Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
- Thread starter
- #321
Ni kwa nini vifungu vya Biblia unavyonukuu wewe uone ndio sahihi na mimi nimekuwekea verse moja tu ya Timotheo unataka kuaminisha umma wa JF kwamba hiyo siyo biblia?1 Wakorintho 7:32-35
32 - Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 - bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
34 - Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 - Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
Mathayo 19:10-12
10 - wanafunzi wake wakamwambia, mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 - Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
12 - Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Au tukubaliane kwamba Biblia ni magumashi inajipinga yenyewe?
Namuarika Kiranga sasa.