Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

[emoji1][emoji1][emoji1]Dini zote hawakupi mwanya wa kuhoji. Yaani mtu mmoja aliyejipa utumishi akisema kasema. And this is how religion was brought to Africa by missionaries to silence any spirit of consciousness. Times have changed na watu wanaanza kuquestion.
 
Dini hizi aisee[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Hivi ile sanamu tunayotembea nayo shingoni ni lazima kuvaa?
Hebu nikuuulize, uliwahi kujiuliza ilikuwaje wewe ukawa dhehebu ulilopo? Je ulishawahi peleleza nani alikuwa chambo mpaka ukajikuta uko humo ulipo?
 
Guys wake up! Hawa jamaa wanapenda maisha mazuri usipime. Yaani unakuta mnamnunulia padri orado wakati hata boda huna. Mzazi wako aliyekuzaa hana hata sehemu ya kuishi ila ukoradhi hata hrla ya kula usimtumie umjengee padre gorofa! Ama kweli haya maajabu ya Afrika
 
Waislamu wanajali sana muda yaani wao siku ya Ijumaa wanaingia kama saa saba na ushee lakini saa nane tu tayari walishatoka.
Halafu zile sala zao fupifupi yaani ni Kama kanu saa au dakika 20 tu hao duh.
Time management hapa wapo vizuri.
Dini zote hizi zilikuja na meli na mashua na waliua za kwetu pambaneni nazo
 
Dogmatism
 
Hayo ni maoni yako na kundi lako, maoni yasiyo na uthibitisho wowote.
Usitumie uongo kuhalalisha maovu yako na unajua fika uongo ndio silaha kubwa ya Ibilisi.
 
Hao Waislamu wa wapi unaowazungumzia [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hawahawa wa mtaani kwetu au
 
guys ! sikuzote kaa mkijua padre au mchungaji hawezi kukupeleka kwa mbingu( kama waamini mbingu). Matrndo yako ukiwa hai yatakupeleka. Hivyo basi wakuzike wasikuzike hawasaidii chochote. Hata ukizikwa na jiji poa tu
Sikubaliani na falsafa yako! Umesahau kuwa imeandikwa kuwa litakalofunguliwa duniani litafunguliwa mbinguni? Je, unajua ni mateso yepi waliobaki duniani hasa ndugu zako wanapata kwa Padre kutokuzika? Kuzikwa na Padre muhimu sana na hii haikuhusu uliyefariki bali waliobaki hai
 
Kwani usipozikwa na kanisa inakuharibia nini wewe uliyekufa??
Hata ndugu wa marehemu waliobaki hai haiwasaidii chochote. Ni basi tu tumeshafanya mazoea ya kuona umuhimu wa kuzikwa na viongozi wa dini kutokana na indoctrination yenye malengo mahususi kutoka kwa wanufaika wake.
 
Ulishawahi kusikia wafu wawili ambao enzi za uhai wao matendo yao yalikuwa ni ya aina moja yaani kutoenda kanisani, kutotoa michango n.k. lakini kutokana na umaarufu na/au utajiri wa mmoja wao akazikwa na padri/mchungaji na mwingine akakataliwa kuzikwa na kanisa? Kwamba kwa vile la huyo mtu maarufu au tajiri "limefunguliwa duniani" hata huko mbinguni limefunguliwa kiasi kwamba na ndugu zake waliobaki hai mateso watakayopata yatapungua tofauti na mateso watakayopata ndugu wa yule asiye na umaarufu au utajiri?
 
Umeambiwa ya kaisari mwachie yeye na ya mungu mwachie mungu! Maana yake ya duniani waachie wanadamu walio hai na ya mbinguni mwachie Marehemu! Nani alikufa akarudi duniani kutusimlia? Kuzikwa na Padre ni muhimu na akikataa inaacha simanzi kwa wanaobaki hai.
 
Hayo ya kumwachia Kaisari badala ya kuhoji na kupata logic, hitaji la kuzikwa na padri na mengineyo mengi ndiyo indoctrination tunayozungumzia. Wanufaika walishaanda kauli za kukataza watu kuhoji sana na kujenga hofu kwanza ili wengine wabaki kufuata maelekezo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…