Kuna haja ya kuanzisha somo la namna ya kumuelewa na kumuenzi Hayati Magufuli

Kuna haja ya kuanzisha somo la namna ya kumuelewa na kumuenzi Hayati Magufuli

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari wana JF, Tanzania tangu kupata uhuru imetawaliwa na viongozi wengi sana lakini changamoto za watanzania ni zile zile .

lakini kiuhalisia kwa nchi kama Tanzania yenye vyanzo mbali mbali vya mapato hatutegemei mpaka leo changamoto hizo ziwepo.

hii ina maana watanzania wengi na viongozi wengi wanakuwa na mawazo yale yale na namna ya kuongoza ile ile.

JPM alikuja mfumo tofauti ambao ulijenga kuwaaminisha watanzania kwamba wanaweza na kwa Mali walizonazo watu sio wa kutegemea Nje ,Hivyo wafanye kazi kwa bidii hakuna pesa rahisi .

Alifundisha watu kuchukia wizi ,akaenda mbali kutoa watu wenye vyeti feki ambao walichukua nafasi za watu wenye sifa hizo kwa njia ya udanganyifu.

Kama baba wa familia alianzisha miradi mingi kwa kuwaaminisha waamisha wanawe kwamba pesa wanazoingiza ndio zinajenga hiyo miradi lengo waendelee kupambana ,kumbe kuna baadhi ya pesa anakopa nje.

Lakini pia aliwaongoza watanzania katika kipindi kigumu cha UVIKO-19 kwa busara zake watanzania wengi walipita salama kiuchumi na kiafya kipindi hicho.

Lakini alienda mbali na kuamini adui wa Nchi ni adui wa JPM pia hivyo alishughulika nao vilivyo na wakati mwingine nguvu kubwa ilitumika kukusanya kodi.

Kwa haya utagundua alikuwa Tofauti na watanzania na viongozi wengi na ndio wengi hawamuelewi hivyo kwa Mambo alifanya na kuanzisha kwa Muda mchache kuna haja elimu hiyo ikamfikia kila Mtanzania na kuienzi .
 
Kumbe haeleweki?

Mbona mlidai anaeleweka na wanyonge?😂😂

Jamaa aliyekiri kwamba UvIKo ilikuwepo ila suluhisho akasema ni maombi ya siku 3?😂😂

Kuanzisha miradi kila mtu anaweza, ishu ni kumaliza hiyo miradi, Magufuli alianzisha na kumaliza mradi gani mkubwa?
 
Alifundisha watu kuchukia wizi ,akaenda mbali kutoa watu wenye vyeti feki ambao walichukua nafasi za watu wenye sifa hizo kwa njia ya udanganyifu .
1. Kama alichukia wizi kwa nini Sabaya anasota ndani kwa makosa ya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha.

2. Mnyeti nae anapandishwa kizimbani kwa ufisadi.

3. Yale magari aliyokuwa anabadilisha makonda akiwa RC yanajulikana mengine alikwapua kwa wauza unga na huyo magu alikaa kimya.

Na bado watu wote hao wa3 wana rekodi mbaya dhidi ya haki za binadamu kama Sabaya kukata masikio na kutesa watu.

Mwisho wa siku marehemu alificha hela za kutosha nyumbani kwake Chato.
MAREHEMU ANA MENGI MACHAFU ALIYOANDIKA KWA MATENDO YAKE MWENYEWE.
 
Uko sahihi sana mkuu.

Watanzania wanapenda sana uongo wa wazungu. Wanadhani wazungu walitajirika kwa demokrasia. Wazungu walitajirika kwanza halafu ndo wakaleta demokrasia baadae. Walitajirika kwa kufanya ujambazi duniani kote ambako walivamia dunia nzima na kupora ardhi na mali. Hayo yote waliyafanya wakiwa chini ya tawala za kiimla, tawala za Kifalme.

Mfano mwingine ni angalia waarabu wenye tawala za kiimla za kifalme, na Wanaijeria au Waangola. Wote wana mafuta ya kutosha kubadilisha nchi zao, lakini ni tawala za kiimla tu ndo zimeweza kubadilisha nchi zao.

Demokrasia sio nzuri kwa nchi inayotaka kufanya mapinduzi ya kiuchumi. Demokrasia ni anasa ya watu ambao wameshatajirika tayari.

Tungekaa na Magufuli kwa miaka mingi nchi ingefika mbali sana kiuchumi na kifikra.

Sasa hivi hatuna uongozi wa fikra kama taifa. Viongozi walioleta uongozi wa fikra Tanzania ni wawili tu - Nyerere na Magufuli.
 
Habari wana JF , Tanzania tangu kupata uhuru imetawaliwa na viongozi wengi sana lakini changamoto za watanzania ni zile zile...
Hata na Polepole alikuwa na akiri kama zakwako ..hadi akaanzisha Chuo kabisa kama UD chakueneza demokrasia ya jiwe baada ya kulamba asali tupo naye hapa Lilongwe akatulia.Wewe pambana usije ukalamba asali nakuterekeza wazo la kipumbavu kama hilo
 
Kumbe haeleweki?

Mbona mlidai anaeleweka na wanyonge?😂😂

Jamaa aliyekiri kwamba UvIKo ilikuwepo ila suluhisho akasema ni maombi ya siku 3?😂😂

Kuanzisha miradi kila mtu anaweza, ishu ni kumaliza hiyo miradi, Magufuli alianzisha na kumaliza mradi gani mkubwa?
Unataka kusema alianzisha miradi ambayo asingemaliza ?
 
Uko sahihi sana mkuu.

Watanzania wanapenda sana uongo wa wazungu. Wanadhani wazungu walitajirika kwa demokrasia. Wazungu walitajirika kwanza halafu ndo wakaleta demokrasia baadae...
Na ndio maana ni rahisi sana kuwatawala wa Tanzania
 
Back
Top Bottom