Kuna jambo linaniumiza toka kwa mke wangu, nimwambieje?

Anauliza mdau wangu wa karibu ambaye tunaheshimiana na kushirikiana mambo mengi.

Mimi na mke wangu tuna miaka mitatu tangu tuoane,
Nampenda sana,na yeye ananipenda sana,sijawahi kushitukia usaliti toka kwake japo akiwa kama binadamu anaweza kufanya hata kwa siri ila binafsi sijawahi mshitukia ,kwani naweza shika simu yake na kuchezea huku na kule ila hajawahi hata kuonesha hataki na siku za weekend tukiwa wote ndiyo kabisa simu anaitelekeza labda ikiita ndiyo anashughulika nayo.

Suala nalotaka kushare nawe (Mimi) ni kwamba mke wangu hajui kupika , iwe wali,ugali,sijui rost lile nalolifaidi migahawani lakini sijawahi onja taste hiyo.

Yeye anapenda sana nile chakula alichopika ,hususani mida ya jioni akiandaa dinner au siku za mapumziko lakini wapi,huwa anaotea mara Moja Moja lakini asilimia 80 hajui.

Tunaye dada wa kazi ambaye ni fundi haswa tena anajua lakini mke wangu hutaka yeye asimame kama mke anipikie na nikiangalia ni kweli anastahili kunipikia,Sasa akipika basi siku hiyo mjiandae kula mataputapu,

Dada wa kazi aliwahi kusema hili wazi kwangu ila nilimkanya nikajifanyq sijui kama chakula huwa kibovu lengo nilitaka heshima kwa my wife isishuke.

Mimi mwenyewe sijui kupika zaidi ya kuchemsha tu vitu ilimradi vimeiva ila huwa si vitamu, natamani ningekuwa najua ningemfundisha mke wangu A to Z jinsi ya kuandaa misosi.

Je,nimuanzeje?

Nimwambie ukweli?

Je,lugha gani nitumie ili tusigombane?

Nampenda sana mke wangu.

Kijana mdogo anawauliza nyie wanaume wa jamii forum,hata wanawake mnaweza kuchangia.
Mkuu,
Tafuta sehemu,mwalimu wa kupika. Umwambie mke wako kwamba umeandaa program yako na yeye kujifunza kupika, na kwamba lengo ni kunogesha pendo na kuongeza ukaribu kupitia program.

Ukishindwa kupata mwalimu, wewe na mke wako, mnaweza kujaribu kupika kwa pamoja weekend yote, na kumpumzisha huyo dada wa kazi pia.Mnaweza kutumia videos za YouTube kujifunza chakula kimoja kimoja kwa pamoja.

Mwanamke sio kazi yake pekee kupika na wewe kula tu! Hiyo ni mentality mbovu! Wote mnaweza saidiana kwenye hili zoezi .

Husimwambie “hajui kupika” ni kama utakuwa unamcheka kwa kilema chake,ila fanya hayo hapo juu,utanishukuru.

Naomba Mungu anisaidie na mimi nipate mke nimpikie. dah,kweli kwenye miti mingi,hakuna wajenzi.
Asante
 
Anauliza mdau wangu wa karibu ambaye tunaheshimiana na kushirikiana mambo mengi.

Mimi na mke wangu tuna miaka mitatu tangu tuoane,
Nampenda sana,na yeye ananipenda sana,sijawahi kushitukia usaliti toka kwake japo akiwa kama binadamu anaweza kufanya hata kwa siri ila binafsi sijawahi mshitukia ,kwani naweza shika simu yake na kuchezea huku na kule ila hajawahi hata kuonesha hataki na siku za weekend tukiwa wote ndiyo kabisa simu anaitelekeza labda ikiita ndiyo anashughulika nayo.

Suala nalotaka kushare nawe (Mimi) ni kwamba mke wangu hajui kupika , iwe wali,ugali,sijui rost lile nalolifaidi migahawani lakini sijawahi onja taste hiyo.

