Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Kila nchi inatofautiana katika rasilimali za kijeshi kuanzia personnel,ujuzi,vifaa,technologia,etc.Sasa kama rasilimali zao za kupambana na ugaidi ni chache unawatuhumu vipi kuwa wanawafuga?
Haijalishi sababu, end result ni wanafugwa!
 
Kwani mimi nimepinga kuwa hawafugwi?Umesoma nilichoandika?Mimi nimepinga lawama
Kama mtu mmoja anawekeza pesa zake kwenye kuongeza mke na mwingine anawekeza pesa zake kusomesha watoto, tunakosea kumlaumu huyu mmoja anaefuga ujinga?
 
Kuongeza mke kwako inaweza kuwa ni ujinga ila kuongeza mke kwangu inaweza kuwa ni baraka.Kwa mfano kwa wenzetu waislam kuongeza mke wa pili ni kupata baraka za mwenyezi Mungu ila kwa wakristo ni dhambi.Wewe ni nani hadi uwe mtu wa kuamua kwa watu wote kuwa kufanya hili ni sawa ila kufanya lile ni ujinga?
Na kwasababu hiyo sasa, kwakuwa wameamua kufanya hiki na wakaacha kile kwa uamuzi wao wenyewe, ndio tunasema wanafuga magaidi, wacha wanyooshwe!!
 
Kwani wamekuambia kuwa wananyooshwa?Wewe unawasemea kama nani?Yaani mimi niwe na wake kumi halafu wewe uje kunisemea kuwa wananipa taabu?What if mimi naenjoy kuwa nao?
Sawa, hatujasema huienjoy, ila fact is watoto hawapati elimu stahiki na hivyo unafuga ujinga!
 
Nasikia washakalishwa zimebaki kambi mbili tu katika 7 zilizokua zinapigana na wajeda na Sasa wajeda wanasubiri mzeebaba awape go ahead wazema kabisa Hadi huko msumbiji Mana ndio wanafugwa huko
 
Nasikia washakalishwa zimebaki kambi mbili tu katika 7 zilizokua zinapigana na wajeda na Sasa wajeda wanasubiri mzeebaba awape go ahead wazema kabisa Hadi huko msumbiji Mana ndio wanafugwa huko
Unafurahisha genge
 
Kilichopo tu ni kwamba baada ya 'Wahuni' hawa 'Wanamgambo' kuondolewa na JWTZ kwa 'style' ambayo hawatakuja Kuisahau huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji 'walipoichokoza' Tanzania baadhi yao hasa wale Waandamizi wao walikimbilia nchini Msumbuji ambako ndiko kuna Ngome yao Kuu na hata walipokuja huku Pwani na kule Amboni Tanga walitokea huko huko.

Taarifa nilizothibitishiwa na Chanzo kutoka katika 'Kikosi Maalum' ni kwamba hawa 'Wahuni' wanatamba na kusumbua sana tu huko nchini Msumbuji japo kwa miezi kama Saba ( 7 ) hivi iliyopita walikuja maeneo ya mpakani na Tanzania ila kutokana na 'Intelligence' imara ya Tanzania na ile ya Jeshini ( CMI ) waliweza 'Kudhibitiwa' na wakakimbilia huko 'Ngomeni' Kwao Msumbiji.

Na ni kweli kwamba 'Wahuni' hawa ( ambao ni Wanamgambo ) wana 'Vifaa' vikubwa tu na uwezo mkubwa wa Kivita hasa hii ya Msituni ( Guerrilla ) na 'Mafunzo' makubwa sana ya 'Kivita' hali ambayo imefanya mpaka wameweza 'Kupambana' vilivyo na 'Jeshi' dhaifu kwa sasa la Msumbiji na kuweza kuteka Bandari muhimu huko ambayo inawasaidia Kuwaingizia Kipato na 'Kutamba' pia.

