Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Kumekuwa na ongezeko la homa kali za mafua zinazowakumba wananchi wengi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Wananchi wanaonekana kuwa na wasiwasi juu ya kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huu, lakini wanahoji ukimya wa mamlaka husika kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na hali hii.
Je, mamlaka zinafanya jitihada zozote za kudhibiti homa hizi, kutoa elimu kwa umma, au kuhakikisha kuna upatikanaji wa taarifa sahihi na ushauri wa kiafya kwa umma?
Kwa nini mamlaka hazitoi taarifa kwa umma ili kuwajulisha kuhusu hali halisi na namna bora za kujikinga? Utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati ni muhimu ili kuzuia taharuki na kuwapa wananchi mwongozo wa hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa ili kujikinga na kusambaa zaidi kwa homa hizi.