Yeye anapenda sana nile chakula alichopika ,hususani mida ya jioni akiandaa dinner au siku za mapumziko lakini wapi,huwa anaotea mara Moja Moja lakini asilimia 80 hajui.

Tunaye dada wa kazi ambaye ni fundi haswa tena anajua lakini mke wangu hutaka yeye asimame kama mke anipikie na nikiangalia ni kweli anastahili kunipikia,Sasa akipika basi siku hiyo mjiandae kula mataputapu,

Dada wa kazi aliwahi kusema hili wazi kwangu ila nilimkanya nikajifanyq sijui kama chakula huwa kibovu lengo nilitaka heshima kwa my wife isishuke.

Mimi mwenyewe sijui kupika zaidi ya kuchemsha tu vitu ilimradi vimeiva ila huwa si vitamu, natamani ningekuwa najua ningemfundisha mke wangu A to Z jinsi ya kuandaa misosi.

Je,nimuanzeje?

Nimwambie ukweli?

Je,lugha gani nitumie ili tusigombane?

Nampenda sana mke wangu.

Kijana mdogo anawauliza nyie wanaume wa jamii forum,hata wanawake mnaweza kuchangia.
Sio kosa mbona, mie nlikuaga napika ugali una mabonge mabonge, mme wangu akanielekeza kupika vizuri, chapati ndo usiseme nlikua napika ile mikate ya yesu akanifundisha pia.....

Muelekeze, ikibidi ingieni u tube mnaelekezana mnaingia jikoni wote kimahaba.
 
Mikate ya Yesu🤣
 
Wakwendreee hukooo 🤣🤣
Chakula ni chakula muhimu ushibe usife njaa..!!
Hivi kwani mtu ukimuelekeza dada vile unataka baba apikiwe kuna shida gani?
Ukute hajui kupika ila ana mambo mengine ya maana anajua ila anaonekana tatizo kisa tu kupika
 
Gubu tu limewajaa 😂😂😂
Bora tulivyokuwa kataa ndoa
 
Mi bana kuspend hours jikoni singeweza labda siku moja moja coz kama kuchepuka atachepuka tu sasa cha kufia nini😀
Wala tusijichoshe hata ujifanye shishi food km kuchepuka litachepuka tyuuu.!!
Tena na wapika chukuchuku 😂😂😂
 
Chukua huu ushauri kama mziefu wa ndoa
Tafuta clip za mapishi ntumie
Mwambie embu jaribu hizi dodnoo za huu upishi leo
Ikiwezekana kaa nae kabisa
Ila pia usijenge distance kubwa kias hiko na mke wako tengeneza ukaribu wa kuzungumza kias kwamba jambo hilo ni rahisi kusema

Mimi najua kupika kwa sababu nimejifunza kupika nikiwa mdogo sana
Kutokana na situation ya maisha wakati najiunga secondary nilikua napika sana kwenye mashuhuli ya shule na kupikia walimu
Lakini huku nilikoolewa mimi ndo mkali wa jiko
Nilichogundua watoto hawapewi nafasi ya kupika mambo yote ni hausgel
Anakuja kujifunza akiwa mkubwa so hapitii yale makosa ambayo sisi tumeyapitia tukiwa la tano la sita huko

Pia kuna mtu in nature tu hawezi kufanya jambo flani hata umuelekeze vipi

Kwa kuanzia tafuta simple food aanze nazo
Kama wali/maarage/mboga za majani
Kuna tons of instagram pages za kupika
Mtumie tafuta namna ushare nae
Ila narudia tena kuna distance kubwa sana na mkeo kama huwezi muelezea jambo hili
Ondoa hiyo mipaka kwanza
 
Jifunze wewe mkuu, sio lazima yeye apike...

Familia nzima hamjui kupika aloo basi huwa mnakula vitu vya hovyo sana.
 
Back
Top Bottom