Kuna taarifa tulipewa kuwa Wanajeshi wa Tanzania ( JWTZ ) sijui 'wametekwa' na Kukimbia hadi Kukiacha 'Kifaru' huku tukiaminishwa kwa 'Video' ila ukweli ni kwamba kilichoonekana siyo 'Kifaru' bali ni 'APC' nadhani wale Watu wa 'Medani' hapa mtakuwa mnaelewa na si vibaya pia mkija kutusaidia zaidi 'Kutuelimisha' juu ya hiki Chombo.

Kuhusu Picha ( Poster ) ya Mgombea Urais wa CCM ( sasa ni Rais ) Dkt. Magufuli kuonekana kwa hawa Wahuni ( Wanamgambo ) ni sehemu tu ya 'Propaganda' ya Watu wenye 'Chuki' na Tanzania na hasa ikiwa inaelekea katika Uchaguzi Mkuu huu ujao kama 'Kuichafua' na hata Kuzua 'Hofu / Tafrani' miongoni mwa Watanzania na hasa hasa Wakazi wa huko Mtwara.

Tumeambiwa kuwa kuna Watanzania 'waliokufa' huko na kwamba hali ni ya 'wasiwasi' mno huko Mkoani Mtwara hasa eneo la Nanyamba ila ukweli ni kwamba eneo liko salama kabisa tena 100% na hakuna 'Mauwaji' yoyote yale isipokuwa Jeshi la Tanzania ( JWTZ ) kwa Kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vimeendelea tu 'Kuimarisha' Usalama huko.

Kilichonishangaza zaidi GENTAMYCINE ni kwamba nina Ndugu zangu huko na nimefanya 'Jitihada' za 'Kudadisi' kama kuna 'sintofahamu' ya aina yoyote ile inayohatarisha Amani huko ( kama tunavyoaminishwa ) nilichojibiwa tu ni kwamba Mtwara iko salama. Na nawaombeni nanyi wana JF pia mjaribu Kuwasiliana na Watu wenu huko ili muweze 'Kujihakikishia' juu ya hili.

Nimalizie tu kwa Kuishukuru Serikali ya Tanzania chini yake Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Magufuli pamoja na Vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania kwa 'Kupuuza' na Kuunyamazia 'Uzushi' huu ambao 'unaratibiwa' vyema kabisa na wale wasioitakia mema nchi yetu na kutaka kuleta 'taharuki' hasa wakiwa na lengo la Kuitia nchi 'Doa' la Kiusalama na Amani yake.

Asante sana na mno Wewe 'Chanzo Changu' kutoka hapo 'Kikosi Maalum' juu ya hili na Mimi nimeamua 'Kushea' hapa na Watanzania wenzangu.
Mkuu you are miss informed!..,Naapa kwa MUNGU Hali ni tete Mtwara,,,Tarehe 18 hii ulipocomment huu uongo Waasi wevamia Wilaya ya Tandahimba,kijiji cha Michenjele,,Wameua watu wamechoma majumba moto!.. Mkuu Wamechinja mwalimu OMBENI wa SHULE ya msingi Michenjele,,wamemteka Mwalimu Mkuu msaidizi wa SHULE ya sekondari Michenjele,,Wamemteka mke wa Mwalimu wa SHULE hiyo pia,,,,,SHULE ZIMEFUNGWA HAKUNA WANAFUNZI,,, BAADHI TU NDO WAMEHAMISHIWA TANDAHIMBA DAY..,,, NIPO TANDAHIMBA MJINI ,,,,,MILINDIMO YA RISASI NA MABOMU NILISIKIA KWA UZURI NA HATA MAITI NA KICHWA CHA MWALIMU OMBENI NILIKIONA ,,SASA SIJUI UNAONGEA NA WATU WA MTWARA IPI?....
 
Wazee leo katika mishe mishe Sina hili Wala lile nikapokea simu ya dogo wangu ni mwanajeshi kambi flani akaniambia bro niko safarini naelekea Mtwara.

Katika kunieleza akasema kule kuna Hawa Islamic State wameingia na mbaya zaidi walimkamata mwanajeshi wamemuua na wakamkata kichwa. Pia kuna habari kwamba wameteka watu zaidi ya 30. Sasa basi juzi waliitisha kikao kambini na kupewa maelekezo na wameanza safari ya kuelekea mtwara huko kupambana na hawa magaidi.

