Kuna jambo linaniumiza toka kwa mke wangu, nimwambieje?

Mwambie ajifunze you tube acha kumchekea 😹😹😹

Ila hata mimi kupika sijui nisiseme sana, kwani ukijua kupika chakula cha usiku lazima kupika mivyakula mingine?? Eti sisy Joannah na Pridah 🀣
Mi mwenyewe tatizo.πŸ˜„
Hamna kitu sipendi kama kukaa jikoni😭
 
Mkuu,
Tafuta sehemu,mwalimu wa kupika. Umwambie mke wako kwamba umeandaa program yako na yeye kujifunza kupika, na kwamba lengo ni kunogesha pendo na kuongeza ukaribu kupitia program.

Ukishindwa kupata mwalimu, wewe na mke wako, mnaweza kujaribu kupika kwa pamoja weekend yote, na kumpumzisha huyo dada wa kazi pia.Mnaweza kutumia videos za YouTube kujifunza chakula kimoja kimoja kwa pamoja.

Mwanamke sio kazi yake pekee kupika na wewe kula tu! Hiyo ni mentality mbovu! Wote mnaweza saidiana kwenye hili zoezi .

Husimwambie β€œhajui kupika” ni kama utakuwa unamcheka kwa kilema chake,ila fanya hayo hapo juu,utanishukuru.

Naomba Mungu anisaidie na mimi nipate mke nimpikie. dah,kweli kwenye miti mingi,hakuna wajenzi.
Asante
 
Sio kosa mbona, mie nlikuaga napika ugali una mabonge mabonge, mme wangu akanielekeza kupika vizuri, chapati ndo usiseme nlikua napika ile mikate ya yesu akanifundisha pia.....

Muelekeze, ikibidi ingieni u tube mnaelekezana mnaingia jikoni wote kimahaba.
 
Mikate ya Yesu🀣
 
Wakwendreee hukooo 🀣🀣
Chakula ni chakula muhimu ushibe usife njaa..!!
Hivi kwani mtu ukimuelekeza dada vile unataka baba apikiwe kuna shida gani?
Ukute hajui kupika ila ana mambo mengine ya maana anajua ila anaonekana tatizo kisa tu kupika
 
Hivi kwani mtu ukimuelekeza dada vile unataka baba apikiwe kuna shida gani?
Ukute hajui kupika ila ana mambo mengine ya maana anajua ila anaonekana tatizo kisa tu kupika
Gubu tu limewajaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Bora tulivyokuwa kataa ndoa
 
Mi bana kuspend hours jikoni singeweza labda siku moja moja coz kama kuchepuka atachepuka tu sasa cha kufia niniπŸ˜€
Wala tusijichoshe hata ujifanye shishi food km kuchepuka litachepuka tyuuu.!!
Tena na wapika chukuchuku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Chukua huu ushauri kama mziefu wa ndoa
Tafuta clip za mapishi ntumie
Mwambie embu jaribu hizi dodnoo za huu upishi leo
Ikiwezekana kaa nae kabisa
Ila pia usijenge distance kubwa kias hiko na mke wako tengeneza ukaribu wa kuzungumza kias kwamba jambo hilo ni rahisi kusema

Mimi najua kupika kwa sababu nimejifunza kupika nikiwa mdogo sana
Kutokana na situation ya maisha wakati najiunga secondary nilikua napika sana kwenye mashuhuli ya shule na kupikia walimu
Lakini huku nilikoolewa mimi ndo mkali wa jiko
Nilichogundua watoto hawapewi nafasi ya kupika mambo yote ni hausgel
Anakuja kujifunza akiwa mkubwa so hapitii yale makosa ambayo sisi tumeyapitia tukiwa la tano la sita huko

Pia kuna mtu in nature tu hawezi kufanya jambo flani hata umuelekeze vipi

Kwa kuanzia tafuta simple food aanze nazo
Kama wali/maarage/mboga za majani
Kuna tons of instagram pages za kupika
Mtumie tafuta namna ushare nae
Ila narudia tena kuna distance kubwa sana na mkeo kama huwezi muelezea jambo hili
Ondoa hiyo mipaka kwanza
 
Jifunze wewe mkuu, sio lazima yeye apike...

Familia nzima hamjui kupika aloo basi huwa mnakula vitu vya hovyo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…