Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji


Mkuu mbona ulicho quote ni kile kile, amezaliwa amejikuta yeye ni Mrc hivyo hana budi kuamini alivyorithishwa.... post ya pili anahoji ina maa waafrika hatuna imani zetu za asili
 
Huwa nawashangaa watu wanapolalama kwenye institution ambayo kujiunga na kutoka ni hiyari na tena haulazimishwi kutoa chochote.
Kama unaona makanisa yaliyopo hayafai, si kasajili la kwako Wizara ya mambo ya ndani uweke utaratibu unaouona unafaaa?
Sawa na kusema mtu alietapewa, ametapeliwa kwa hiyari yake...
 
... amezaliwa amejikuta yeye ni Mrc hivyo hana budi kuamini alivyorithishwa....
Kwa umri aliofikia hadi kujiunga JF mwaka 2010, ni dhahiri unamtosha kuwa ameshaamua kuendelea na dini ya waafrika, ambayo haina mabenchi ya kuinuliwa mara saba kwenda kutoa sadaka
 
Mimi naamini sadaka na zaka ndio michango ninayopaswa kutoa......
hayo mambo mengine yamekaa kimchongo zaidi
Mm pia natoa sadaka tu na zaka
Mm najiulizaga pia..
Sadaka ya jumapili inakua zaidi ya millioni 1
Lakini utaambiwa Mavuno, mara Pasaka kuwalisha mapdre hio menu unakuta kila jumuia inajirudia rudia
Najiulizaga sana
 
Sisi leo tumeingia saa moja kasoro,ibada ikaanza saa moja kamili,tulianza kwa kuimba hadi saa tatu na robo,mahubiri yakaanza hiyo tatu na robo hadi saa sita na dakika 25,ikafuata sadaka session,hiyo ilienda hadi kama saa saba kasoro kidogo,ikafuatia mnada wa sadaka,ikaenda sijui hadi saa nane kasoro,ndiyo tukatoka,tukasimama hapo nje kuagana kwa dakika tano,nilipoingia kwenye gari niondoke mara mwinjilisti kagonga dirisha,eti samahani mtumishi,naomba usiondoke,tuna kikao kifupi cha kama robo saa tu hivi,nimetoka hapo saa kumi na madakika yake,na bado kuna semina inaendelea ndani
 
isingekuwa hofu ya kifo,jehanamu na kutokuzikwa na kanisa,watu wengi wangeshazipiga chini hizi dini
 
Hongera Sana Mkuu, MUNGU akubariki sana.
Amina kiongozi. Matoleo hayakuanza Leo tangia Kaeni na Abel miaka mingi nyuma. Leo hii kijana shababi analalamika bahasha ya elfu 10. Kila sehemu kuna michango haya makanisa na misikiti hayajashuka tu kama mvua yamejengwa na michango ya watu
 
Siku hizi mamilooo, usipotoa ni kosa kwani wanaangalia registaa, hivyo huduma za kikanisa kama vile ubatizo, ndoa nk haupati.
Hata Ukipata Msiba usipoangalia unaweza ita Shehe akufanyie ibada maana Kanisa linagoma,mchungaji harushi mguu msibani.

Bahasha ya ahadi lazima iwe imechangamka changamka kidogo umejaza raw kazaa palee.
 
Mimi naamini sadaka na zaka ndio michango ninayopaswa kutoa......
hayo mambo mengine yamekaa kimchongo zaidi
Watu ni ngumu kuelewa. Ni kweli kanisa litajengwa na waumini
Kanisa litajengwa na Waumini (Absolutely !!!).
Hii kitu ingawaje kila mtu anaichukulia kwa mtizamo wake but kumekuwa na ongezeko la malalamiko kuhusiana na hili kutoka kwa waumini. Baadhi wamejikuta wakiacha kwenda kanisani na hata kuamia kwenye makanisa ya upako ingawaje huku nako kuna changamoto zake kwani mengine yana muelekeo ya kiutapeli.
Michango ina umuhimu katika ujenzi wa Kanisa na nia ya waumini kutoa ipo ila isipitilize, iwe pale ambapo kuna ulazima wa kufanya hivyo, itolewe kulingana na uwezo wa muumini, na isipelekee ubaguzi au muumini kutengwa kihuduma kisa tuu ameshindwa kutimiza hilo na sii kwa makusudi bali ni kutokana na hali halisi ya kipato/kimaisha aliyonayo muumini husika.
 
Hata Ukipata Msiba usipoangalia unaweza ita Shehe akufanyie ibada maana Kanisa linagoma,mchungaji harushi mguu msibani.

Bahasha ya ahadi lazima iwe imechangamka changamka kidogo umejaza raw kazaa palee.

[emoji3]
 
Tatizo ni maneno laini amna ndio nimeliona
 
Siku hizi mamilooo, usipotoa ni kosa kwani wanaangalia registaa, hivyo huduma za kikanisa kama vile ubatizo, ndoa nk haupati.
Unajua kwamba kwa sasa kuna wimbi kubwa la makanisa ya wachungaji binafsi, kwa hiyo lazima Paroko ajiridhishe na Ukatoliki wako. Sasa kama rejesta inaonyesha hauhudhurii jumuiyani, na kanisani hauonekani, ni ishara gani hiyo? Kwamba unawezaje kujiita Mkatoliki wakati haushiriki jambo lolote linaloelekezwa na Kanisa Katoliki? Ndoa hutaki kufunga, unaishi tu na mtu wako, nani atakuchukulia kama wewe ni Mkatoliki? Hakuna Paroko atakayekunyima huduma kwa kigezo cha kutoa fedha, ila ubatizo, ndoa na mahudhurio kanisani vinaweza kukuondolea sifa
 
Amina kiongozi. Matoleo hayakuanza Leo tangia Kaeni na Abel miaka mingi nyuma. Leo hii kijana shababi analalamika bahasha ya elfu 10. Kila sehemu kuna michango haya makanisa na misikiti hayajashuka tu kama mvua yamejengwa na michango ya watu
Si ndio hapo!!!, Halafu unakuta pesa yake anaimalizia kwenye ishu za kipuuzi kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…