HOJA Kuna haja ya kuwa na vituo vya kulea wazee mikoa yote Tanzania

HOJA Kuna haja ya kuwa na vituo vya kulea wazee mikoa yote Tanzania

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Nchi zilizoendelea ndiyo maisha yao haya.

Hakuna mtu aliye na muda na kulea wazazi wao wakishazeeka.

Unakuta kila mtoto yuko busy kukimbizana na maisha yake.

Mzazi ukishazeeka kiasi cha kushindwa kujifanyia zile ADL (Activities of Daily Life) basi unapelekwa huko centre za kulelea wazee.

Na sisi ndiko tunakoelekea.
Nchi zilizoendelea kaka.... Sio hizi mpaka leo maji mtihani, umeme mtihani, barabara chenga, ajira mgogoro, madawa hospital chenga, vifaa tiba chenga ndio ulete huduma ya makazi ya wazee !?? Makazi ya polisi tu chenga ,magereza wanakaa kota za nyumba za tope....mtawatesa tu wazee
 
nimesema hakuwezi kuwa na makampuni ya kulea wazee kwa sabab hiyo na hoja yangu hapo familia zao ndo ziweke uangalizi kwa wazee wao kwan ukiwa busy na kazi huwezi ajili mtu wa kumtunza mpaka umpeleke akalelewe kwenye vituo
Hoja yako ni dhaifu sana,au inawezekana una lack of exposure kwenye hii issue,

Hujulikani hata unachokipinga,unapinga Day care halafu hapo hapo unaleta issue ya kuajiri mtu akulelee mzazi wako!

Kwani wewe ukisikia vituo vya kulelea wazee,kwenye akili yako hua unawaza ni Jela sio? au unawaza ni sehemu ya mateso sio?
 
Kaka umefika hata kituo kimoja Cha Serikali ukaona maisha ya wale Wazeee!?? Sio maisha yale .... Hatujafikia kabisa uwezo huo... Labda vituo binafsi..... Vya Serikali!?? Bora muwauwe tu wanateseka sana kule
 
Kila mzee ana mtoto?
Good point J.

Na hata kama wanao, process za maisha hatujui nini kilitokea katikati inawezekana wawepo wasiwe willing kuwatunza wazee wao.

Wazee ni raia wa nchi hii, wameijenga kwa nguvu na kulipa kodi, serikali ifanye jambo.

Ziwepo tu, tutakaolea wazee wetu nyumbani tulee, watakaokosa mahali pakulelelewa walelewe huko.
 
Ukweli mchungu sana Mkuu

Ni Kuna umuhimu wa kuweka vituo vya kulea wazee japokuwa sio watu wote watawapeleka wazee wao , hivyo

Huko mitaani tunaona wababu/wabibi wapo majumbani kwao wakiwa dhoofu lihali, hawana Moja wala mbili kama wametelekezwa na watoto au hawana watoto so kama vituo vitakuwepo na ikatokea wakapata pesa za pention zao wanaweza kujipeleka/kujilipia wakaenda mapumziko sio lazima upelekwe na watoto wako

Walioandaa hivyo vituo kwenye nchi zao walifikiria mengi sana ambavyo sisi wenye fikra finyu ni vigumu sana kung'amua

Jirani hapa Kuna mama anaumwa hatari na anayemuhudumia ni mwanae wa miaka 16 Kasichana, na hakuna ndugu yake aliyefika kumuhudumia , Bali ni majirani tu kuja kumuangalia na kusaidia vijipesa vya mahitaji, kama mgonjwa au mtu mzima huyu si angeweza kupelekwa tu kwenye vituo kama hivyo kupewa uangalizi.
 
Kaka umefika hata kituo kimoja Cha Serikali ukaona maisha ya wale Wazeee!?? Sio maisha yale .... Hatujafikia kabisa uwezo huo... Labda vituo binafsi..... Vya Serikali!?? Bora muwauwe tu wanateseka sana kule
Mimi ninachojadili hapa ni System ya kua na utaratibu wa kua na hivyo vituo,naamini kua sio system mbaya,na huyo niliyemquote,yeye anapinga System ya kua na vituo vya aina hiyo,

Huku nilipo hilo ni jambo la kawaida sana,sema wabongo watazowea tu polepole coz huko tunapoelekea na kwa kizazi hiki cha leo,vituo vya kulelea wazee itakua ngumu kuviepuka.
 
Najua ni wazo zuri alivyolileta ndio changamoto... Aseee oyaaaaa... Yake sio maisha Mzee.... Kule kwa kulea wazee sioni kabisa faida yake kwa malezi Yale kwa wanaofahamu watanielewa. Bongo kulea tu yatima tumeshindwa hao wazee mtawaua mapemaaaaa ..... Uzuri nipo Mwanza na kati ya vituo 13 vya Serikali Tanzania mzima ... Mwanza tunavyo viwili oyaaa.
Sawa mkuu
 
Hoja yako ni dhaifu sana,au inawezekana una lack of exposure kwenye hii issue,

Hujulikani hata unachokipinga,unapinga Day care halafu hapo hapo unaleta issue ya kuajiri mtu akulelee mzazi wako!