Katika kumuuliza zaidi na kuomuombea kwamba Mungu amlinde na wamelize zoezi salama huku nikiwa na mshituko kidogo dogo akaniambia usiwe na wasiwasi tuko vizuri na tumejipanga pia tumebeba siraha nzito nzito yani tukifika ni Moto tu paka waelewe yani kimsingi tuko vizuri

Daah hili nalo linakichanganya kwamba wamebeba siraha nzito na za kutosha huko kuna nini?

Kwa wanaojua je huko kumetokea Nini na kwa Nini serikali Kama hakuma taarifa za haya matukio?

Yote kwa yote nawaombea Askari wote wanaoenda huko na dogo pia Mungu awe nao na warudi salama
In God we trust[emoji123]
Mkuu,, ni KWELI Wapo na mipaka kwa sasa inalindwa Naungana na wewe kumuombea dogo
 
Mkuu you are miss informed!..,Naapa kwa MUNGU Hali ni tete Mtwara,,,Tarehe 18 hii ulipocomment huu uongo Waasi wevamia Wilaya ya Tandahimba,kijiji cha Michenjele,,Wameua watu wamechoma majumba moto!.. Mkuu Wamechinja mwalimu OMBENI wa SHULE ya msingi Michenjele,,wamemteka Mwalimu Mkuu msaidizi wa SHULE ya sekondari Michenjele,,Wamemteka mke wa Mwalimu wa SHULE hiyo pia,,,,,SHULE ZIMEFUNGWA HAKUNA WANAFUNZI,,, BAADHI TU NDO WAMEHAMISHIWA TANDAHIMBA DAY..,,, NIPO TANDAHIMBA MJINI ,,,,,MILINDIMO YA RISASI NA MABOMU NILISIKIA KWA UZURI NA HATA MAITI NA KICHWA CHA MWALIMU OMBENI NILIKIONA ,,SASA SIJUI UNAONGEA NA WATU WA MTWARA IPI?....
Mkuu kuna mijitu humu ipo kusifia ujinga ujinga tu by the time the situation is not good at all
 
Nimearifiwa na mmoja wa wahanga kuwa katika kijiji cha Kitaya kilichopo katika Halmashauri ya Nanyamba huko Mtwara kuna hali tete inaendelea huko.

Kijiji kimevamiwa na watu wenye risasi za moto hali iliyopelekea Wananchi kukimbilia Porini.

Mpaka asubuhi hii risasi zilikuwa zinaendelea kurindima.

Nimepatiwa taarifa hii na mkazi mmoja akiwa huko mafichoni na familia yake.

Nitaendeea kuwajuza kadri nipatavyo taarifa.

Tuwaombee.
Update 1:
View attachment 1602008

View attachment 1602010

UPDATE:

Tanzania border village attack 'leaves 20 dead' - BBC

Mozambique: Suspected militants attack Tanzanian border village of Kitaya (Mtwara Region) October 15
tuendelee kupambana na watu waliopo na wanaofanya majukumu yao kwa mujibu wa katiba,
 
We akili huna yani unashindwa kujua mgaidi Wana kambi au hawana?
Hawa magaidi wanaovaa ndala na bunduki za kupasiana ndio unasema wana kambi. Kambi ina ghala la silaha, hifadhi ya mafuta, zana za kivita, makazi ya wapiganaji. Muhimu, kambi inakuwa na namna ya kulindwa.

Sasa magaidi wakiwa na kambi si unatuma ndege zikaishambulie na kumaliza kazi? Unadhani wao ni wajinga kiasi hicho kujirundika sehemu moja wawe target wakati hata silaha zenyewe wanabahatisha. Kwanza gharama za kuendeshea wala kujenga hiyo hawana.

Hawa hata observation post hawana sembuse camp.
 
JWTZ inabidi lipelekwe Syria kuona jinsi gaidi avyozibitiwa
 
Back
Top Bottom