Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mkuu kwa iyo situation ilokukuta haihitaji kufikiria mara 2 kua kanisa linakunyonya.

Sasa kma anaumwa mbona kanisa halimsaidii kitu ila wao ndo wanataka?

Laiti angekua Muislamu huyo waislamu wangejichanga wangemuhudumia badala ya yy kudaiwa huduma

Uislamu ni dini ya haki
Kila mmoja anavutia kwake, apa Alie leta malalamiko ni Christian hakuna sehem hakuna changamoto, hata uko kwenu zipo Tena Sana sema haziwa displayed, ninazijua baadhi lakin siwez ziweka apa eti kushindanisha , big no sisi tubakitu kinaitwa upendo yaan kumpenda Mungu pasipo upeo, personal siwez lalamikia michango kanisan even if waseme nilete my whole salary , I love God personally Ila huwa nasikia watu wanasema michango mingi binafsi sijawah ona kama Kuna michango hata mmoja , kila siku naona ni shamba jipya linatangazwa la kupanda naona fursa ,

Kwa Hy tunatofautiana jinsi tunavo ona ,kwa kifupi tu Kuna watu wanalipa mchango ya mwezi ujao yaaan anatoa anasema kama mwez ujao kutakua na michango mingine ela hii apa kateni ,

Yupo huyo mtu na huwa hataki matangazo mm namjua kwa kua naishi nae,

Karibu kwa yesu
 
😂😂 Hapo kuna kitu sio sawa kama uzi huu unavyonadi. "..Yani ile ya chini pamoja na uzuri wake wanaona sio hadhi yao". Mkuu, Simamia hapo-hapo kidedea.
Kwani walioishi hapo hiyo miaka takribani 6 hawakuwa Mapadre?
Ila narudia tena Ila kama haijitoshelezi kwa mfano Nyumba na Ofisi au Huduma kwa Idadi ya wale wanaoishi hapo e.g. Uwepo wa Masister, Ukumbi wa mikutano, Huduma Mtambuka e.g. Vyoo, Bafu,Stoo, mahali pa chakula au Jiko la ndani n.k. na Eneo lililopo ni dogo au finyu. Kweli inabidi Mjinyime/Mjibane zaidi lakini pia kuwe na maboresho kimawasiliano kwa mfano kutumia neno linaloonesha kudharau au Kubeza e.g. sio Hadhi ya mapadre....sio kauli nzuri. Pia namna nzuri na ya unyenyekevu Kuwahamasisha Waumini ili washiriki kutoa michango kwa Hiari bila vitisho.
Mkuu nyumba za mapadre zinazojengwa siku hizi haziingiliani na huduma nyingine za waamini.
Hiyo ninayosema ipo ndani ya uzio wa kanisa lakini ina uzio wake humo ndani kutenganisha na kanisa
 
Kwani huko nyuma tuliweza vipi kujenga makanisa na mashule kwa sadaka za kawaida bila huu uharamia mpya ulioingia? Ni nini kilichobadirika?

Sisi parokia yetu ilikuwa na vigango vitatu na vyote vimekuwa parokia sasa zenye makanisa makubwa tu, tuliwezaje hayo kwa mwendo wa kawaida bila watu kunung'unika na leo kimebadirika nini?


Watakuambia ni athari za vita ya Urusi na Ukraine [emoji16][emoji16]
 
...To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Hivi ina maana Africa hatukuwa na dini zetu kabla ya kuletewa hizi dini za middle East?
Maana zinawalevya Waafrica kuliko bangi au konyagi.

Huwa tunatunza post za wanafiki, leo atakwambia mimi sina dini, kesho atakwambia mimi Mkatoliki, ili mradi afanye justification ya kile anachotaka kupost wakati huo. Mimi nina server yangu kabisa kwa ajili ya vitu kadhaa, na JF huwa naweka backup mida fulani fulani
 
Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa...
Huyu anafanya biashara ya imani ?
 
Kuhusu hilo nisikubishie ntakuwa nakutenda vibaya ,sema nini me napenda kitu inaitwa logic!
Sawa,lkn logic bila kuwa na Imani ni bure.
Mwanasayansi Albert Einstein aliwahi kusema hivi "Religion without science/Philosophy is blindness, Science/philosophy without religion is lameness".
Akimaanisha kuwa "Dini bila sayansi au Falsafa ni upofu, Sayansi au Falsafa bila dini ni ulemavu".

Kwa hiyo hizo logic zako zisipotanguliwa na imani ni bure hutaweza kuamini.Mt.Thoma wa Akwino ktk kitabu chake SUMMA THEOLOGICA, anasema kuwa ili mtu aweze kuwa imara ktk Imani inatakiwa aamini kwanza ndipo aweze kudadisi,akianza udadisi kabla ya kuamini huyu ni vigumu kuwa na Imani Ali summarize mafundisho yake kwa maneno machache, "Philosophy ancilla theologie".
 
Umeshawahi kufuatwa au kulazimishwa kutoa sadaka? Umeshawahi kusitishiwa huduma yoyote mf ekaristi kitubio n.k Kisaa haujatoa sadaka? Umeshawahi kwenda kusali ukaambiwa hapa wanaingia waumini waliochangia ujenzi wa kanisa pekee? Kanisa uliloenda unajua waliochangia mpaka Leo unaingia bila shida??
Mwenye kukuelewa atakuelewa.
 
