Akhi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2021
- 3,380
- 5,906
Ukishaanza dhihaka basi hua nakupotezeaHao Waislamu wa wapi unaowazungumzia [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hawahawa wa mtaani kwetu au
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukishaanza dhihaka basi hua nakupotezeaHao Waislamu wa wapi unaowazungumzia [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hawahawa wa mtaani kwetu au
Siku hizi wamejanjaruka hawakatai kuzika hata kama ulikua huhudhurii. Wanachofanya ni kwamba mkienda kuomba huduma ya ibada ya mazishi na kama marehemu alikua sio mchangiaji, basi mnapigiwa mahesabu ya michango yote ambayo alitakiwa kulipa. Kuna jamaa tulilipa laki 6 ndio padri akakubali kuja. Ukiona padri hajaja kabisa ujue ndugu wameshindwa kulipa "deni" la michango!Umeambiwa ya kaisari mwachie yeye na ya mungu mwachie mungu! Maana yake ya duniani waachie wanadamu walio hai na ya mbinguni mwachie Marehemu! Nani alikufa akarudi duniani kutusimlia? Kuzikwa na Padre ni muhimu na akikataa inaacha simanzi kwa wanaobaki hai.
Dini ni scam tu,njia ya kucontrol watu,ndo mana watoto wangu sitaki wawe chini ya mnyororo wa dini wawe huru.Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.
To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.
Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.
Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.
Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?
Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.
Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.
Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.
Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?
Tumsifu Yesu kristu.
Kili imani yako ukiwa hai utazikwaje kama ulikataa kuikili?Siku hizi wamejanjaruka hawakatai kuzika hata kama ulikua huhudhurii. Wanachofanya ni kwamba mkienda kuomba huduma ya ibada ya mazishi na kama marehemu alikua sio mchangiaji, basi mnapigiwa mahesabu ya michango yote ambayo alitakiwa kulipa. Kuna jamaa tulilipa laki 6 ndio padri akakubali kuja. Ukiona padri hajaja kabisa ujue ndugu wameshindwa kulipa "deni" la michango!
Inasikitisha sanawana abuse dini siku hizi
Huyo ni mkatoliki kabisa na asemacho ni kweli bila chenga. Hata mm ni mkatoliki naunga mkono home yake. Katoliki ukusanyaji wake wa fedha hata hao TRA wakasome.Ndiyo maana nimesema wewe siyo mkatoliki tena, itakuwa unajilazimisha tu ili uwe huru ubadili dini uwe Muslim, maelezo yako yanakuelezea na kuonyesha imani yako juu ya dini inaelekea upande hupi.
Hii nimeipenda maana rambirambi zinaweza kuokoa jahazi. Ni uchuro kwa ndugu waliobaki kuona ndugu yao hakuzikwa na Padre!Siku hizi wamejanjaruka hawakatai kuzika hata kama ulikua huhudhurii. Wanachofanya ni kwamba mkienda kuomba huduma ya ibada ya mazishi na kama marehemu alikua sio mchangiaji, basi mnapigiwa mahesabu ya michango yote ambayo alitakiwa kulipa. Kuna jamaa tulilipa laki 6 ndio padri akakubali kuja. Ukiona padri hajaja kabisa ujue ndugu wameshindwa kulipa "deni" la michango!
Hujaelewa hoja yangu! Mimi nazungumzia ubinadamu tu. Masuala ya Mungu mimi siyazungumzii maana hakuna aliyekufa akarudi akatusimulia ni nini kipo huko. Nasema tunajua hapa kwetu mtu ukifa unazikwa na Padre au mchungaji. Hii haikuhusu wewe uliyekufa ila wale ndugu zako wanaobaki duniani inakuwa aibu yao. Ni vyema tukajitahidi kutoletea wasiohusika aibu zisizowahusuHayo ya kumwachia Kaisari badala ya kuhoji na kupata logic, hitaji la kuzikwa na padri na mengineyo mengi ndiyo indoctrination tunayozungumzia. Wanufaika walishaanda kauli za kukataza watu kuhoji sana na kujenga hofu kwanza ili wengine wabaki kufuata maelekezo tu.
Unafikiri ni nani ambaye anazuia usihoji au ambaye anatakiwa kujibu hoja zako kwenye dini?[emoji1][emoji1][emoji1]Dini zote hawakupi mwanya wa kuhoji. Yaani mtu mmoja aliyejipa utumishi akisema kasema. And this is how religion was brought to Africa by missionaries to silence any spirit of consciousness. Times have changed na watu wanaanza kuquestion.
