Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #41
Watu wanadandia tu hoja hapa na pale haya mambo ni mazito watu wako kazini tangu enzi na enzi Putin lazima wamdondoshe Kwa gharama yake mwenyewe na Uchumi wao utaanguka sana tu Tena sana sana
Anahimili? Bila shaka hujui Kiingereza.ajenerali wa Urusi wanasema hakuna askari asiemtukana Putin kwa sasa. Yaani Putin anapigika sawasawaNampongeza putin kupigana na ulaya na marekani na bado anahimili vishindo.
Mkuu, hii ni Twit ya Urusi. Ndio kitu kinaitwa propaganda, mbona unadanganyika kirahisi?Nchi unazozitegemea kumuangusha Urusi zenyewe ziko frustratedView attachment 2389072
Mkuu, umeandika vizuri na inaonyesha una kitu fulani ila pia kimeegamia upande fulani!Watu wengi walio kwenye nchi maskini na wengine wanaochukia ubepari wameegdmea upande wa urusi, na ni kundi hilo hilo linamshabikia Rais wa Korea ya kaskazini. Hata hivyo, pamoja na madhira yaliyosababishwa na Marekani kwa nchi nyingi zilizo kinyume na msimamo wake, tunapaswa kutambua hii vita ya Russia na Ukraine, Putin ni kama yuko peke yake pamoja na ujasiri alionao. Ukraine anasaidiwa na wengi tena wazi wazi. Nchi za magharibi zinaijua urusi zaidi kuliko sisi wa mitandaoni. Kujitoa wazi wazi kuisaidia Ukraine, maana yake hazitishwi na uwezo wa urusi kama tunavyofikiri. Wako wengi wenye tekinolojia ya juu zaidi. Viinchi kama Norway unaweza kuvidharau, lakini viko mbali sana kwenye sayansi ya nyuklia. Wakati mtambo wa nyuklia unavuja huko urusi mwa miaka ya 90 waliogundua ni wasweden ndo waliwapa taarifa warusi. Pia wakati nyambizi ya kirusi iliyobeba silaha za nyuklia ilipolipuka na kuzama na baadaye kuua wanamaji wote 118. Walioweza kwenda kuifunga nyambizi hiyo ikiwa kwenye kina cha mita zaidi ya 100 ni waNorway, kumbuka warusi wenyewe walikuwa wameshindwa. Kwa hiyo, vita hii siyo nyepesi kwa urusi kama wengi wanavyofikiria. Vita inapochukua muda mrefu huharibu uchumi. Urusi inatumia gharama kubwa sana kwenye vita hii. Tena ingekuwa bora huko nyuma ikiwa imekumbatia ukomunisti, sasa hivi urusi ina uchumi wa soko huria, kama ilivyo china. Wakati huo ilikuwa siyo rahisi raia kiipinga serikali yao kwenye mission kama hizi.
I see ni kweli.Uyo jamaa ni mwehu achana naye wala asikupe shida mzee mpotezee kabisa sasa uyo mtu anayeandika vitu kama ivo huoni kuwa hajielewi yaani ni empty set chiz fresh uyo achana naye
Kama unajua Kiingereza soma hapa chini. Ila nina wasiwasi hujui, la sivyo usingekuwa unatoa off point kama hizi bila kuwa na chanzo. Halafu mbona nimeshasema kwentye thread Putin kajipendekeza kuwapa Ulaya gesi wamemshushua kuwa wako tayari kukaa na baridi kuliko kuchukua gesi yake?We umemsikia nani hizi habari? Waache kutumia gesi Ili waokote kuni Kwa ajili ya kuotea moto majira ya baridi? Unawazimu bila shaka .
Hakuna unachojua zaidi ya daipa na ushoga, inaonekana ndiyo fani yako.Badilisha DIAPER wewe, ndio urudi hapa jukwaani ukiwa msafi.
Sikiliza huu mziki hapa chini kabla ya kumpongeza Putin. Askari wake wanaanza kusingizia kuharisha wasiende vitani, hadi wanajikata na visu waseme wamejeruhiwa vitani!Nampongeza putin kupigana na ulaya na marekani na bado anahimili vishindo.
