KUNA KIMFUKO KIDOGO CHA KARATASI NIMEKIKITA KWENYE MKOBA WA MKE WANGU

Nilitaka nikutajie jina la hiyo dawa ila nimesahau

Hiyo ni dawa ya kukufanya umpende zaidi na umtii.

Zipo mbili, Kuna Moja ya kuogea na hiyo Moja ya kuweka kwenye chakula.

Hiyo ya kuogea ni yake yeye, ili akioga uzidi kumwona Malikia

Na hiyo ya kwenye chakula, atakuwa anakuwekea wewe ili ukila, basi usiwe na kauli juu yake.

Sio Mganga, ila nimetumia uzoefu.

Wanasema tembea uone, kwahiyo tusiache kutembea Duniani
 
Nikimuuliza sidhani kama ataniambia ukweli,,,najua atatafuta namna ya kunidanganya,,,na nitamfanya aanze kufanya vitu kwa Siri,,,,maana atakuwa ashajua nishaanza kumfatilia
Sasa wewe unaamini hapa utapata jibu? Huo unga ni wewe unauona sisi tunaona picha tu sio rahisi kujua ni kitu gani.
 
Ndio maana zamani vijana walikuwa wanapelekwa jandoni. Mwanaume kamili hawezi kuweka mambo yake ya ndani mtandaoni. Kuna watu wengi ungeweza kuwauliza kuhusu suala lako badala ya kweka mambo yako binafsi hadharani.
 
Huo unga unatoka Tanga ni wa limbwata, kazi yake si mbaya ni kwa ajili ya kukukamata yaani usiuone mlango wa kutoka nje.
 
Unatumbia sisi tukujibuje ? Mke wako huwezi kumhoji ? Nani mke sasa wewe ama yeye ? Muite mueleze scenario yote ilivyokuwa,,, atakujibu
 
Ufiche. Utaona anavyohangaika na kuanza kuwa makini na mkoba wake tangu kupotea kwa kitu chake. Kama ni chema atakuuliza na kukueleza, kama ni kibaya hatokuuliza.
Mkorogee paka ah mbwa ale then uone nini? Kama ni unga wa sangoma. Rudisha kwao akaonane na kungwi wake.
 
Hakuna fatagha kati ya mme na mke na ndio maana mkaitwa mwili mmoja.
 
Asante,kwa mawazo mazuri
 
Ndio maana zamani vijana walikuwa wanapelekwa jandoni. Mwanaume kamili hawezi kuweka mambo yake ya ndani mtandaoni. Kuna watu wengi ungeweza kuwauliza kuhusu suala lako badala ya kweka mambo yako binafsi hadharan

Inaweza kuwa hivyo,,,ngoja niendelee kufuatilia kwa umakini
 
Tafu 1; Tafuta unga tofauti na huo ila uelekee kufanana na huo,weka kwenye kimfuko kama ulivyokuta halafu rudisha mkobani.
2; Tunza unakojua wewe halafu tulia kana kwamba hakuna ulichoona.
3; Weka mbadala wa hicho ulichokuta,halafu hayo mazaga yapeleke ofisini kwa Mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi,peleka kiasi na kiasi endelea kuficha.
4; Usipende kuwa na sehemu yako maalumu ya kukaa (kwenye sofa kaa kwa hamahama) ikiwezekana geuza vya kukalia juu chini uone kinacho ning'inia huko.
5; Ikiwezekana epuka matumizi ya mto wa kulalia.
6; Usipende kula pekee yako,wala kumtuma eti niletee maji ya kunywa.
7; Oya,kaa CHONJO.
 
Asante,,,kwa mawazo Bora sana ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…