JWTZ inatarajia kufanya mazoezi mawili ya kijeshi hivyo imewataka wananchi kutokuwa na hofu

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa linaendelea na Maandalizi ya Mazoezi mawili ya Kijeshi yatakayofanyika hapa nchini ambapo Wananchi wametaarifiwa kutokuwa na taharuki kwa kuwa katika Mazoezi hayo kutakuwa na ongezeko la matumizi ya Ndege Vita na Meli Vita.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa JWTZ mazoezi hayo yanajulikana kama Justified Accord’ na ‘Cutlass Express’ yatakayoshirikisha Jeshi la Marekani na Majeshi mengine ya nchi 12 ikiwa ni muendelezo wa ukishiriki wake katika Mazoezi mbalimbali ya Kijeshi ya pamoja baina yake na Majeshi mengine ya nchi rafiki Duniani.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa zoezi la kijeshi ‘Justifield Accord’ ni zoezi la nchi Kavu linalotarajiwa kufanyika eneo la Msata wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani na Nanyuki nchini Kenya kuanzia tarehe 10 Februari 2025 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi ya Marekani.

Zoezi hilo litazinduliwa rasmi tarehe 10 Februari 2025 na linatarajiwa kufungwa tarehe 21 Februari 2025 na kubainisha kwamba kufanyika kwa zoezi hilo kutatoa fursa kwa vikundi shiriki kuongeza weledi na uelewa wa pamoja wa kupambana na matishio mbalimbali ya kiusalama kama vile matishio ya ugaidi.

Zoezi lingine la ‘Cutlass Express’ ni zoezi litakalofanyika kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja na ushirikiano katika kukabiliana na matishio ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yetu ya uwajibikaji baharini ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Zoezi hilo ni la Jeshi la Wanamaji linalotarajiwa kufanyika katika nchi za Tanzania, Madagascar na Ushelisheli kuanzia tarehe 10 Februari 2025 na kufungwa tarehe 21 Februari 2025 ambapo kwa Tanzania litafanyika katika Jiji la Tanga.

Zoezi hilo litashirikisha nchi kumi na nne (14) ikiwemo Marekani ambayo inashirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika Maandalizi ya Mazoezi hayo hapa nchini.

Nchi waalikwa katika zoezi hilo ni pamoja na Kenya, Madagascar, Shelisheli, Djibout, Comoro, Georgia, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Tunisia, Somalia na Senegal.
 
Wangekuja huku tabora,huku kuna uwazi mkubwa na maeneo tengefu mengi hivyo kusingeleta hofu wala wasiwasi kwa wananchi,isitoshe sisi huku tumezoea kuona misafara ya magari ya kijeshi na vifaru vya kijeshi hivyo wangekuja huku tungeburudika na wangepata uwanda mpana kwa ajiri ya mafunzo hayo.
 
Sio kwa bahati mbaya!hii inafanywa kimkakati sana!

Deep down Kuna reason kuu inayofanya hago yafanyike!!

Nilimsikia huko YouTube kwamba "katiba ya Chama na nchi imekiukwa" Kwa ule mchakato wa Dodoma!

Halafu Kuna la clip ka Monduli mjeda mmoja akitangazia wajeda wenzake umuhimu wa uchaguzi mkuu na kuchagua kiongozi mwadilifu!

Mwenue hizo clips mbili atusaidie !

Kifupi kimenuka SEMA wanatuficha kimenukaje!

Kazi iendelee hata mazoezi nayo ni kazi!!
 
Nchi waalikwa katika zoezi hilo ni pamoja na Kenya, Madagascar, Shelisheli, Djibout, Comoro, Georgia, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Tunisia, Somalia na Senegal.
Jirani yetu asiyepangiwa la kufanya analijua hili?
 
😄 jeshi lipi hilo la kukinukisha

Ova
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa linaendelea na Maandalizi ya Mazoezi mawili ya Kijeshi yatakayofanyika hapa nchini ambapo Wananchi wametaarifiwa kutokuwa na taharuki kwa kuwa katika Mazoezi hayo kutakuwa na ongezeko la matumizi ya Ndege Vita na Meli Vita.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa JWTZ mazoezi hayo yanajulikana kama Justified Accord’ na ‘Cutlass Express’ yatakayoshirikisha Jeshi la Marekani na Majeshi mengine ya nchi 12 ikiwa ni muendelezo wa ukishiriki wake katika Mazoezi mbalimbali ya Kijeshi ya pamoja baina yake na Majeshi mengine ya nchi rafiki Duniani.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa zoezi la kijeshi ‘Justifield Accord’ ni zoezi la nchi Kavu linalotarajiwa kufanyika eneo la Msata wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani na Nanyuki nchini Kenya kuanzia tarehe 10 Februari 2025 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi ya Marekani.

Zoezi hilo litazinduliwa rasmi tarehe 10 Februari 2025 na linatarajiwa kufungwa tarehe 21 Februari 2025 na kubainisha kwamba kufanyika kwa zoezi hilo kutatoa fursa kwa vikundi shiriki kuongeza weledi na uelewa wa pamoja wa kupambana na matishio mbalimbali ya kiusalama kama vile matishio ya ugaidi.

Zoezi lingine la ‘Cutlass Express’ ni zoezi litakalofanyika kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja na ushirikiano katika kukabiliana na matishio ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yetu ya uwajibikaji baharini ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Zoezi hilo ni la Jeshi la Wanamaji linalotarajiwa kufanyika katika nchi za Tanzania, Madagascar na Ushelisheli kuanzia tarehe 10 Februari 2025 na kufungwa tarehe 21 Februari 2025 ambapo kwa Tanzania litafanyika katika Jiji la Tanga.

Zoezi hilo litashirikisha nchi kumi na nne (14) ikiwemo Marekani ambayo inashirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika Maandalizi ya Mazoezi hayo hapa nchini.

Nchi waalikwa katika zoezi hilo ni pamoja na Kenya, Madagascar, Shelisheli, Djibout, Comoro, Georgia, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Tunisia, Somalia na Senegal.
Kuna kibaka atakuwa anaonyeshewa show kwa mbali. Jeshi letu imara huwa halicheki na kima. Viva JWTZ.
 
Shida ya Tanzania ni kutoka na madanga ambao wana uadui.

Juzi tu hapa walifanya mazoezi na jeshi la China leo wanafanye na marekani? alafu watatumia mazoezi haya kupeleka vifaa vingi ambavyo ni made in China& Russia.
Ukifikiria sio sahihi sababu Tanzania bado ipo kijamaa zaidi...kitakachofanyika hapo marekani anakuja kukusanya data kwa nia ovu maana anajua kabisa hatujatulia na bwana mmoja.

Marekani ikitia mikono kwenye jeshi la Tanzania, itabidi tukubali kutumika kama rwanda na Kenya vinginevyo tutatafutiwa matatizo.

Fikiria leo Korea kusini ifanye mazoezi ya kijeshi na China au Korea kaskazini ifanye mazoezi ya kijeshi na Marekani 😃😃

Kwanini wasifanye mazoezi na Kenya ambao mwaka jana imeteuliwa kuwa mwanachama asiye wa moja kwa moja afrika?
 
Back
Top Bottom