Ikiuma chomoa.Hakuna unachojua zaidi ya daipa na ushoga, inaonekana ndiyo fani yako.
Warusi wamuombe sana mungu, huyo Dictator amwondoe. Sisi mungu alitufanyia makubwa sana kwa kutuondolea lile jitu.Vita ya Urusi na Ukraine imeathiri karibu nchi zote duniani, na hasa upande wa mafuta. Vita hii imeleta hali ambayo haikubaliki duniani kote na ndani ya Urusi pia. Kimsingi, Putin ndio anaonwa kua chanzo cha haya yote.
Na ni wazi Putin hakutarajia kwamba hali ya vita na Ukraine ingekua kama ilivyo sasa. Kwa sasa anawaza sana jinsi ya kuepukana na aibu ya kupigwa na Ukraine. Juzi hapa alichukua hatua ya kulipiza kisasi na kupiga miji katika maeno ya raia, jambo ambalo alijua kabisa ni kosa kubwa sana katika sisa za kimataifa. Anatapatapa (desparate) na sasa kuna wasiwasi nje na ndani ya Urusi kwamba anaweza kutumia silaha za nuklia.
Mafanikio ya Ukraine yametokana na silaha sa kisasa sana tuka NATO. Ni silaha ambazo huwezi hta kukificha kifaru, na zinafanya Ukraine waone kila sehemu silaha za Urusi zilipo na kuzipiga wanavyotaka. Urusi ndio sasa wanatambua teknolojia ya NATO kwenye kuziona silaha zake iko juu sana. Kutumia vifaru kwenye vita ni sawa na kuamua kujiua! Ukraine amepiga maghala ya silaha karibu yote yanayoonekana katika sehemu zilizochukuliwa na Urusi, na lengo sasa ni kuizuia Urusi kupeleka silaha zaidi maeneo hayo, ndio maana wanaharibu madaraja.
Na juzi hapa kajaribu kujikosha na kusema nchi za Ulaya bado zinaweza kuendelea kutumia gesi ya Urusi maana kuna bomba lipo kusafirisha gesi hii kupitia Germany. Putin ameanza kulia poo lakini Wajerumani wamekataa ofa yake.
Na pia Ulaya imeamua kwamba hata vita ikiisha hawataki tena kuitegemea Urusi kwa gesi na mafuta. Hivyo hata vita ikiisha na Putin bado akawa raisi, hali ya uchumi kwa Urusi haitakuwa nzuri kwa kuwa atakuwa na mafuta na gesi kwa wingi bila kuwa na sehemu za kuyauza. Hili litaporomosha sana bei ya mafuta na gesi duniani. Saud Arabia kwa kutambua hili ameanza kujiweka karibu na upande wa Ukraine. Wamewapa USD 400 milioni kukabili athari za makombora ya Urusi kwa wananchi.
Katikati ya mafanikio ya kivita ya Ukraine, nchi hiyo na Ulaya wanatambua kwamba hata kama Ukraine wakifanikiwa kuyaondoa majeshi ya Urusi Ukraine na kurudisha maeneo yote huku Putin akiendelea kuwa Raisi wa Urusi, kuna sku atarudi tena akiwa amejiandaa vizuri zaidi na vita itakuwa mbaya zaidi. Kwa hiyo wanaona suluhisho la kudumu ni Putin kutokuwa raisi wa Urusi, eidha kwa kulazimishwa kuondoka, au ikibidi kuuwawa (assassination). Wanasema hili ndilo lilikuwa lengo la vikwazo vya uchumi kwa Urusi na matajiri wa Urusi, na lazima lifanikiwe ili amani ipatikane.
Ndani ya Urusi, kutambua kwamba kuendelea kwa Putin kuwa raisi wa Urusi ni janga litakaloendelea kuwakabili hata kama vita na Ukraine ikiisha, kumeanza kuleta vuguvugu wanalotaka mataifa ya Ulaya - Putin aondoke kwa njia moja au nyingine. Apinduliwe? Auwawe? Moja kati ya haya mawili linakuja na litaathiri sana bei ya mafuta, hasa kuitelemsha. Watch this space
Anaongea kishabiki tuWe umemsikia nani hizi habari? Waache kutumia gesi Ili waokote kuni Kwa ajili ya kuotea moto majira ya baridi? Unawazimu bila shaka .