Halafu bila tone la aibu wanataka serikali iwaondolee kodi.kimsingi miradi ya kanisa haina faida ya moja kwa moja kwa muumini asilani. Utadikia eti wanajenga shule na wakati huwezi kumpeleka mwanao akasoma bure kwenye shule zao. Na hata hospitali zao kama huna hela hutibiwi na wakati sadaka na michango unatoa. Kwa ufupi, haya madhehebu yana fanya biashara tu. na ni wakati muafaka wa sisi waumini kuamka
Hiyo mbona imefika kwa kuchelewa sana kanisani kwenu
Muda wa sadaka pastor akafungua kapu na kuruhusu watu watoe sadaka, zoezi lilipo kamilika akaja na ajenda nyingine ya mchango kwa ajili ya mradi wa kanisa wa mashine ya alizeti
Pastor kama kawaida na safari hii akawa anawaimbia na pambio ya kuwa motivate huku akiweka kapu jingine kwa ajili ya mchango wa huo mradi
Zoezi lilipokamika pastor akaja na agenda ingine kuwa leo hapo kanisani wametembelewa na mtoto wa miaka 7 anayesumbuliwa moyo, hivyo anahitaji msaada. Akatoa kapu jingine
Hapo ndio nikaona kuanzia waumini mpaka pastor wote hawana akili, nikajiuliza hizi pesa za sadaka si huwa tunaaminishwa kuwa zinaenda kusaidia watoto yatima na wagonjwa?
Imekuwaje leo mtoto mdogo huyu mgonjwa amekuja hapa halafu kanisa limeshindwa kumpatia sadaka ambazo ndio dedicated kwa ajili ya watu wa namna hiyo?
Mtoto alipata mchango wa 30,000 kwenye kanisa lenye waumini 300 kwa misa moja hiyo ilitokana na ulafi wa mchungaji kwasababu mchango wa matibabu ya mtoto ungeanza kabla ya sadaka watu wengi wangemchangia, ila kwakua pastor alikuwa mlafi akaona hizo pesa zote ziingie kwenye mfuko wake
Hapo ulipo quote hamna sehemu kasema hana dini...sasa sijui umefanya kusudi au umepitiwa?Anayelalamika ni huyo ambaye ameshakiri mwenyewe kuwa sio muumini mzuri. Kwanza alishasema hana dini, soma hapa:
Ni waafrika tu ndio nadhani tunawaza hivyo, ukiangalia hizo dini zipo sehemu kubwa tu duniani ila hatuoni wengine kulalamika kwamba imani za mababu zao kuachwa na watu kufuata imani zengine.Dini zote hizi zilikuja na meli na mashua na waliua za kwetu pambaneni nazo
Sorry bro! Unachojaribu kukitetea hapa ni kipi?Huwa nawashangaa watu wanapolalama kwenye institution ambayo kujiunga na kutoka ni hiyari na tena haulazimishwi kutoa chochote.
Kama unaona makanisa yaliyopo hayafai, si kasajili la kwako Wizara ya mambo ya ndani uweke utaratibu unaouona unafaaa?
Huyo jamaa..ni mamluki..sio mkristo fuatiria uzi zake utajua hilo..kaja kuleta hoja za kuvuruga kanisa la Mungu..atabue kutoa ni upendo..muumini wakweli hawezi kuacha kutoa sadaka kanisani.Aya ya mwisho tayari inathibitisha wewe siyo mkatoliki.
Dini ni utapeli au kuna matapeli kupitia mgongo wa dini?Dini ni utapeli na hakuna Mungu
Wavaa kobazi ni bahili hatari..wategemezi kila kitu wafanyiwe na waarabu..hadi tende wanasubiri waletewe na waarabu.Mkuu fikilia Sana imani zingini ni kukomoana tu bora waislamu ya menyewe ni kuswali tu basi.
Hata kuhoji tu hujui..sasa unataka watumie masaa mangapi kama kwa siku wanasali zaidi ya mara 5..hao ndio hawana time management.Waislamu wanajali sana muda yaani wao siku ya Ijumaa wanaingia kama saa saba na ushee lakini saa nane tu tayari walishatoka.
Halafu zile sala zao fupifupi yaani ni Kama kanu saa au dakika 20 tu hao duh.
Time management hapa wapo vizuri.
Hivi si mkawe waislamu nani kawakataza..huwezi ubeza ukristo mana hiyo ndio kanuni yake ya upendonna kujari.Kwakweli waislam ukiugua hata mskitini inasemwa unachangiwa bd kuna wale wa kujitolea kutembelea wagonjwa wasojiweza na kuwapa misaada ya vyakula na dawa
Sasa huyo anayefaidika kwa watu kucontroliwa na dini ni nani?Dini ni scam tu,njia ya kucontrol watu,ndo mana watoto wangu sitaki wawe chini ya mnyororo wa dini wawe huru.