Kwa ujumla vita hivi vimeiweka mahali pabaya sana Urusi. Sasa ule udhaifu wa nguvu za kijeshi umewekwa wazi, na kuonekana kuwa kumbe Urusi si chochote.
Silaha zake nyingi za kisasa, mrusi alikuwa anaokoteza parts kadhaa toka Ulaya. Baada ya vikwazo hawezi kutengeneza silaha mpya wala kufanyia marekebisho ya zile zilizoharibika. Sasa Urusi imefikia kutumia silaha za kale, silaha za wakati wa enzi za USSR, silaha zisizo na ubora wala umakini.
Askari wa Urusi, kila mmoja analazimika kujinunulia vest ya kujikinga na risasi yeye mwenyewe. Maana yake ni kama Putin anawaambia kuwa usiponunua shauri yako, unaenda kuishia huko huko.
Putin ameamua kuwapeleka mpaka wazee wenye miaka 60 mstari wa mbele, alimradi kama una mafunzo ya kijeshi. Jana, wapiganaji wawili miongoni hawa wa kuokoteza waliamua kuwaua wenzao 11, na kujeruhi wengi kadhaa waliokuwa kwenye mafunzo, kwa risasi. Jana hiyo hiyo, bogari yao moja ya mafuta huko Ukraine imelipuka moto, ni mikasa kila siku.