Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Muandishi anawajibika kutuwekea audio hapa. Tusijie mahojiano wenyewe. Ama sivyo aombe radhi kwa kupitisha maneno ya RPC kuhusu binti kujiuza.
Kwa sababu, msemaji wa polisi na RPC mwenyewe wamesema kuwa RPC hakusema kuwa binti alikuwa anajiuza.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi na RPC, RPC Aliulizwa kama binti anajiuza, akasema hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahili kufanyiwa hivyo.
Muandishi wa habari akaandika kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza, kitu ambacho RPC hakusema.
Mpaka hapo, kama walichosema msemaji wa polisi na RPC ni kweli, muandishi wa habari kapotosha.
Ikiwa walichosema msemaji wa polisi na RPC ni sahihi, kuna uwezekano mkubwa kuwa muandishi wa habari kakosea kwa ujinga wake. Lakini uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba muandishi wa habari kapotisha makusudi ili auze magazeti yake.
Muandishi wa habari anatakiwa ama kukubali makosa na kutuomba radhi kwa kutupa habari potofu, ama kutoa ushahidi (kama wa audio na mahojiano) kwamba msemaji wa polisi na RPC wanafanya spinning.
Mpaka hapo tu muandishi wa habari ana a big credibility issue na haaminiki chochote alichoandika, anaonekana ni mtu wa kuungaunga habari na kuweka nukuu nje ya muktadha.
Anatakiw akujieleza kwanza.
Haya hapa maongezi ya muandishi mwingine wa habari wa Bongo FM akimuhoji RPC kutaka kupata ufafanuzi zaidi kuhusu kauki hizo tata zilizoripotiwa na Mwananchi.
View: https://x.com/habaridigital_/status/1825486215514100164?s=48&t=jWAcnldKo9nLRz35dWFJbg
Ukiunganisha na kauli nyingine alizosema huyu RPC ambazo hajazikanusha siwezi kushangaa kwamba aliweza pia kusema huyo binti ni kama kahaba (either kwa kumlinda mmoja wa watuhumiwa muhimu au kutokuwa sensitive vya kutosha na kesi yenyewe). Hii kesi imeshakuwa na utata mkubwa kupita kiasi, huwezi kudhania tu kirahisi kwamba mwandishi wa mwananchi alipotosha kauli ya RPC na sio kwamba RPC mwenyewe na jeshi la polisi wanajisafisha kwa sasa baada ya kelele nyingi, shughuli itakuwa kama hakuna audio, lakini pia audio inaweza kuwepo na zikifanyika jitihada za makusudi kutoka upande mmoja kuipoteza, uwezekano wa kupata kauli sahihi katika haya mazungumzo ni finyu sana. Jambo la muhimu kwa sasa ni kesi ipelekwe mahakamani iendeshwe kwa haraka iishe watu waendelee na mambo mengine.