyo lazima ujue english ukifika ubalozi unaulizwa unataka interview kwa kiswahili au english.

Binafsi na ndugu zangu wengi ambao hawajui english zaidi ya ok na yes lakin wamepata visa
 
Uongo huo maana bei haitoi picha halisi ya gharama ya taxi kutoka airport to city centre, kichekesho chako ungekifanya kiendane na hali halisi

Na we umeligundu hilo. Inabidi wawe wanafikiria kabla ya kupost. Kwanza hakuna dereva tax airport ambae ajui hii lugha ya akina thank you ya kutajia bei
 
Na we umeligundu hilo. Inabidi wawe wanafikiria kabla ya kupost. Kwanza hakuna dereva tax airport ambae ajui hii lugha ya akina thank you ya kutajia bei

Nani alikwambia ni airport ?acheni kujitungia mambo yenu
 
nisawa kutojua kiingereza waje nawakalimani wao nasi tupate ajira afu nadhani uyo mzungu alikua nania yakumtapeli mtz. mwenzetu amekuja kutalii na ametembea nch kadhaa za afrika mashariki hajui hata kiswahili lugha inayo kua kwa kasi sasa
 
Back
Top Bottom