Kuna kiongozi yeyote wa CCM kalaani kauli ya RPC wa Dodoma kuhusu binti aliyebakwa?

Hata Lucas huwezi kumsikia wala Choicevariable.

.hawana huo upendo ati.
 
Kwani RPC kasemaje? Kwa maneno yake mwenyewe. Kuna audio au video?

Mpaka sasa kuna utata wa alichosema RPC na alichoripotiwa kusema, msemqji wa Polisi kaandika waraka kuelezea hili.
Ameripotiwa kusema maneno mengi, kwa ufupi
1.Binti ni kama alikuwa anajiuza
2.Waliomfanyia hiko kitendo sio askari
3.Hata mgambo anaweza kuwa askari
4.Hawakutumwa na yeyote
5.Waliofanya hiko kitendo ni "kama" walevi na wavuta bangi tu.
 
Sasa naanza kumwelewa Samia! Kwa Watanzania, ukimya ni muhimu sana maana huwezi kuwatimiliza kila mmoja.
 
Mpaka leo kama wahusika wote hawajafikishwa mahakamani hilo nalo litakuwa ni tatizo lake. Au aseme DPP anachelewesha tuanze nae.
 

Labda baada ya wewe kuuliza... utaona...
 
Ameripotiwa kusema maneno mengi, kwa ufupi
1.Binti ni kama alikuwa anajiuza
2.Waliomfanyia hiko kitendo sio askari
3.Hata mgambo anaweza kuwa askari
4.Hawakutumwa na yeyote
5.Waliofanya hiko kitendo ni "kama" walevi na wavuta bangi tu.
Muandishi anawajibika kutuwekea audio hapa. Tusijie mahojiano wenyewe. Ama sivyo aombe radhi kwa kupitisha maneno ya RPC kuhusu binti kujiuza.

Kwa sababu, msemaji wa polisi na RPC mwenyewe wamesema kuwa RPC hakusema kuwa binti alikuwa anajiuza.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi na RPC, RPC Aliulizwa kama binti anajiuza, akasema hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahili kufanyiwa hivyo.

Muandishi wa habari akaandika kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza, kitu ambacho RPC hakusema.

Mpaka hapo, kama walichosema msemaji wa polisi na RPC ni kweli, muandishi wa habari kapotosha.

Ikiwa walichosema msemaji wa polisi na RPC ni sahihi, kuna uwezekano mkubwa kuwa muandishi wa habari kakosea kwa ujinga wake. Lakini uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba muandishi wa habari kapotisha makusudi ili auze magazeti yake.

Muandishi wa habari anatakiwa ama kukubali makosa na kutuomba radhi kwa kutupa habari potofu, ama kutoa ushahidi (kama wa audio na mahojiano) kwamba msemaji wa polisi na RPC wanafanya spinning.

Mpaka hapo tu muandishi wa habari ana a big credibility issue na haaminiki chochote alichoandika, anaonekana ni mtu wa kuungaunga habari na kuweka nukuu nje ya muktadha.

Anatakiw akujieleza kwanza.

Haya hapa maongezi ya muandishi mwingine wa habari wa Bongo FM akimuhoji RPC kutaka kupata ufafanuzi zaidi kuhusu kauki hizo tata zilizoripotiwa na Mwananchi.


View: https://x.com/habaridigital_/status/1825486215514100164?s=48&t=jWAcnldKo9nLRz35dWFJbg
 
Mpaka leo kama wahusika wote hawajafikishwa mahakamani hilo nalo litakuwa ni tatizo lake. Au aseme DPP anachelewesha tuanze nae.
Hilo la wahusika kutofikishwa mahakamani naweza kuwa nawe.

Aliyechoma picha ya Samia alifikishwa mahakamani mara moja, hawa ambao kuna ushahidi mpaka wa video kwa nini hawafikishwi? Utaambiwa uchunguzi unaendelea.

Ila mimi kwenye uzi huu nataka pia kuwamulika waandishi wa habari wanaopotosha ili kuuza magazeti yao.

Yani mtu kabakwa, halafu muandishi anapindisha maneno ili auze magazetu tu?

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi na RPC.

Mahojiano yalienda hivi.

Muandishi: Binti alikuwa anajiuza?
RPC : Hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahili kufanyiwa hivyo.

Muandishi kaandika kichwa cha habari "RPC Asema Binti alikuwa anajiuza".

This is so wrong.
 
Badilikeni
 
Hicho kilichofanywa na IGP kumtumbua RPC ni utekelezaji wa maagizo kutoka CCM,sasa wewe ukisubiri hadi mwana CCM mmoja mmoja atoke hadharani kulaani utachelewa maana CCM ni chama tawala kilichojengwa kwa misingi imara inayozingatia utaratibu wa chama tofauti na vyama vingine hivyo visivyo na utaratibu kila mmoja anatoka na kuongea anavyojisikia.
 
KWaiyo mnataka kuhamia kwa mwandishi wa habari tena
 
KWaiyo mnataka kuhamia kwa mwandishi wa habari tena

Nimeeleza kwamba siko hapa kuwatetea polisi. Wana mapungufu mengi. Mengine nimeyataja hapo juu.

Kwa mfano, hakuna sababu ya msingi watuhumiwa hawajapelekwa mahakamani mpaka leo.

Lakini pia.

Tunaweza kuongelea jambo zaidi ya moja.

If at all the police spokesperson and the RPC are correct, hapa kuna mada kubwa nyingine ya waandishi wapotoshaji wanaopindisha habari, apparently ili kuuza magazeti. Over rape no less.

Lakini watu wanamshambulia RPC tu, like simpletons, bila kuiangalia hii angle, because it is fashionable to do so.

It is a nuanced and complex detour which shows that the police could be wronged and unfairly reported on.

But we are not ready to acknowledge that.

It distracts from our simple story that the police is bad and journalists are good.

The story is not that simple.
 
Ndiyo. Mimi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…