Watu wengi walio kwenye nchi maskini na wengine wanaochukia ubepari wameegdmea upande wa urusi, na ni kundi hilo hilo linamshabikia Rais wa Korea ya kaskazini. Hata hivyo, pamoja na madhira yaliyosababishwa na Marekani kwa nchi nyingi zilizo kinyume na msimamo wake, tunapaswa kutambua hii vita ya Russia na Ukraine, Putin ni kama yuko peke yake pamoja na ujasiri alionao. Ukraine anasaidiwa na wengi tena wazi wazi. Nchi za magharibi zinaijua urusi zaidi kuliko sisi wa mitandaoni. Kujitoa wazi wazi kuisaidia Ukraine, maana yake hazitishwi na uwezo wa urusi kama tunavyofikiri. Wako wengi wenye tekinolojia ya juu zaidi. Viinchi kama Norway unaweza kuvidharau, lakini viko mbali sana kwenye sayansi ya nyuklia. Wakati mtambo wa nyuklia unavuja huko urusi mwa miaka ya 90 waliogundua ni wasweden ndo waliwapa taarifa warusi. Pia wakati nyambizi ya kirusi iliyobeba silaha za nyuklia ilipolipuka na kuzama na baadaye kuua wanamaji wote 118. Walioweza kwenda kuifunga nyambizi hiyo ikiwa kwenye kina cha mita zaidi ya 100 ni waNorway, kumbuka warusi wenyewe walikuwa wameshindwa. Kwa hiyo, vita hii siyo nyepesi kwa urusi kama wengi wanavyofikiria. Vita inapochukua muda mrefu huharibu uchumi. Urusi inatumia gharama kubwa sana kwenye vita hii. Tena ingekuwa bora huko nyuma ikiwa imekumbatia ukomunisti, sasa hivi urusi ina uchumi wa soko huria, kama ilivyo china. Wakati huo ilikuwa siyo rahisi raia kiipinga serikali yao kwenye mission kama hizi.
Mkuu, umeandika vizuri na inaonyesha una kitu fulani ila pia kimeegamia upande fulani!
Haya mambo yana namna kadhaa za kuyaelewa ila inabidi uwe na free mind sana.
1. Kuna conspiracy zinasema vita ya kwanza na ya pili ya dunia zilikuwa planned na kuna ushahidi na kwa nini zilitakiwa zotokee, migogoro mingi huwa iko planned itokee kwa malengo ya watu au kundi fulani... kuna ushahi wa haya mambo na hata hii vita ya saiz ilishatabiriwa miaka kadhaa nyuma na watu wanajaribu kuielezea inakoelekea sema tumeamua kupuuza na kushikilia sababu nyepesi.
Unaweza kujiuliza hizi shida zote za uchumi, tafrani iliyokotea duniani, uwezekano wa vita ya nuclear kutokea ikaharibu dunia yetu viongozi wa dunia hawaoni namna ya kulikwepa... kuna ugumu gani kufanya mazungumzo ya kawaida matakwa ya putin yakasikilizwa. Na ni matakwa mepesi na yanayotekelezeka tu kuliko kuvuruga amani ya dunia. Jibu ni hawawezi kuzungumza kwa sababu wana agenda tusizozijua.
2. Kwa nini rusia alivamia na hataki kurudi nyuma... ili linasemwa kirahisi kwamba ana matakwa yake ambayo yanakuwa mentioned tu hayasemwi kiundani.. ili uelewe inabidi ujaribu kufatilia interview za viongozi wa russia at least kuanzia 2008, utajua logic yao ni kwa nini ni lazima wafanikiwe na iyo mission yao au dunia isiwepo tu... maneno ya putin ayo.
3. Tunaijua ulaya na amerika jinsi wanavotumia mifumo yao ya ubepari kunyonya mataifa mengine na kuona watu wengine ni tofauti na wao.
Kumbuka biashara za utumwa, ukoloni na mengine mengi, mpka leo na kesho bado tunachukuliwa sisi ni kama makoloni yao ushahidi upo kwene mambo mengi, yaan wanahubiri uhuru na usawa lakini wanachofanya ni tofauti, ulaya ukiondoa amerika ni sehemu ambayo ilishaishiwaga rasilimali, ndo mana utaona walitakiwa watawale mataifa mengine ili kusurvie, tumeona ushahidi mpk saiz tunaona vita ya ukraine imeonesha hawana hata uhakika wa chakula na nishati.
Ni hivi kwa miaka mingi wanaplan kurudisha hali ya zamani... yaan warudi kutumia watu wengine kama sehemu ya uzalishaji mpk saiz wanafanya ivo ila sio kwa kiwango wanachotaka. Uwepo wa russia na china zinazostawi ni kikwazo katika hilo lengo... sasa karata yao ya sasa ilikuwa ni kudistabalize russia ikiwezekana kuivamia kabisa, na unaona choko choko wanazopeleka china ili mradi tu nako kupoteze stability... lakini yote ili wafanikishe mambo yao.
Nyongeza ni kwamba mfumo wa kijamaa ndio adui wa ajenda zao kwa sabb kwene ujamaa binadamu wote ni sawa ila kwene ubepari kuna mtumwa na bepari mwenyewe.
Kuna mlundikano wa mambo mengi ili kujua wanaelekea wapi, moja ya ajenda ya ni kupunguza idadi ya watu duniani ili kutawalike vizuri, na ilo jambo ujamaa upo kinyume