Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Waumini wa makanisa wanakamuliwa sio poa, Ila kwa vile ni ridhaa yao hakuna shida kabisa.

*Kujenga makanisa ni kazi ya waumini.
*Kujenga mashule.
*Kujenga hospitali/vituo vya afya/dispensary ni kazi ya waumini.
*Kujenga nyumba za watendakazi wa makanisa.
*Kuwanunulia magari huku sisi tukipiga mihuri.

Bado tutoe zaka na sadaka kwa uaminifu.

Sisi tunapata nini?
*Tunawapeleka watoto wetu kwenye shule tulizojenga wenyewe na ada tunalipa sawa na wengine.

Anyways, mimi siendi kanisani Ila nikipigiwa simu ya kuchangia kitu natoa tu, nilipatwa na msiba hawakunibagua, labda kwa vile hivyo vimchango nashiriki.
 
Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
[qoute]na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.[/quote]
Ni heri jamii inayopata kusikia neno la Mungu walau kwa uchache kuliko ile isiyosikia kabisa.
 
Hiyo mbona imefika kwa kuchelewa sana kanisani kwenu

Muda wa sadaka pastor akafungua kapu na kuruhusu watu watoe sadaka, zoezi lilipo kamilika akaja na ajenda nyingine ya mchango kwa ajili ya mradi wa kanisa wa mashine ya alizeti

Pastor kama kawaida na safari hii akawa anawaimbia na pambio ya kuwa motivate huku akiweka kapu jingine kwa ajili ya mchango wa huo mradi

Zoezi lilipokamika pastor akaja na agenda ingine kuwa leo hapo kanisani wametembelewa na mtoto wa miaka 7 anayesumbuliwa moyo, hivyo anahitaji msaada. Akatoa kapu jingine

Hapo ndio nikaona kuanzia waumini mpaka pastor wote hawana akili, nikajiuliza hizi pesa za sadaka si huwa tunaaminishwa kuwa zinaenda kusaidia watoto yatima na wagonjwa?

Imekuwaje leo mtoto mdogo huyu mgonjwa amekuja hapa halafu kanisa limeshindwa kumpatia sadaka ambazo ndio dedicated kwa ajili ya watu wa namna hiyo?

Mtoto alipata mchango wa 30,000 kwenye kanisa lenye waumini 300 kwa misa moja hiyo ilitokana na ulafi wa mchungaji kwasababu mchango wa matibabu ya mtoto ungeanza kabla ya sadaka watu wengi wangemchangia, ila kwakua pastor alikuwa mlafi akaona hizo pesa zote ziingie kwenye mfuko wake
 
Mkuu, wewe inaelekea ni Mzee wa kamati ya kuhesabu sadaka!
Mtoa Uzi hakusema hataki kutoa Sadaka! Amelalamikia wingi wa sadaka siku hizi! Amelalamikia Kanisa limekuwa kama Pango la Wanyanganyi Yesu aliovunja me,a zao Enzi zake!
Hayo tote uliyoyasema hayakuwepo zamani?? Kanisa lilikuwa linajiendeshaje?? Sadaka ilikuwa ni hiari TU ya Mtu kutoa alicho nacho. Na Huduma za Kanisa ziko pale pale!
Kwa Nini Sasa ukikosa sadaka Moja kati ya rundo zilizopo unafungiwa Huduma za Kanisa, hubatizi ama huzikwi na Kanisa Kwa Sadaka Yako Moja kama ilivyokuwa zamani? SI ndio imegeuza Kanisa 'Pango la Wanyanganyi' anachosema Muumini??
 
Tumsifu Yesu Kristu mpendwa

Nadhani changamoto ipo kwenye ufahamu wa namna ufalme wa Mungu unavyofanya kazi. Sioni tatizo kwako wala mtizamo wako maana ninatambua unachohitaji wewe ni elimu na ufahamu wa jinsi Yesu anavyotenda kazi
Basi tutaanza na neno la Mungu ili iwe rahisi kupokea elimu hii
Tafadhali soma Mathayo 25:14-30
Nitachukuwa mstari 24-26 ili upate kuelewa ufalme wa Mungu unavyofanya kazi
24 - Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
25 - Basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako
.
26 - Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

Hoja yako kwa kanisa haina tofauti sana na hadithi hii
Kwani kinachokuumiza wewe ni kanisa kuwa na michango mingi angali wewe ndio unayefanya kazi.
Naamini kama ungali fahamu vyote ulivyonavyo sio vyako sidhani kama ungelalamika. Kitu kinachotugharimu kibinadamu ni ile hali ya kuamini kwamba hii fedha/mali ni YANGU. Pasi na kufahamu yote tuliyonayo ni matokeo ya upendo wa Mungu kwako. Kibinadamu kuamini falsafa hii ni ngumu sana maana Ipo kiroho wakati tunadhani yote tuliyonayo ni matokeo ya juhudi zetu pekee yetu.
Ukisoma mstari wa 28 utaona ni nini matokeo ya ubinafsi wa mtumwa yule.
Yesu anasema duniani kuna mabwana wawili ambao ni fedha na Mungu. Utachagua mwenyewe wa kumtumikia lakini huwezi kuwatumikia wote kwa pamoja, Ukishindwa kufahamu kama vyote ni mali ya Bwana hakika itakuwa ngumu sana kuachilia yote ulionayo kwa Mungu.

Kwa kumalizia jitahidi sana kujifunza kanuni za Mungu hasa kwa kusoma neno lake ili uongeze maarifa ya kimungu kuanzia namna ya kupata fedha/mali, kutumia na kuzalisha uli usipungukiwe ukamkufuru Mungu, maana kumcha Bwana ndio chanzo maarifa na hekima. Tena Suleiman anasema bora hekima na ujipatie hekima na kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Mwisho kasome Hosea 4 upate kufahamu nini kinachoangamiza Imani. Usilaumu kanisa jilaumu wewe kwa kuwa gizani.

Uwe na jumapili njema ya matawi na nikutakie kwaresma njema.

Tumsifu Yesu Kristu.
 
Yaani wewe na mimi ni mapacha mkuu. Nikienda kanisani mara 1 kwa miaka miwili, basi stimu inakata kwa ninayoyakuta huko. Nimeishia kuwa nasali tu home, nafunga pale inaponibidi (Kama Niko na maombi critical.
 

Kutoa Ni hiari, hulazimishwi
 
Nimetoka kanisani kwangu Lutheran na sadaka tumetoa moja tu ndiyo utaratibu wetu.
 
Siku hizi mamilooo, usipotoa ni kosa kwani wanaangalia registaa, hivyo huduma za kikanisa kama vile ubatizo, ndoa nk haupati.

Kama ninhivyo wanakosea. Maana unamtolea Mungu sio mwanadamu.
 
Waumini hawalalamiki wakifikiri wakitoa pesa watauona ufalme wa mbingu.
Kanisa lina miradi mingi ambayo inaingiza faida kubwa, watu wanaenda kanisani kupata faraja ya Mungu na sio kufanywa kitega uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…