Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!
Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.
Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!
Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??