Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,051
- 51,217
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa nyumbani nahisi labda kuna jambo sisi wananchi tumeikosea serikali yetu na imeamua kutuadhibu.
Kwakua ,Serikali yetu ipo busy kuhakikisha kuwa maisha ya Mtanzania yanakua magumu kila siku.
Kwanza walibadili bei ya kuunganishwa umeme toka elfu 27 mpaka laki tatu. Zanzibar imebakia ile ile.
Pili wakawafukuza kila mahali wamachinga. Zanzibar wameboreshewa vitambulisho vyao ili wakopesheke.
Tatu wakaondoa kiasi cha shs mia kwenye mafuta na kuirejesha tena kipindi ambacho bei ya mafuta imepanda. Hapa ukali wa bei umeongezeka mara mbili.
Nne hakuna mradi hata mmoja wa kimkakati uliokamilika wala hakuna jitihada za wazi na za dhati kuhakikisha inakamilika.
Tano ongezeko la mikopo isiyokuwa na tija inayopelekwa katika miradi ambayo haileti faida.
Sita kuanzishwa kwa tozo juu ya kodi jambo linalofanya mwananchi alipe kodi mara mbili kwa huduma moja.
Saba umeme na maji sio vya uhakika.
Nane bei za bidhaa na huduma zinapanda kila siku na hakuna anayejali.
Kurejea kwa huduma mbovu za kijamii na rushwa.
Unabaki kujiuliza nia halisi ya serikali hii ni nini??
Je kuna jambo sisi wananchi tumeikosea serikali hii?? Tuambiwe tujue.