Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Siku hizi wamejanjaruka hawakatai kuzika hata kama ulikua huhudhurii. Wanachofanya ni kwamba mkienda kuomba huduma ya ibada ya mazishi na kama marehemu alikua sio mchangiaji, basi mnapigiwa mahesabu ya michango yote ambayo alitakiwa kulipa. Kuna jamaa tulilipa laki 6 ndio padri akakubali kuja. Ukiona padri hajaja kabisa ujue ndugu wameshindwa kulipa "deni" la michango!
 
Dini ni scam tu,njia ya kucontrol watu,ndo mana watoto wangu sitaki wawe chini ya mnyororo wa dini wawe huru.
 
Kili imani yako ukiwa hai utazikwaje kama ulikataa kuikili?
 
Ndiyo maana nimesema wewe siyo mkatoliki tena, itakuwa unajilazimisha tu ili uwe huru ubadili dini uwe Muslim, maelezo yako yanakuelezea na kuonyesha imani yako juu ya dini inaelekea upande hupi.
Huyo ni mkatoliki kabisa na asemacho ni kweli bila chenga. Hata mm ni mkatoliki naunga mkono home yake. Katoliki ukusanyaji wake wa fedha hata hao TRA wakasome.

Ili wakuhesabu unafaa huduma zao, lazma wajue kama unasali jumuia. Na huko jumuia ndio kuna michango na mikusanyo ya fedha isiyo mithilika. Kwa nyongeza tu, hata shule za katoliki bei ipo juu kama za watu binafsi, na zina michango na mahitaji ya malipo ya ajabu sana. Hata Mia ikipungua wanamtimua mtoto. Kwanza kuzipata tu hizo shule kwa mzazi alieshiriki michango ya ujenzi ni shida, hata kama mtoto ana vigezo.

Mleta mada kaeleza vyema sana, kuwa kama vyanzo vya mapato kama kumbi Mashule mahospitali frame za maduka vimejengwa kulisaidia Kanisa, sasa kuna haja gani ya kukakamua namna ya uporaji waumini walioshiriki ujenzi wake kwa fedha zao?

Hakuna mahali imeandikwa kwny biblia kuwa Utaenda mbinguni kwa kutoa sadaka au hutoenda kwakua hutoi sadaka. Unadhania Yesu alipo mwambie yule jamaa kauze ulivyonavyo uwape masikini kisha unifuate, angekuwa hawa mapadiri au wachungaji wa sasa, angesemaje kama sio kusema kauze ulivyonavyo kisha uvilete hapa ndio unifuate.
 
Hii nimeipenda maana rambirambi zinaweza kuokoa jahazi. Ni uchuro kwa ndugu waliobaki kuona ndugu yao hakuzikwa na Padre!
 
Hujaelewa hoja yangu! Mimi nazungumzia ubinadamu tu. Masuala ya Mungu mimi siyazungumzii maana hakuna aliyekufa akarudi akatusimulia ni nini kipo huko. Nasema tunajua hapa kwetu mtu ukifa unazikwa na Padre au mchungaji. Hii haikuhusu wewe uliyekufa ila wale ndugu zako wanaobaki duniani inakuwa aibu yao. Ni vyema tukajitahidi kutoletea wasiohusika aibu zisizowahusu
 
Unafikiri ni nani ambaye anazuia usihoji au ambaye anatakiwa kujibu hoja zako kwenye dini?
 
Halafu bila tone la aibu wanataka serikali iwaondolee kodi.
 

Very sad [emoji22]
 
Dini zote hizi zilikuja na meli na mashua na waliua za kwetu pambaneni nazo
Ni waafrika tu ndio nadhani tunawaza hivyo, ukiangalia hizo dini zipo sehemu kubwa tu duniani ila hatuoni wengine kulalamika kwamba imani za mababu zao kuachwa na watu kufuata imani zengine.

Imani za asili ya India zimesambaa sana huko Asia katika nchi mbalimbali ila hatuoni hizo nchi kulalamika kwamba watu wao wameacha imani za mababu zao na kufuata dini za wahindi.
 
Huwa nawashangaa watu wanapolalama kwenye institution ambayo kujiunga na kutoka ni hiyari na tena haulazimishwi kutoa chochote.
Kama unaona makanisa yaliyopo hayafai, si kasajili la kwako Wizara ya mambo ya ndani uweke utaratibu unaouona unafaaa?
Sorry bro! Unachojaribu kukitetea hapa ni kipi?
 
Aya ya mwisho tayari inathibitisha wewe siyo mkatoliki.
Huyo jamaa..ni mamluki..sio mkristo fuatiria uzi zake utajua hilo..kaja kuleta hoja za kuvuruga kanisa la Mungu..atabue kutoa ni upendo..muumini wakweli hawezi kuacha kutoa sadaka kanisani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu fikilia Sana imani zingini ni kukomoana tu bora waislamu ya menyewe ni kuswali tu basi.
Wavaa kobazi ni bahili hatari..wategemezi kila kitu wafanyiwe na waarabu..hadi tende wanasubiri waletewe na waarabu.

Ukristo ni dini ya upendo na utoaji..kama huna hela kaa kimya sio kutaka kuharibu utaratibu na tamaduni za wakristo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Waislamu wanajali sana muda yaani wao siku ya Ijumaa wanaingia kama saa saba na ushee lakini saa nane tu tayari walishatoka.
Halafu zile sala zao fupifupi yaani ni Kama kanu saa au dakika 20 tu hao duh.
Time management hapa wapo vizuri.
Hata kuhoji tu hujui..sasa unataka watumie masaa mangapi kama kwa siku wanasali zaidi ya mara 5..hao ndio hawana time management.

Wakristo siku 6 piga kazi siku moja ni kupumzika na kuabudu...na zile sala ndogo ndogo binafasi..sasa wepi wanaofanya time management nzuri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwakweli waislam ukiugua hata mskitini inasemwa unachangiwa bd kuna wale wa kujitolea kutembelea wagonjwa wasojiweza na kuwapa misaada ya vyakula na dawa
Hivi si mkawe waislamu nani kawakataza..huwezi ubeza ukristo mana hiyo ndio kanuni yake ya upendonna kujari.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…