Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
Huwa nawashangaa watu wanapolalama kwenye institution ambayo kujiunga na kutoka ni hiyari na tena haulazimishwi kutoa chochote.
Kama unaona makanisa yaliyopo hayafai, si kasajili la kwako Wizara ya mambo ya ndani uweke utaratibu unaouona unafaaa?
 
Hiyo sio sbb, sadaka za Jpili peke yake zinatosha sana, na kanisa ina miradi mikubwa mingi sana, iweje ikamue waumini kiasi hicho.

Kwnn kanisa liwe na matumizi makubwa hivyo, kisa ni nn? Yesu hakuwa na hayo yote, ukiona hivyo ni binadamu wanakula fedha hizo na kuzitumia sbb zinapatikana bure bure.

Mimi kanisani naenda wakati wa Pasaka na Christmas tu, siku nyinginezo nasali kwangu na familia yangu, makanisa yamekuwa tofauti kabisa, ni kukusanya fedha na michango isiyoisha, imekuwa biashara ya uhuni sana, narudia, Yesu Kristo hajawahi kuwa hivyo, full stop
Yesu na ukiristo ni vitu viwili tofauti
 
Nani kakudanganya! utatengwa, na hata katekista hawezi sogelea mzoga wako.
Kumbe unataka bado kuwa sehemu ya taasisi na bado hutaki kufuata utaratibu uliopo?
Hama nenda unakoona panafaa. Kama hakuna sajili kanisa lako ujipangie taratibu zako!
 
Mkuu nyumba za mapadre zinazojengwa siku hizi haziingiliani na huduma nyingine za waamini.
Hiyo ninayosema ipo ndani ya uzio wa kanisa lakini ina uzio wake humo ndani kutenganisha na kanisa
Hao Mapandre inaonekana ni vijana(sina uhakika) au Wana lao jambo.
 
Huwa nawashangaa watu wanapolalama kwenye institution ambayo kujiunga na kutoka ni hiyari na tena haulazimishwi kutoa chochote.
Kama unaona makanisa yaliyopo hayafai, si kasajili la kwako Wizara ya mambo ya ndani uweke utaratibu unaouona unafaaa?
Kwa kiasi kikubwa ruzuku kutoka Vatican imepungua au kuondolewa kabisa. Kanisa la miaka ya 40,50,60 lilieneza Injili Afrika, sasa ni wakati wa Afrika kuisimamia Injili ienee kwa watoto wetu.
 
Anayelalamika ni huyo ambaye ameshakiri mwenyewe kuwa sio muumini mzuri. Kwanza alishasema hana dini, soma hapa:
Wewe ni kichaa, mimi sijafungia akili zangu kwenye kabati la paroko, ni wapi nimesema sina dini?

Hapo nilihoji kama ninavyohoji leo, akili zangu si kama zako shake well before use.
 
Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.

Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
Wafadhili siku hizi hawapo, kwa hiyo ni lazima kuwepo na mbwembwe zakupata fedha
 
Kwa kiasi kikubwa ruzuku kutoka Vatican imepungua au kuondolewa kabisa. Kanisa la miaka ya 40,50,60 lilieneza Injili Afrika, sasa ni wakati wa Afrika kuisimamia Injili ienee kwa watoto wetu.
Kama unaufahamu vizuri ukatoliki ruzuku hazikuwa zinatoka Vaticano, bali ni mashirika ya kitawa ndio yalikuwa yanaboost, pale ambapo walipoona malengo yamekamilika walihamia sehemu nyingine.

Madhehebu ya Kilokole sasa hivi ndio yanapata ufadhiri kutoka kwa wazungu wa madhehebu hayo ili kuyapa nguvu, nao target yao ikikamilika hutoona hawa manabii wakiendesha tena magari ya kifahari na kulindwa na bodyguard, hizo zote ni jeuri ya hela za wazungu ukichanganya na sadaka za mazezeta ni full kunoga.
 
Kusema kweli kusali niliaacha kitambo..
Watumishi wamegeuka walanguzi wafanya biashara wa&@nzi waongo walaghai matapeli kuvuruga nyumba za watu kuwatia watu hofu eti 'usipokuja kusali ukifa kanisa halikuziki....

