Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.
To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.
Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.
Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.
Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?
Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.
Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.
Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.
Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?
Tumsifu Yesu kristu.
Wewe jamaa utakuwa mgonjwa wa akili, kwanza umesema mahudhurio yako Kanisani sio mazuri,Sasa kwenda tu siku moja umeleta malalamiko JF, Naomba nikuulize maswali yafuatayo na unijibu vizuri.
1.Ulipokuwa huendi Kanisani, Kwani Kanisa lilishindwa kuendesha mambo yake kisa kukosa sadaka yako??
2.Je,Kuna mtu au watu waliokulazimisha kutoa sadaka ambazo unazilalamikia hapa??.
3.Hivi ktk maisha Yako ni pesa kiasi gani huwa unatoa kugharamia mambo ambayo si ya msingi sana, Matharani kuwanunulia watu pombe,kuhongea mademu ambapo wengine wanaishia kukutosa,kutoa michango ya sendoff,harusi,n.k.Lkn hujawahi kuja hapa kulalamika?
4.Je, unadhani hayo makanisa mengine hawana michango??,Ikiwa hawana michango je,Wanajiendeshaje?,wanawezaje kujenga makanisa?, wanawezaje kulipa gharama za umeme,maji,walinzi,chakula,vifaa mbalimbali,nk.??.
5.Umewaita watetezi wa sadaka na michango kuwa Walevi wa mvinyo,Hivi kati ya wewe unayepinga na wao wanaounga mkono nani ni mlevi wa mvinyo??
6.Hivi unadhani wewe ukiacha kutoa sadaka na michango,ndio Kanisa halitasonga mbele??.Hebu jiulize miaka yote hiyo takribani 2000 liliwezaje kusambaa na kujengwa maeneo mbalimbali km sio michango ya watu wema??.Wewe umezaliwa ukalikuta Kanisa Katoliki, utakufa na kuliacha likiendelea kutamalaki.Kwa hiyo uache kusali, kuchangia wala huna impact yeyote.
Ushauri WANGU.
Chagua kuwa Mkristo Mkatoliki au wa Dhehebu jingine ambalo litaendana na matakwa yako,na Ukiona kote kugumu basi acha tu, hakuna atakayekulazimisha hutakuwa wa kwanza kufanya hivyo,kuliko kuja hapa kulia lia Bora tu ukakaa pembeni.