Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Zamani makanisa yalikuwa yanapata sana misaada toka nje lakini kwa sasa nje hawatoi sana misaada (wanasema mioyo yao kuhusu dini imepoa) so inabidi makanisa yajiendeshe yenyewe. Hapo ndipo uhitaji mkubwa wa hela unapoanzia
Makanisa ya kina Masanja, MC pilipili, Mwamposa, Gwajima n.k nayo unayaweka kwenye hili kundi la kunyimwa misaada?
 
Mimi sijaenda church na ninauhakika asilimia 100 kama Yesu atarudi muda huu, hakika mimi nitatwaliwa (chukuliwa) nipae na Yesu kwenda Mbinguni.

Shida wakristo hatuna Neno la Mungu, Tumesahau kabisa nini kilichofanyika Pale msalabani, na tumeona kama karama za Mungu hutolewa kwa fedha.
 
Viongozi wa Dini watafute kazi za kufanya, waache kutegemea sadaka kuendesha maisha Yao, kazi ya kuingoza ibada malipo yake ni mbinguni.
 
kweli dunia imekwisha!!
yaani muumini wa kanisa unalalamika kutoa sadaka?!
hujui umuhimu wa sadaka kwako binafsi na kwa familia yako?!

Elimu inahitajika juu ya Kutoa Sadaka ktk nyumba za ibada.
 
Kwa ufupi tu, wanapojenga kitegauchumi maanake wanataka kuondokana na michango kutoka kwa waumini, hiyo michango sio ya uhakika sana kama faida itokayo bank, shule, hospital nk
 
Religion is an opium for the poor , you are far better off without it
 
Kwani mkisema sadaka ya maintenance ya kanisa kuna shida gani?
Umesikia jamaa anasema bahasha kila mwezi ya wanandoa na watoto hii ya nini ya kua mkristu tu?
Hapo kuna sadaka ya kwanza na pili kanisani kuna michango ya kwenye jumuiiya mengi tu bado mtu lazima utoe zaka,
Hapo bado kanisa lina miradi kama frame, ukumbi, hospitali,shule,.
Na umechangia ujenzi wa hio miradi,
Sijui unaongea hivo uko kwenye level gani lakini naweza sema 50-60% ya wakatoliki hawatoi hizo pesa kwa kuridhika au moyo mkunjufu wanaumia ila tu hakuna namna
Jaribu kuwasoma waumini utalijua hili.

Ni wakati wa kusema huna kama huna kweli, Na usiache kwenda kanisani bali unaishi maisha ya ukweli ya ukristu.
 
Kwa ufupi tu, wanapojenga kitegauchumi maanake wanataka kuondokana na michango kutoka kwa waumini, hiyo michango sio ya uhakika sana kama faida itokayo bank, shule, hospital nk
Hakuna taasisi yeyote ya kidini inayotufikia kanisa katiliki kwa investment lakini mbona hali inazidi kuwa mbaya?

Wale waislamu wa madhehebu ya Ismailia chini ya kiongozi wao mtukufu Agha Khan ndio wamiliki wa Agha Khan hospital, shule za Agha Khan na Diamond trust bank kama sikosei ni tayari kusahihishwa, lakini wenzetu hawa wananufaika na hivi vitu vinavyomilikiwa na taasisi zao.

Mimi swali langu linabaki palepale, investment zote hizi mkatoliki ananufaika vipi?
 
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.
Warumi 10:11

14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Warumi 10:14

15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Warumi 10:15

17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Warumi 10:17

Mafungu haya kwa mkristo yanampa WAJIBU .
Wajibu wa kupeleka injili ili watu WAMUAMINI

Ni lazima wahubiri WAPELEKWE.
Wataenda
1. Nauli ili kuwafikisha
2. Na vifaa vya kufanyia kazi
Biblia, vyombo vya sauti , machapisho, n.k
3. Watahitaji chakula na mahali pa kulala.
Hivi vyote na vingine vinahitaji pesa kupitia michango mbali mbali akina baba wajichange, watoto na wa mama. Lkn watoe kadri WALIVYOJALIWA wasitoe nje ya uwezo wao, bali watoe kwa moyo wa kupenda.

Kuweka viwango huenda ni kutafuta bajeti lkn sio kufungia mtu kutoa alichobarikiwa.

Kumfungia mtu huduma kwa kuwa HAJATOA ni roho ya KIPAGANI na USHETANI. Hili huenda ndio TATIZO wala si watoaji.

Kumdai mtu kitu asicho nacho ni kufuru, maana awapaye watu RIZIKI ni MUNGU.

Asalaam aleikum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…