HajielewiAnaongea kishabiki tu
Maelezo mengi unatujazia server alafu pumba yaani kila siku ni maconsipirac yasio isha makosa ayafanye putin alafu lawama wabebeshwe west ar you serious swali UKRAIN ni nchi huru ama sio huru?Mkuu, umeandika vizuri na inaonyesha una kitu fulani ila pia kimeegamia upande fulani!
Haya mambo yana namna kadhaa za kuyaelewa ila inabidi uwe na free mind sana.
1. Kuna conspiracy zinasema vita ya kwanza na ya pili ya dunia zilikuwa planned na kuna ushahidi na kwa nini zilitakiwa zotokee, migogoro mingi huwa iko planned itokee kwa malengo ya watu au kundi fulani... kuna ushahi wa haya mambo na hata hii vita ya saiz ilishatabiriwa miaka kadhaa nyuma na watu wanajaribu kuielezea inakoelekea sema tumeamua kupuuza na kushikilia sababu nyepesi.
Unaweza kujiuliza hizi shida zote za uchumi, tafrani iliyokotea duniani, uwezekano wa vita ya nuclear kutokea ikaharibu dunia yetu viongozi wa dunia hawaoni namna ya kulikwepa... kuna ugumu gani kufanya mazungumzo ya kawaida matakwa ya putin yakasikilizwa. Na ni matakwa mepesi na yanayotekelezeka tu kuliko kuvuruga amani ya dunia. Jibu ni hawawezi kuzungumza kwa sababu wana agenda tusizozijua.
2. Kwa nini rusia alivamia na hataki kurudi nyuma... ili linasemwa kirahisi kwamba ana matakwa yake ambayo yanakuwa mentioned tu hayasemwi kiundani.. ili uelewe inabidi ujaribu kufatilia interview za viongozi wa russia at least kuanzia 2008, utajua logic yao ni kwa nini ni lazima wafanikiwe na iyo mission yao au dunia isiwepo tu... maneno ya putin ayo.
3. Tunaijua ulaya na amerika jinsi wanavotumia mifumo yao ya ubepari kunyonya mataifa mengine na kuona watu wengine ni tofauti na wao.
Kumbuka biashara za utumwa, ukoloni na mengine mengi, mpka leo na kesho bado tunachukuliwa sisi ni kama makoloni yao ushahidi upo kwene mambo mengi, yaan wanahubiri uhuru na usawa lakini wanachofanya ni tofauti, ulaya ukiondoa amerika ni sehemu ambayo ilishaishiwaga rasilimali, ndo mana utaona walitakiwa watawale mataifa mengine ili kusurvie, tumeona ushahidi mpk saiz tunaona vita ya ukraine imeonesha hawana hata uhakika wa chakula na nishati.
Ni hivi kwa miaka mingi wanaplan kurudisha hali ya zamani... yaan warudi kutumia watu wengine kama sehemu ya uzalishaji mpk saiz wanafanya ivo ila sio kwa kiwango wanachotaka. Uwepo wa russia na china zinazostawi ni kikwazo katika hilo lengo... sasa karata yao ya sasa ilikuwa ni kudistabalize russia ikiwezekana kuivamia kabisa, na unaona choko choko wanazopeleka china ili mradi tu nako kupoteze stability... lakini yote ili wafanikishe mambo yao.
Nyongeza ni kwamba mfumo wa kijamaa ndio adui wa ajenda zao kwa sabb kwene ujamaa binadamu wote ni sawa ila kwene ubepari kuna mtumwa na bepari mwenyewe.
