Kuna haja ya Rais Samia kufundishwa jinsi ya kudhibiti hisia zake anapoongea/anapohutubia

Mama anakuwa mtulivu kwa mambo yoote ila swala la Lissu na Katiba Mpya huwa vinamtoa kwenye line kabisa.

Sijajua shida ni nini
 
Sasa utamfananisha na yule aliyekuwa anasema mkanye mavi nyumbani kwenu?
 
Sawa kwa maoni na mawazo yako, lakini si wote tunamuona kama unavyotiririka hapa. Yupo vizuri tu kwa maoni yangu.
 
Mtu ambaye alikuwa anauweza urais na kujibu maswali tata ni Nyerere tu baada ya yy hakuna mtu
Siyo kila mtu anaweza kuwa kama Nyerere. Nyerere alikuwa hana mipasho kwenye masuala ya utawala. Nyerere, kama haelewi kitu alikuwa mtafutaji mpaka akielewe ndipo atoke hadharani. Ndiyo maana hata hotuba zake zilikuwa zinatisha. Nakumbuka dunia ilishtuka Nyerere alipotoa hotuba Marekani,New York, akisema haingii akilini kwa wacha Mungu kama Wamarekani,wakati huo, ambao wanajua kuwa Mwenyezi Mungu alimwuumba binadamu kwa mfano wake, je kama theluthi mbili ya wanadamu, wakati ule, ni maskani hawaoni aibu kuwa hiyo ni sura ya Mungu hapa duniani ni sura ya umaskini!?Mkuu ye yote hawezi kufahamu kila kitu lakini ni jukumu lake kutafuta Watanzania wenye uelewa na uwezo wa kumshauri masuala ya nchi siyo ndugu au marafiki. Kwa hakika hao hawawezi kumshauri, watampendeza tu. Washauri wa namna hiyo ni sawa na nchi kupeleka wacheza mpira wa miguu marafiki au second division team kwenye world cup competition halafu unashangaa matokeo !
 
Wapi naweza pata mahojiano ya Mkapa?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Haya
 
Sijaelewa
 
Sikiliza rais ni binadamu,kuonesha hisia ni sawa kabisa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana Nchi kama USA,CHINA &RUSSIA hawawezi kumpa Mwanamke Urais-siku zote wanajua wapo dhaifu dhidi ya Mwanaume na ndivyo uhalisia.
Imagine angekuwa Rais wa Nchi tajwa si angeonekana kituko mbele ya Dunia.
 
Mkapa alitaka kupiga mtu kwenye hard talk!
Sio Mkapa tu, hata Kikwete alizinguaga eti hajui kwa nini Nchi yake ni maskini.Ndio maana nasema hii Nchi kiongozi kidogo alikiwa Nyerere hasa wengine ni bahati tu walikuwa nazo wakajikuta katika nafasi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…