Mr Sir1
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 1,749
- 7,945
Kwa wanotumia Pugu/Nyerere Road kutokea Gongo la mboto kupitia Airport watakuwa mashuhuda wa utitiri wa wasafirisha mayai maarafu kama Wakurya wanao ongozana wakiwa na shehena za mayai kwenye baiskeli.
Tatizo linakuja kwa namna ya wanavyoongozana katika barabara kubwa na kuchomekea wenye magari. Na ikitokea kwa bahati mbaya ukamgusa mmoja wao basi wanakuzingira na kukufanyia fujo. Uendeshaji wao wa baiskeli ni wa hatari mno, kama haupo makini ni rahisi sana kuwagonga. Kitendo chao cha kutokutaka kuendesha pembezoni mwa barabara kunaleta hatari zaidi za kuweza kuwavaa na kuwagonga.
Mamlaka za usalama wa barabarani wanapaswa kuwaangalia kwa usalama wao na watumiaji wengine wa barabara na ikiwezekana kushurtishwa kwa faini pale wanapokosea kama watumiaji wa vyombo vya moto, labda hii italeta nidhamu kwao.