Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Ni kwa nini vifungu vya Biblia unavyonukuu wewe uone ndio sahihi na mimi nimekuwekea verse moja tu ya Timotheo unataka kuaminisha umma wa JF kwamba hiyo siyo biblia?

Au tukubaliane kwamba Biblia ni magumashi inajipinga yenyewe?

Namuarika Kiranga sasa.
 
Jinga kabisa wewe
 
Poleni sana
 
Upigaji umeingia sehemu nyingi Sana.Mimi mtanisamehe nilishachaga kwenda kanisani.

Nimekuwa mkristo mfu.
 
Nipe ufafanuzi kwa nini unasema alizikwa na Katekesta ila hakukuwa na Misa...?
Mzee Misa huongozwa na Wapakwa mafuta tu, yaani Padre au Askofu.Akiongoza Katekista hiyo sio misa bali ni Ibada tu.Ili iitwe misa lazima iwe na sehemu kuu mbili yaani Liturujia ya Neno na Liturujia ya Ekaristi Takatifu,sasa Mwenye mamlaka ya kuadhimisha sehemu zote Liturujia hizi mbili ni padre au Askofu, Kumbe Katekista yeye anaadhimisha tu sehemu ya Liturujia ya Neno, hawezi kuadhimisha Liturujia ya Ekaristi Takatifu.
 
Umepuyanga sana ndugu, hakuna sehemu nimepinga sadaka wala michango kanisani.

Rudi post namba nilichoandika utaelewa napinga nini.

Kwa taarifa yako parokia yetu ina miaka 40 na mimi ni ministrant wa kwanza wa parokia na tumezaa parokia tatu, mimi siyo intruder naandika ninachokijuwa ma nimekulia kanisani lakini siyo kanisa hili la leo.

Mhadhama Polycaply Cardinal Pengo akiwa ndio Askofu wetu mkuu wa jimbo kuu la Dsm alikuwa akiwa na shida ya pesa ya matumizi alikuwa akituomba jimbo zima kila mwana kaya amchangie pesa ya matumizi sh 100 tu, ambayo ukijumlisha wana kaya wote wa jimbo kuu la Dsm alikuwa anapata tsh million 400 cash. Je ni nani wa kumnung'unia Kadinali Pengo kwa kuomba achangiwe tsh 100 tu?

Msidhani hatuna akili, sasa ukiacha Charismatic ambao mliwapinga, subiri movement za UAMSHo ndani ya kanisa katoliki kuwakombowa mazezeta wasiojielewa wanaodanganywa na kauli mbiu ya Vaticano kwa Roma ikiongea ni Finito causa.

UAMSHO unakuja zaidi ya ule wa kina sheikh Farid.
 
Walutheri wanazo sadaka nyingi Ni kweli, ila Cha ajabu wanazidi kukusanya washarika kila uchao na kwa huduma za kiimani na kiroho katoliki hamuwafikii hata robo,,
 
Ukifa hawakuziki. Hapo ndipo wametushika pabaya
Mkuu Aikambee; Hivi bro, ulishaona mtu amekufa halafu akaacha kuzikwa??? Ukisha RIP watu bila kujali urembo wa nje eti uzikwe na Padri, Shemasi, Katekista, Mchungaji etc.Iwepo kwaya, cjui nani, nini-UTAZIKWA TU. Watakaokuzika ni watu wenzio bila kujali imani zao. Kwani zamani (Kabla ya hizi dini)watu wakifa walikuwa hawazikwi? Ifike mahali Upatikanaji wa hizi huduma kusitumike kama fimbo ya kutuchapia! eti unamwadhibu Marehemu. Hii sio sawa.
 
Shukurani kwa ufafanuzi.....Ni Marehemu wa aina gani anastahili kuongozwa na Padri ama Askofu, na huyu anaeongozwa na Katekesta sifa zake ni zipi.?
 
Upigaji umeingia sehemu nyingi Sana.Mimi mtanisamehe nilishachaga kwenda kanisani.

Nimekuwa mkristo mfu.
Sawa,baki hivyo hivyo,na uwaambie na ndugu zako wote kuwa siku ukifariki wasiwasumbue Watumishi wa MUNGU kuja kukufanyia ibada ya mazishi.Maana watu km nyie huwa mnakuja kuleta shida mkiwa mmefariki na Ndugu zenu wanaanza kulilaumu Kanisa kuwa halipo fair Kumbe ninyi wenyewe mlijichagulia kuishi pasipo kuwa na mahusiano mema na MUNGU,kwa kujitenga na Kanisa (Excommunication).
 
Badili heading mkuu usijumuishe au usisemee makanisa yote. Andika kuna kitu hakipo sawa kanisa la RC.
Umewahi kujiuliza kwanini hakukuwa na michango miaka ya nyuma na sasa IPO?
 
Mkuu ukitaka kujuwa mimi ni mkatoliki kindakindaki ni kwamba Kinyerezi kilikuwa ni kigango cha kanisa la Parokia ya Segerea na hiyo nyumba ni ya kisasa na imenunuliwa kwa Tsh million 400 kutoka kwa mwanaparokia wa hapohapo kinyerezi.

Watu wasidhani tunaandika hapa kuchangamsha baraza, ni kwamba imetosha hatuwezi tena kukubaliana na uhuni huu eti kisa kuna wapakwa mafuta amesema abcd.
 
Padre au Askofu wote wametumwa fedha
 
Upo sahihi kabisa mkuu, imagine ile nyumba eti haina hadhi ya padre kuishi
Nadhani wanataka waipate pepo hapa hapa
 
Pandikizi!
 
Kwani wamesema usipotoa watakufungilia mashitaka??.
Hakuna mashtaka lakini unapata restrictions ktk huduma.
Haya mambo yakiachwa yaendelee tunazidi kuwapa umungu wasioustahili

Walianza na kutokuwapa huduma za ndoa, ubatizo nk wale wasiochangia, wakaja na kukataa kutoa ibada ya maziko, tukinyamaza kesho itakuwa unaingia ibadani kwa ID
 
Mzee Kwanini tuandikie mate wakati wino upo??,Ingia YouTube angalia mazishi ya Mzee Kingunge yalivyokuwa.

Nipe ufafanuzi kwa nini unasema alizikwa na Katekesta ila hakukuwa na Misa...?
Kwa ninavyojuwa mimi ibada ya misa ya mazishi ikishafanyika kanisani na kuongozwa na Padre si kazima Padre kwenda makaburini, ni katekista anaachiwa hilo jukumu.

Labda mwambie akujibu swali hili ni kwa nini watu wengine hawakuishi maisha yoyote ya utakatifu lakini wanazikwa na Askofu na siyo Padre?

Ikumbukwe Askofu ndio daraja la juu kabisa katika kanisa kuliko Kadinali, ingawa makadinali wengi ni maadkofu ila hata Padre au Shemasi anaweza kuteuliwa kuwa Kadinali kwa mujibu wa canon law na imeshatokea Padre Ujerumani aliteuliwa kuwa kadinali lakini siyo Askofu, anakuwa tu ni mjumbe wa Conclave kumchaguwa Papa inapotokea uchaguzi wa Papa mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…