Wazazi wetu wanashindwa kujikimu kimaisha ukiwapa pesa kidogo anakuambia ongeza na ya kanisani sijui fungu la kumi na sadaka za ujenzi nk

Serikali ikemee haya ama sivyo walipishwe kodi kwani Makanisa ni biashara
Mungu yupo ulipo ukiomba anasikia fungu la kumi katembelee na kuwasaidia wenye uhitaji wagonjwa sio kupeleka pesa kanisani huku ni kujengeana umaskini wa kulazimisha

Funga makanisa watu wasali majumbani

Mtoa Mada Asante sana kwa ujumbe huu


Milele Amina
 
Makanisa mengi ya kikristo yaliletwa Afrika na wamisionari wa kizungu, sana wa ulaya magharibi na Marekani.
Uendeshaji wa makanisa haya kwa sehemu kubwa zilibebwa na hawa wamisionari. Walilipa mishahara ya wachungaji au mapadri na watenda kazi wote wa makanisa aidha waligharamia matibabu yao mpaka elimu yao.
Kwa ujumla walifanya kila kitu. Baadaye ilitokea kuanguka kwa ukomunisti ulaya ya mashariki ikiongozwa na urusi (Soviet Union) au USSR, ambako kwa itikadi zao hawakuwa wakiamini dini.
Baada ya anguko la ukomunisti wamisionari waliona haja ya kuanza kupeleka injili huko ulaya mashariki,na ikumbukwe wale Ni wazungu wenzao au ndugu zao.
Gharama za kuendesha upelekaji wa injili kwa kiasi kikubwa zilibebwa na hawa wamisionari kutoka Marekani na Ulaya magharibi na misaada iloyopelekwa huko kwa vyovyote ilikuwa ni mikubwa kuzidi iliyoletwa Afrika.
Na hivyo ilipelekea kupungua kwa misaada iliyokuwa ikiletwa Afrika.
Ni wakati huo ndipo siye waafrika tulijikuta tunabeba mzigo wa kugharamia shughuli za injili wenyewe na ni kitu ambacho hatukuwa tumezoea na haswa wakatoliki,wao hawakuachwa mapema kama walutheri au Protestants wengine.
Kumbuka ulutheri ulianzia ujerumani na ulipokea misaada mingi zaidi toka ujerumani japo kuna nchi chache pia za ulaya haswa scandinavian countries zilikuwa zikichangia.
Hata hivyo kushindwa kwa ujerumani kwenye vita vya dunia kwa maana ya kwanza na ya pili kuliathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa wajerumani na automatically misaada ya kuendeshea shughuli za kanisa pia ilipungua sana na kupelekea gharama za uendeshaji wa makanisa kuwa mikononi mwa waumini.
Hata hivyo naomba nikuhakikishie hakuna hasara kwenye kumtolea Mungu au kutoa sadaka. Mungu siyo maskini kutegemea hela zako,isipokuwa ameagiza utoe sadaka kupima discipline yako kwake. Alipomwambia Ibrahim amtoe.mwanawe wa pekee Isaka,hakuwa na shida na Isaka alitaka kupima discipline ya Ibrahim kwake. Toa sadaka usiangalie inaenda kufanya nini hiyo siyo kazi yako,hao wanaoifuja Mungu ndiye atadeal nao,wewe kazi yako inaishia kutoa tu.
Jaribu kutoa bila kunung'unika hutajuta mkuu.
Utashangaa baraka ambazo utazipata na zaidi utakuja kujuta kwa nini ulilalamika humu.
Mungu akubariki.
 
Hakuna mashtaka lakini unapata restrictions ktk huduma.
Haya mambo yakiachwa yaendelee tunazidi kuwapa umungu wasioustahili

Walianza na kutokuwapa huduma za ndoa, ubatizo nk wale wasiochangia, wakaja na kukataa kutoa ibada ya maziko, tukinyamaza kesho itakuwa unaingia ibadani kwa ID
Eti unaingia Ibadani kwa ID🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Niungane na mwanzisha mada...ni hivi hao jamaa wana miladi lukuki inasaidia waumin,mfano wana shule zao kama ile ya mbagala unakuta ada imechamka balaa mtt wa hoehae asomi pale na shule kanisa.Sasa inakuwa na tofauti gani na shule za watu binafsi ,naomba tuweke hisia pembeni tuweke facts.
 
Back
Top Bottom