Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Aya ya mwisho tayari inathibitisha wewe siyo mkatoliki.
 
Mimi ninavyojuwa dini ni swala binafsi la mtu mahusiano yake na Mungu, hizi dini za Abraham sioni kama zinatofautiana, zote zinaongelea kitu kilekile ila tu tafsiri na mapokeo ni tofauti, vitabu ambavyo vipo kwenye biblia baadhi yake vipo kwenye Quran.

Huwezi kuamini nikikwambia huwa naita masheikh kufanya duwa nyumbani kwangu.

Tatizo la upande wa Ukristo sasa hivi viongozi wameamuwa kuwa wanyang'anyi na kuwafanyia uharamia waumini wake pasipo kuwaonea huruma.
Ndiyo maana nimesema wewe siyo mkatoliki tena, itakuwa unajilazimisha tu ili uwe huru ubadili dini uwe Muslim, maelezo yako yanakuelezea na kuonyesha imani yako juu ya dini inaelekea upande hupi.
 
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.

Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!

Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
Mkuu fikilia Sana imani zingini ni kukomoana tu bora waislamu ya menyewe ni kuswali tu basi.
 
Ona waislam duniani kote wanajijua Kuna wale wajahidina na wasio wajahidina hata uende wapi duniani ukikuta muslam atakuwa kundi moja hapo ndio maana warabu wanawajengea misikiti, mda huu wa mwezi mtukufu Kuna misikiti Kila siku inatoa pesa kwa watu wasiojiweza kwenda kununua futari umeona hapo kwanini hawajaingiza ubinafsi na umimi kwenye Imani njoo kwetu Sasa

Kanisa la masanja mkandamizaji
Kanisa la mc pilipili
Kanisa la gwajima
Kanisa la mzee wa upako
Kanisa la mwamposa
Kanisa la kakobe
Na bado Kuna utitiri wa makanisa na bado wanapigana vijembe unasali wapi wewe ukisema kwa MC pilipili wanaanza kusengenya njoo uku yani

ingekuwa kula kitu moto inaruhusiwa uslam unaenda uko sema kiti moto kuacha dah ngumu, maana nishaionja Sasa kuacha ngumu
Hahahaha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu mbona vitu vidogo tu ndugu!
Utatafuta mbadala mfano kuku au mbuzi.
 
Waislamu wanajali sana muda yaani wao siku ya Ijumaa wanaingia kama saa saba na ushee lakini saa nane tu tayari walishatoka.
Halafu zile sala zao fupifupi yaani ni Kama kanu saa au dakika 20 tu hao duh.
Time management hapa wapo vizuri.
 
Mkuu kwa iyo situation ilokukuta haihitaji kufikiria mara 2 kua kanisa linakunyonya.

Sasa kma anaumwa mbona kanisa halimsaidii kitu ila wao ndo wanataka?

Laiti angekua Muislamu huyo waislamu wangejichanga wangemuhudumia badala ya yy kudaiwa huduma

Uislamu ni dini ya haki

Kwakweli waislam ukiugua hata mskitini inasemwa unachangiwa bd kuna wale wa kujitolea kutembelea wagonjwa wasojiweza na kuwapa misaada ya vyakula na dawa
 
Ukifiwa ndipo jinai unaiona
guys ! sikuzote kaa mkijua padre au mchungaji hawezi kukupeleka kwa mbingu( kama waamini mbingu). Matrndo yako ukiwa hai yatakupeleka. Hivyo basi wakuzike wasikuzike hawasaidii chochote. Hata ukizikwa na jiji poa tu
 
Alie design hiyo business model ya church business ni genius ndio maana alihakikisha kuna njia za kukubana ili usiache kutoa hela maisha yako yote.

Kwanza kabisa wanaanzia mbali kwa kukuingiza kwenye system tangu ukiwa mtoto mchanga kwa ubatizo. Pili unaaminishwa kwamba bila kubatizwa kanisani na kupewa sakramenti wewe si mkristo.

Hiyo yote unajengwa kisaikolojia ili uje upigwe vizuri. Baadae unaaminishwa kwamba ili uwe mkristo lazima utoe sadaka na michango yote ili "kueneza injili" na kusaidia jamii wakati kiuhalisia hamna kitu kama hicho.

Mwisho unaambiwa usipotoa michango hautazikwa na kanisa na unatishiwa usipozikwa na kanisa unaenda motoni..!!! Yaani system ipo self contained mwanangu kila kitu ni mumo kwa mumo..!

Yaani mtu unafika mahali unajua kabisa hapa napigwa, ila huna pa kutokea dadeki..!

