Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,971
- 9,437
Hakuna ubishi kuwa Simba ndio nembo ya Taifa hili kwenye medani za kimataifa ngazi ya klabu barani Afrika.
Simba imekuwa tunu ya Taifa hili hakika tunapaswa kujivunia, huko nyuma tulikuwa wanyonge timu kutoka nje ya nchi zilikuja na kujibebea pointi na kuondoka zao.
Hivi sasa kuna klabu gani kubwa Afrika isiyoijua Simba SC? Hasa inapokuwa uwanja wake wa nyumbani? Benjamin Mkapa (lupaso), jibu ni hapana hivi sasa ni tishio barani Afrika hii haijaja kwa bahati mbaya ni mikakati na uthubutu.
Hivi sasa Tanzania tumepata uwakilishi wa klabu nne kimataifa, hii siyo ndondokela ni Simba kufanya kwake vizuri kimataifa, kuna haja ya bunge la nchi hii kuhakikisha kila wanapopitisha bajeti kila mwaka basi na bajeti ya Simba iwepo.
Jumapili ijayo itamenyana na Orlando Pirates kutoka South Africa, embu vuta picha ni mashabiki wangapi dunia wataufuatili mchezo huo? Ni kiasi gani cha pesa kama taifa tutaingiza kupitia mchezo huo? Jibu ni pesapesa za kutosha.
Nimalize kwa kuwaomba Watanzainia hii ni timu yetu sote tuiunge mkono kwa hali na mali tujitokeze kwa wingi tarehe 17 tukiwa na uzi wetu mwekundu, hii mechi hatuhitaji kushinda tu bali tunataka ushindi wa kishindo.#NGUVUMOJA.