Hali ni mbaya kwakweli ....lutheran ndo balaa zaidi
Huku ndo' tunakamuliwa haswa.

Kila saa ni kunyanyuka kwaajili ya sadaka.

Siku nilipochoka ni kumsikia mchungaji wangu (mpya kwa wakati huo) akisema,

"Ni lazima mtoe pesa. Moja ya adhimio nililokuja nalo hapa ni kuongeza mapato ya kanisa. Na mapato hayo ni sadaka zenu."

Siku ile niliufikiria sana ukristo wangu.
 
Nimeona Uzi , kutoa ni kupenda kwako na kama hupendi usitoe maana huto barikiwa ,
Nikiwa natoa najua ipo siku ntavuna na natoa kwa furaha , natoa kwa kadri Mungu alivonijaria , Ila ikizid siwez mind , kazi ya Mungu ni ngumu mno, kama huamini kajaribu
Kutoa Tena kutoa shambani mwa bwana tusijisikie vizuri, 2 Wakorintho 9:6
[6]Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
 
Huwa tunatunza post za wanafiki, leo atakwambia mimi sina dini, kesho atakwambia mimi Mkatoliki, ili mradi afanye justification ya kile anachotaka kupost wakati huo. Mimi nina server yangu kabisa kwa ajili ya vitu kadhaa, na JF huwa naweka backup mida fulani fulani
Ubarikiwe Sana Mtumishi,huyu Matola ni mnafiki sana,amejifanya Mkatoliki ili kuuchafua Ukatoliki, nashukuru kwa kumuumbua.Huyu ni wakala wa shetani.
 
Basi msije kulalamika mnavyokamuliwa huko makanisani mwenu
Anayelalamika ni huyo ambaye ameshakiri mwenyewe kuwa sio muumini mzuri. Kwanza alishasema hana dini, soma hapa:

Hivi ina maana Africa hatukuwa na dini zetu kabla ya kuletewa hizi dini za middle East?
Maana zinawalevya Waafrica kuliko bangi au konyagi.
 
Basi msije kulalamika mnavyokamuliwa huko makanisani mwenu
Ulishawahi kuona post zangu kuhusu kulilalamikia Kanisa Katoliki juu ya taratibu zake??.Mimi ni Mkristo Mkatoliki niliyekomaa kweli kweli,kisiki Cha mpingu kitoke nyuma.
 
Nimeona Uzi , kutoa ni kupenda kwako na kama hupendi usitoe maana huto barikiwa ,
Nikiwa natoa najua ipo siku ntavuna na natoa kwa furaha , natoa kwa kadri Mungu alivonijaria , Ila ikizid siwez mind , kazi ya Mungu ni ngumu mno, kama huamini kajaribu
Kutoa Tena kutoa shambani mwa bwana tusijisikie vizuri, 2 Wakorintho 9:6
[6]Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
AMINA Mtumishi.Mungu akubariki sana.
 
Ikawaje Mkuu?
Kuna mlokore alijitolea kumzika,Tena huyo kijana dada yake wakuzaliwa Ni mudhuliaji mzuri wa kanisani Hadi jumuhia ,

Lakini waligoma kumzika yule kachanga kisa baba Yake na mama yake hawakuwa na ushirikiano na kanisa, Mimi nikasema Sasa Basi siwangekuja kumzika kwa niaba ya shangazi yake maana yeye anaudhulia kanisani vizuri na mambo mengine, lakini waligoma kabisa.,,
Sasa mtoto mchanga wa miezi minne ana makosa gani


Sijui Kama umenielewa,maana nimeandika huku nna mambo mengi
 
Mimi nijuavyo misa ya Kikatoliki isiyokuwa na tukio maalum la sherehe au sakramenti huwa haizidi saa moja na nusu. Umesema mmeinuliwa mara saba kutoka katika benchi, na nafsi yako inashuhudia hayo kwamba uliyosema ni ya kweli, kwamba mmeinuliwa kutoa michango mara saba! Kwangu mimi hiki kitu ni kipya kabisa katika Kanisa Katoliki, na siwezi kukupinga kwa kuwa nafsi yako imetoa ushuhuda huu hadharani, na kwamba ushuhuda huu ni wa kweli. Ninachoweza kusema ni kwamba kama uyasemayo ni kweli kabisa, basi yanahitajika marekebisho makubwa hapo Parokiani kwenu, maana Paroko kuruhusu misa kuwa ndefu kiasi cha kutoa sadaka kwa kuinuka mara saba sio jambo la kawaida
[emoji23][emoji23][emoji23], Umeona eenhh??!!!. Ukute amejitungia mwenyewe ili mradi tu atimize azma yake ya kuchafua Kanisa.Maana maelezo yake ni full ukakasi.
 
Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
Nani kakudanganya! utatengwa, na hata katekista hawezi sogelea mzoga wako.
Ila ukiwa na hela au ni maarufu na huwa huendi kanisani, padri na hata askofu anaweza kuja kwenye ibada ya mazishi nyumbani kwako, kwani sadaka/matoleo yatakua makubwa, na tv zitamwonyesha live.
 
Back
Top Bottom