Kuna mlundikano wa mambo mengi ili kujua wanaelekea wapi, moja ya ajenda ya ni kupunguza idadi ya watu duniani ili kutawalike vizuri, na ilo jambo ujamaa upo kinyume
Da, I say kuna watu matomaso kweli kweli. Yaani video zote za Sun jinsi Ukraine wanavyppasua silaha za Mrusi, Video za CNN wanaonyesha skari wa Urusi wanalalamika hawajala, simu za askari wa Urusi wakiongea na ndugu zao wakimtukana Putin nk, vyote hivyo hamuamini? Kweli kuna watu mna shingo ngumu.BBC wamekiri kwamba kama ni vita ya mtandaoni ukraine angeshashinda lakini kinachoendelea kwenye battle field ni tofauti hata mleta mada anategemea propaganda za western media,ukitaka kujua nguvu ya mrusi piga hesabu ya wanaomsapoti ukraine ndio utajua mwanaume ni nani!
Afadhali mtu upoteze macho kuliko kupoteza akili. Kichwa kimejaa urojo mtupu. Naona umebakiwa na akili za kulia ugali tu.Yaani unasyongelea Urus kama unaongelea mavi.
Ulizia vipi HIMARS zimeishia wapi? Urus imeonesha uimara mkubwa sana, maana kipekee imeweza kukabiliana na Madola karibia 40 yenye nguvu.
Uchumi wa Ulaya umedolola na inflation ni kubwa sana, nilikuwa huku wiki kama tatu tuache utani, Uchumi wa Uingereza unasuasua, Marekani inegeukana na Saudi Arabia, Ruble ya Urus imezidi kuimarika katikati ya vikwazo.
Swala la chakula duniani tumeona, Urus ndo ana karata muhimu hapa duniani, Marekan kapigana vita kibao lkn dunia haikuwahi kutikisika hivi.
Maghara ya silaha Ulaya yapo depleted, mnasema silaha za Urus nidhaifu, are you serious guys?
Stingers, hiwitzers, Juveline, HIMARS zote pamoja na mifumo ya ulinzi imeshindwa kumzuia Putin kupiga popote hapo Ukraine.
Saivi ni Urus Vs NATO jiulize kama ingekuwa walau Ulaya tu bila Marekani wangeweza kuhimili?
Mpaka leo Marekani kashatumia zaidi ya dola bilion 18 kijeshi hapo Ukraine yaani trilion zaidi ya 40 lkn bado Urus imeyachukua maeneo manne waziwazi na yamepiga kura Ukraine akiwa anaona na Ulaya wakibweka tu.
Dunia hii tumejua wazi kuwa Urus imeweza kuitikisa Ulaya kisawasawa na hapa tunazungumza kama mzaha lkn Ulaya inaweza kuwa deindustrialized kama hujui Marekani anatamani hili jambo litokee ili Ulaya iendelee kuwa nyanya kwake.
Yote kwa yote sisi ni watoa maoni, Putin kajitaidi kwa kiasi chake lkn pia Ulaya na Marekani hawakujua kama Uchumi wao ungeweza kutikiswa kiasi hiki China anafurahia tu huu mpalaganyiko.
Afrika hatujielewi badala ya kutumia nafasi hii vizuri tupo kupinduana tu huko Afrika magharibi, mtoto wa Mseven anaongea utoto tu anapandishwa vyeo..very hopeless
Hakuna mwamba wewe duniani ni majira tu kula mtu anayajiweke.Hakuna mtu aliyetisha kama Hitler na wakamwondoa after 2 years. Putin ni muda tu .Yeye nwenyewe Ameshaona after this winter kama ulaya hawatatumia gas yake inamaana hana cha ku offer ndio kwishei.Uchafu unaomwagwa hapo Ukraine umeshindwa kuamua mwisho wa mapambano,hata sasa wanajigeuza magaidi,wakiendelea kumtibua mwamba watakiona cha moto,endapo naye akaamua kutumia njia hizo za kigaidi 🤸🤸
Siyo silaha za kizamani tu, bali pia wana jeshi la kizamani sana lislokuwa na mbinu za kivita. Linategemea kutisha tu.Hili la kupinduliwa au kuuwawa kwa Putin ni dhahiri. Na vita hii imesaidia kuanika Russia kuwa ina silaha za kizamani sana.