Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Usipotoa sadaka na michango hilo kanisa lako litajiendesha je?.
Achen kulalamika na kuweka excuse nyingi kumtumikia Mungu.
Naomba usome:-
1Yohana 2:19;
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
Jambo kubwa nikuacha kulalamika maana hutapata dhawabu yoyote.
Leo hii watu wanawanyenyekea wanasiasa kuliko watumish wa Mungu maana wanasiasa wana connection nyingi.
Kama unaona utumishi ni mzigo acha kuabudu
 
Tena usijaribu kuzungumzia kuhusu swala la miradi ya kanisa. Miradi mingi imajaa upigaji mkubwa sana. Watu wanatumia sadaka za waumini kujineemesha kupitia kamati za fedha na miradi kanisani.
Una Elimu kiasi gani kuhusu usimamizi na uendeshaji wa miradi??.
NAjua utabisha kwa sababu unatetea kanisa lako.

Ila Uhishahidi upo wa kutosha kama utahitaji.
 
Sasa si uuweke hapa huo ushahidi, shida iko wapi??.
 
Kwa hiyo huyu alitaka Wakatoliki wawe wanagawiwa pesa kutokana na miradi hiyo??.
Hivi wewe mbona una andika ujinga?
Jibu swali!
Miradi ya kanisa Katoliki inawasaidia vipi waumini?
Kama haifai kuwagaia pesa kwanini kuwachangisha ili kuanzisha hiyo miradi?
Kanisa limekuwa taasisi ya wizi, inayotaka kuvuna isikopanda.
 
Katekista!!! Acha kupotosha ukweli. Misa takatifu katika ibada ya mazishi iliendeshwa na mpakwa mafuta.
Mzee Kwanini tuandikie mate wakati wino upo??,Ingia YouTube angalia mazishi ya Mzee Kingunge yalivyokuwa.
 
Sina elimu yoyote, kwa akili yangu tu inatosha kusema uwekezaji wa kanisa huendeshwa kwa gharama za waumini ambao hawagusi faida…. wao ni kuchanga tu na faida hairudi kwao.
Basi nikushauri tu kuwa si busara hata kidogo kuongea juu ya Jambo fulani ikiwa hujawahi kufanya research yoyote na huna ushahidi.
 
Mdau anauliza, mbona zamani haikuwa hivyo? Kuna bills na huduma gani zinazofanya kuwe na utitiri wa sadaka na matoleo mengi tofauti na zamani?
Zamani makanisa ya afrika yalikua yanapokea misaada sana kutoka ulaya na marekani kwa sasa misada hiyo imepungua sana..hivyo makanisa yanajitagemea.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwani wamesema usipotoa watakufungilia mashitaka??.
 
Eti? Kwani kabla ya kuletewa hizi dini kwenye ngalawa watu walikuwa hawazikwi?
 
Pole sana mkuu. Inasikitisha Sana.Meanwhile wenye pesa hata wawe na mitaala (polygamist), bado watazikwa na kanisa,. Mifano hai ipo mingi .
Hiyo mifano mingi,ungeiweka hapa angalau mitatu tu.
 
Eti? Kwani kabla ya kuletewa hizi dini kwenye ngalawa watu walikuwa hawazikwi?
 
Acha uongo bhana!!.Kingunge alizikwa na Katekista,wala hakukuwa na Misa napo ni kwa vile tu familia yake ilikuwa mshirika mzuri,pia dakika za mwisho alionyesha kutaka kumrudia MUNGU lkn bahati mbaya hakuwa ametubu.
Nipe ufafanuzi kwa nini unasema alizikwa na Katekesta ila hakukuwa na Misa...?
 
Hii kitu ni kama makanisa ya hizi taasisi yamegeza kwa hawa born again mega churches. Now wote somo ni moja. Toa toa toa toa toa toa hata mahuburi ya kuacha dhambi au kuiona pepo ni 5% @ and 95% Ni TOA TOA TOA TOA na kama hutoi hatuhudumii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…