11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.
Warumi 10:11
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Warumi 10:14
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Warumi 10:15
17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Warumi 10:17
Mafungu haya kwa mkristo yanampa WAJIBU .
Wajibu wa kupeleka injili ili watu WAMUAMINI
Ni lazima wahubiri WAPELEKWE.
Wataenda
1. Nauli ili kuwafikisha
2. Na vifaa vya kufanyia kazi
Biblia, vyombo vya sauti , machapisho, n.k
3. Watahitaji chakula na mahali pa kulala.
Hivi vyote na vingine vinahitaji pesa kupitia michango mbali mbali akina baba wajichange, watoto na wa mama. Lkn watoe kadri WALIVYOJALIWA wasitoe nje ya uwezo wao, bali watoe kwa moyo wa kupenda.
Kuweka viwango huenda ni kutafuta bajeti lkn sio kufungia mtu kutoa alichobarikiwa.
Kumfungia mtu huduma kwa kuwa HAJATOA ni roho ya KIPAGANI na USHETANI. Hili huenda ndio TATIZO wala si watoaji.
Kumdai mtu kitu asicho nacho ni kufuru, maana awapaye watu RIZIKI ni MUNGU.
Asalaam aleikum