Kwani wewe ukisikia vituo vya kulelea wazee,kwenye akili yako hua unawaza ni Jela sio? au unawaza ni sehemu ya mateso sio?
cyo jera but ni heri mzee akalelewa na familia yake
 
Mimi ninachojadili hapa ni System ya kua na utaratibu wa kua na hivyo vituo,naamini kua sio system mbaya,na huyo niliyemquote,yeye anapinga System ya kua na vituo vya aina hiyo,

Huku nilipo hilo ni jambo la kawaida sana,sema wabongo watazowea tu polepole coz huko tunapoelekea na kwa kizazi hiki cha leo,vituo vya kulelea wazee itakua ngumu kuviepuka.
Umeona uliposema "huko ulipo" ..sio "huku tulipo sisi"..... Huko ulipo bado mnahangaika na maji safi na salama!?? Sasa sisi huku tunakunywa maji na ng'ombe kwenye malambo bado ndio unataka tutengeneze vituo vya kulea wazee!??
 
Kaka umefika hata kituo kimoja Cha Serikali ukaona maisha ya wale Wazeee!?? Sio maisha yale .... Hatujafikia kabisa uwezo huo... Labda vituo binafsi..... Vya Serikali!?? Bora muwauwe tu wanateseka sana kule
Ni kweli mkuu unachosema, ndio maana kama tunavyobanana na serikali iboreshe shule, hospital, barabara tubanane nao hivyo hivyo kuboresha hivi vituo kwasababu ni necessity.

Ni hitaji ambalo linatakiwa lipigiwe kelele bungeni kama zilivyo hoja zingine, kidogo kidogo tutapata mabadiliko.

Tusiwe na aleji na mabadiliko hasa mabadiliko chanya.
 
Huna ardhi
Huna nyumba
Huna watoto wengi.
Uzee lazima unyooke.

Watoto ukishakuwa nao wakutosha, mahali pakuishi na mashamba. Uzee hauwezi kukusumbua.
Zingatia sio mtoto mmoja au wawili.
Walau watoto wanne na kuendelea.

Na lazima watoto hao uwalee kifamilia sio uwapelekee boarding tangu wakiwa watoto
 
Umeona uliposema "huko ulipo" ..sio "huku tulipo sisi"..... Huko ulipo bado mnahangaika na maji safi na salama!?? Sasa sisi huku tunakunywa maji na ng'ombe kwenye malambo bado ndio unataka tutengeneze vituo vya kulea wazee!??
Wewe una amini kua ni wazee wote watapata tabu kwenye hivyo vituo kuliko tabu wazozipata sasa hivi huko mitaani?

Kuna wazee wanaishi mitaani tu,Jua lao Mvua yao,kulala vibarazani,hakuna cha medical care wala uangalizi wa aina yeyote ile,wazee kama hao ndio ninao waongelea Mimi,

Ziwepo pia za Private itakua ni jambo bora zaidi,so mtu atakua na choice.
 
Na lazima watoto hao uwalee kifamilia sio uwapelekee boarding tangu wakiwa watoto
Na hapa ndipo wazazi wengi wanapokosea,mtoto toka mdogo unaenda kumtupa boarding,
Mtoto anakua bila ya kua na feeling na wewe,

Ni lazima mtoto akiwa mdogo awe karibu na wewe ili kutengeneza Emotion connection/Emotion bond,kati ya mzazi na mtoto,

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kulea na kuhudumia,
Wazazi wengi hujidanganya kua kuhudumia ndio kulea!
Mtoto humkumbuka zaidi aliyekua nae karibu wakati wa makuzi yake,humkumbuka aliyemlea.
 
Huyu mtoto mmoja niliyenaye huko juu naona uwe na wengi duuh 🤔

cha msingi kuweka bond nzuri na mwanao hali akikukumbuka, au ukiwa na uhitaji naye anajua nn maana ya mzazi, sio anakuchukulia km mpita njia

Eniwei uzee ni miaka mingp wazee wangu nijipange
 
Good point J.

Na hata kama wanao, process za maisha hatujui nini kilitokea katikati inawezekana wawepo wasiwe willing kuwatunza wazee wao.

Wazee ni raia wa nchi hii, wameijenga kwa nguvu na kulipa kodi, serikali ifanye jambo.

Ziwepo tu, tutakaolea wazee wetu nyumbani tulee, watakaokosa mahali pakulelelewa walelewe huko.

Na inawezekana hao watoto walikuwepo lakini wakatangulia
Cases za wazee kukosa misaada sababu zipo za kutosha tu

Kimsingi kama ulivyosema,serikali ifanye jambo watakaoweza kulea walee
 
wengne hawana ila asilimia kubwa ya hao wazee hupitia changamoto sabab siyo hawana watoto hukosa malez kutokana na watoto wao kutoku wajali

Hiyo sasa ni case nyingine,ya maamuzi ya mtoto kulea ama asilee

Serikali iweke tu hivyo vituo bila kujali
 
Hiyo sasa ni case nyingine,ya maamuzi ya mtoto kulea ama asilee

Serikali iweke tu hivyo vituo bila kujali
ni kweli kunaumhimu lakn serkali kunamikadi ming haijakamilsha mfano barabara kutoka mariny to irakar yaan ukipita hutamani tena kuludi rakin piah kunasehem hata maji safi hamna
 
Back
Top Bottom