Na kwenye biblia hamna why watu hawahoji?!
 
Ni vigumu kwa vijana wa kizungu kuwaswaga kama tunavyofanyiwa waumini wa Tanzania.

Uzuri wa wazungu wana reasoning, ndio maana hata walipoleta hii dini walikuwa wanajenga wao makanisa na hospitali target yao ilipotia wakavuta end break.

Sasa ajitokeze mkatoliki hapa leo anieleze miradi mikubwa ya kanisa chuo kikuu cha SAUT mashule, mahospitali mahostel yana faida gani kwetu kama waumini tunaendelea kukamuliwa hivi?

Maana hata Martin Luther alipojitenga na Vaticano na yeye kuna mambo ya kipuuzi yalimkwaza.
kimsingi miradi ya kanisa haina faida ya moja kwa moja kwa muumini asilani. Utadikia eti wanajenga shule na wakati huwezi kumpeleka mwanao akasoma bure kwenye shule zao. Na hata hospitali zao kama huna hela hutibiwi na wakati sadaka na michango unatoa. Kwa ufupi, haya madhehebu yana fanya biashara tu. na ni wakati muafaka wa sisi waumini kuamka
 
Mavuno nadaiwa laki mbili mwisho mwezi wa sita.

Nadaiwa zaka sijarudisha bahasha hii lazima nitoe.

Leo jpili lazima nizame kanisani na sadaka 3.

Nadaiwa laki mbili mchango wa gari la Paroko...nili-pleadge.

nisipotekeleza haya nitaonekana sio mkristo
ukristo wako uko na muumba wako na sio mwanadamu mwenzio. Padre/ mchungaji ni mwanadamu kama wewe , ana mahitaji kama ww tena wanaspend hata kukuzidi. Ni ww kuamua kuwa kitegauchumi chao au kujikomboa.
 
Kuna ile ya kuwataka waumini waliofiwa na wapendwa wao eti watoe sadaka kubwa kubwa kadri wawezavyo kama kikokotoo cha kuwawezesha hao wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kupata ahueni ya maisha huko kaburini. Yaani mimi hii haijawahi kuniingia akilini kabisa.
huu ni uongo na misconception. Kristo alipokufa msalabani aliwakomboa wanadamu wote. Pesa yako haiwezi kumwokoa mtu aliyekwisha kufa, wake up.
 
Mkuu, hata ukitoa unaweza usipewe huduma vilevile!

Mimi mama yangu mzazi alikua kiongozi wa jumuia huko kijijini na alikua mtoa sadaka asie na kifani, shughuli zote za ujenzi wa kanisa alishiriki kikamilifu kwa maisha yake yote mpaka amezeeka.

Bahati mbaya akaja kupata tatizo la kiafya ambalo limemuweka kitandani zaidi ya miaka 10 sasa. Cha ajabu eti kila mwaka analetewa bahasha ya zaka na kanisa linatishia kwamba akifa halitamzika kama sisi watoto hatutakua tunatoa hela za kwetu na zake!

Sasa mimi najiuliza, mtu ambae amelala kitandani hilo fungu la 10 analitoa wapi? Tangu amelala kitandani, kanisa limemsaidia vipi? Michango yote aliyochanga tangu akiwa binti mdogo mpaka sasa ni mzee, haijatosha tu? Ni mpaka tone la mwisho??
Mkuu pole sana kwa yaliyomkuta bi mkubwa! Tatizo linakuja pale mtu mweusi anapojivika kazi ya Mungu na kujiona bira kuliko mwenzake. Hebu jiulize hivi sadaka yako unayotoaga kanisani ungekuwa anawasaidia wasiojiweza ni wapi ungepata baraka zaidi? These churches are just institutions established by human beings to fullfull thier objectives. Time to wake up
 
Hiyo sio sbb, sadaka za Jpili peke yake zinatosha sana, na kanisa ina miradi mikubwa mingi sana, iweje ikamue waumini kiasi hicho.

Kwnn kanisa liwe na matumizi makubwa hivyo, kisa ni nn? Yesu hakuwa na hayo yote, ukiona hivyo ni binadamu wanakula fedha hizo na kuzitumia sbb zinapatikana bure bure.

Mimi kanisani naenda wakati wa Pasaka na Christmas tu, siku nyinginezo nasali kwangu na familia yangu, makanisa yamekuwa tofauti kabisa, ni kukusanya fedha na michango isiyoisha, imekuwa biashara ya uhuni sana, narudia, Yesu Kristo hajawahi kuwa hivyo, full stop
U nailed it
 
Back
Top Bottom