Muandishi anawajibika kutuwekea audio hapa. Tusijie mahojiano wenyewe. Ama sivyo aombe radhi kwa kupitisha maneno ya RPC kuhusu binti kujiuza.
Kwa sababu, msemaji wa polisi na RPC mwenyewe wamesema kuwa RPC hakusema kuwa binti alikuwa anajiuza.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi na RPC, RPC Aliulizwa kama binti anajiuza, akasema hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahili kufanyiwa hivyo.
Muandishi wa habari akaandika kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza, kitu ambacho RPC hakusema.
Mpaka hapo, kama walichosema msemaji wa polisi na RPC ni kweli, muandishi wa habari kapotosha.
Ikiwa walichosema msemaji wa polisi na RPC ni sahihi, kuna uwezekano mkubwa kuwa muandishi wa habari kakosea kwa ujinga wake. Lakini uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba muandishi wa habari kapotisha makusudi ili auze magazeti yake.
Muandishi wa habari anatakiwa ama kukubali makosa na kutuomba radhi kwa kutupa habari potofu, ama kutoa ushahidi (kama wa audio na mahojiano) kwamba msemaji wa polisi na RPC wanafanya spinning.
Mpaka hapo tu muandishi wa habari ana a big credibility issue na haaminiki chochote alichoandika, anaonekana ni mtu wa kuungaunga habari na kuweka nukuu nje ya muktadha.
Anatakiw akujieleza kwanza.
Haya hapa maongezi ya muandishi mwingine wa habari wa Bongo FM akimuhoji RPC kutaka kupata ufafanuzi zaidi kuhusu kauki hizo tata zilizoripotiwa na Mwananchi.
View: https://x.com/habaridigital_/status/1825486215514100164?s=48&t=jWAcnldKo9nLRz35dWFJbg