Tumsifu Yesu Kristu mpendwa
Nadhani changamoto ipo kwenye ufahamu wa namna ufalme wa Mungu unavyofanya kazi. Sioni tatizo kwako wala mtizamo wako maana ninatambua unachohitaji wewe ni elimu na ufahamu wa jinsi Yesu anavyotenda kazi
Basi tutaanza na neno la Mungu ili iwe rahisi kupokea elimu hii
Tafadhali soma Mathayo 25:14-30
Nitachukuwa mstari 24-26 ili upate kuelewa ufalme wa Mungu unavyofanya kazi
24 - Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
25 - Basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
26 - Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
Hoja yako kwa kanisa haina tofauti sana na hadithi hii
Kwani kinachokuumiza wewe ni kanisa kuwa na michango mingi angali wewe ndio unayefanya kazi.
Naamini kama ungali fahamu vyote ulivyonavyo sio vyako sidhani kama ungelalamika. Kitu kinachotugharimu kibinadamu ni ile hali ya kuamini kwamba hii fedha/mali ni YANGU. Pasi na kufahamu yote tuliyonayo ni matokeo ya upendo wa Mungu kwako. Kibinadamu kuamini falsafa hii ni ngumu sana maana Ipo kiroho wakati tunadhani yote tuliyonayo ni matokeo ya juhudi zetu pekee yetu.
Ukisoma mstari wa 28 utaona ni nini matokeo ya ubinafsi wa mtumwa yule.
Yesu anasema duniani kuna mabwana wawili ambao ni fedha na Mungu. Utachagua mwenyewe wa kumtumikia lakini huwezi kuwatumikia wote kwa pamoja, Ukishindwa kufahamu kama vyote ni mali ya Bwana hakika itakuwa ngumu sana kuachilia yote ulionayo kwa Mungu.
Kwa kumalizia jitahidi sana kujifunza kanuni za Mungu hasa kwa kusoma neno lake ili uongeze maarifa ya kimungu kuanzia namna ya kupata fedha/mali, kutumia na kuzalisha uli usipungukiwe ukamkufuru Mungu, maana kumcha Bwana ndio chanzo maarifa na hekima. Tena Suleiman anasema bora hekima na ujipatie hekima na kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Mwisho kasome Hosea 4 upate kufahamu nini kinachoangamiza Imani. Usilaumu kanisa jilaumu wewe kwa kuwa gizani.
Uwe na jumapili njema ya matawi na nikutakie kwaresma njema.
Tumsifu Yesu Kristu.